08/06/2022
WILAYA YA CHAKE CHAKE
SABRINA KHAMIS JUMA
AFISA HABARI
WILAYA YA CHAKE CHAKE
Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Bw. Abdalla Rashid Ali amekabidhi Nyumba za makaazi kwa watu wenye Mahitaji Malumu katika Maeneo tofauti ndani ya Wilaya hiyo
Nyumba hizo zimwjengwa kupitia Taasisi ya IFRAJ ZANZIBAR FOUNDATION kwa lengo la kuwasaidia Jamii ambazo zinahitaji msaada.Waliokabidhiwa nyumba hizo Bw.Ali Khamis Kombo Mkaazi wa Mfikiwa na Bi Rehema Mzee Bakari mkaazi wa Chanjamjawiri.
Mkuu huyo amezitaka Familia kuzitunza na kuziboresha ilo ziweze kudumu muda mrefu ili lengo la kujengwa nyumba kufaidika kizazi na kizazi
Aidha katibu Tawala wa wilawa hiyo Bw. Suleiman Hamadi Suleiman amewashukuru tasisi ya IFRAJI ZANZIBAR FOUNDATION kwa kuiunga mkono serekali na kujenga nyumba hizo kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum
Kwa pamoja Familia hizo zilizokabidhiwa Nyumba huzo wameishukuru serekali pamoja na Tasisi ya IFRAJ ZANZIBAR FOUNDATION kwa msaada huo na wameahidi kuzitunza na kuzienzi nyumba hizo
.....MWISHO......
03/03/2022
WILAYA YA CHAKE CHAKE
NA SABRINA KHAMIS
AFISA HABARI
WILAYA YA CHAKE CHAKE
Mkuu wa Wilaya ya chake chake Bw. Abdalla Rashid Ali amefungua mafunzo ya kuwawezesha kiutendaji kwa Walimu wakuu wa Maandalizi pamoja na Tutu huko katika skuli ya Madungu sekondari .
Mkuu huyo amewataka Walimu kuyatumia vizuri mafunzo hayo na kuwa mfano mzuri katika Jamii na kuacha tabia ya kuwazuia wanafunzi pindi ikiwa mwanafunzi atakosa yunifomu jambo ambalo linarejesha nyuma wanafunzi na kuwakosesha haki zao za msingi kwa wanafunzi hao
Pia Mkuu huyo amewataka Walimu kuongeza mashirikiano baina ya walimu na wazazi na kushiriki katika sensa ya watu na makazi ili waweze kuto tarifa sahihi
Kaimu Afisa mdhamini wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Pemba Nd M***a Khamis M***a amesema dhamira ya mafunzo hayo ni kubadilisha fikira na uwelewa na uwezo wa kuwasimamia wanafunzi wa Maansalizi pamoja na Tutu ili kuweza kufikiwa lengo lililo kusudiwa na Serekali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kwa upande wa Walimu hao wamemshukuru Mkuu wa Wilaya pamoja na uongozi wake kwa mafunzo hayo na wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo hayo na kuwa mabalozi wazuri kwa walimu wengine ambao hawakubatika kupata mafunzo hayo.
.....MWISHO..
04/02/2022
WILAYA YA CHAKE CHAKE
MKUU wa Wilaya ya Chake chake Bw. Abdalla Rashid Ali Pamoja na Katibu Tawala Bw. Omar Juma Ali wametembelea eneo ambalo linategemewa kujengwa kiwanda cha kuchakata madaga ikiwa ni juhudi za serekali ili kukuza uchumi wa bluu na kuzungumza na Wajasiriamali hao pamoja na Wanakijiji wanaofanya shughuli hiyo huko Ndagoni Wesha
02/02/2022
WILAYA YA CHAKE CHAKE
Na SABRINA KHAMIS Juma
AFISA HABARI
WILAYA YA CHAKE CHAKE
MKUU wa Wilaya ya
chake chake Bw.Abdalla Rashid Ali amewataka walimu pamoja na k**ati za skuli kuongeza mashirikiano ya pamoja ili kutatua changamoto zilizopo ndani ya skuli hiyo.
Ameyasema hayo huko katika skuli ya Mandalizi ilioko Pujini Mtimbu alipokwenda kuwatembelea kwa ajili ya kusikiliza changamoto zinazowakabili skuli hiyo
Mkuu huyo amesema jitihada za makusudi zinahitajika katika kuongeza mashirikiano kati ya walimu wazazi na k**ati ya skuli hiyo kwa ajili ya kupeleka mbele maendeleo ya kielimu.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Skuli Bi.Maimuna Abasi Omar amesema changamoto zinazo wakabili skulini hapo ni uhaba wa Walimu ,uharibufu wa miundo mbinu ya skuli ikiwemo wananchi kufunga Mifugo katika eneo hilo pamoja na umbali wa skuli jambo ambalo linawapa hofu wazazi kwa watoto wao kutokana na usalama kwa watoto hao.hivyo amemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa kufika skulini hapo na wa na imani ya kupatiwa ufumbuzi changamoto zao .
Mwisho Mkuu huyo ya amewataka
Wanajamii kutunza miundombinu ya skuli hiyo ili iweze kudumu na kufaidika vizazi na vizazi.
Na kuzipatia ufumbuzi wa changamoto hizo ili kuwaondoshea ugumu walimu hao .
....MWISHO....
21/12/2021
WILAYA Ya chake chake
Na Iptisam Kassim Mohd
AFISA HABARI
WILAYA YA CHAKE CHAKE
Katibu Tawala Wilaya ya chake chake Bw.Omar Juma Ali amefungua mafunzo ya siku tatu ya uaandaji na utumiaji wa mfumo wa masjala mtandao huko katika ukumbi wa
wa Nyaraka Chake chake
Katibu huyo amewataka wafanya kazi hao kutunza siri za maofisi pamoja na kazi zao na kufata misingi ya kazi zao zinavowaelekeza pamoja na kutunza faili hizo.
Aidha Katibu Tawala huyo amewapongeza wafanyakazi hao kwa kujitolea na kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kutunza siri na kumbukumbu za ofisi hiyo .
Msimamizi wa wa Taasisi hiyoya Nyaraka Pemba Bw. Kombo khamisi Bakari amewataka wafanya kazi kuongeza juhudi katika utendaji wao wa kazi kwani wao ni kiungo muhimu sana katika Ofisi zao.
Kwa pamoja wafanyakazi hao wakitoa shukurani zao wamesema wamefarijika kuwa miongoni mwa watakaopatiwa mafunzo hayo na wana imani mafunzo hayo yataongeza uelewa kupitia mfummo huo hivyo wameeahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo na kuwajibika ipasavyo.
..... MWISHO ........
26/11/2021
WILAYA YA CHAKE CHAKE
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Bw. Abdala Rashid Ali pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Omar Juma Ali wamefanya ziara ya kutembelea shamba la migomba na mihogo huko katika Kijiji cha Vitongoji na kuona eneo ambalo limeombwa kwa ajili ya ufugaji samaki
23/11/2021
WILAYA Ya Chake Chake
Na Iptisam Kassim Mohd
AFISA HABARI
WILAYA YA CHAKE CHAKE .
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Bw.Abdala Rashid Ali Amezindua Skuli ya ELITE NURSERY SCHOOL ilioko Chanjaani nijia Air Port kwa ajili ya kuanza kupokea Wanafunzi mara tu bada ya ufunguzi huo
Mkuu huyo amepogeza Bi. Shuwekha Saidi Rashid kwa mamuzi na uzalendo aliouonyesha kwa kuwekeza katika sekta ya Elimu na kuona kuna uhitaji wakufungua Skuli katika eneo hilo,hivyo amewataka Wanajamii kwa ujumla kuitumia Skuli hiyo kwa kuwapeleka watoto wao kwa ajili ya kujipatia elimu na kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.
Nae Katibu Tawala Omari Juma Ali amewataka Wana jamii hao kushirikiana na walimu na kwa kuwasimamia watoto hao katika kujipatia elimu kwani kuwepo kwa Skuli katika eneo hilo kutasaidia kupunguza masafa kwa watoto wao.
Hata hivyo Mmliki wa Skuli hiyo ambae pia ni Mwalimu Mkuu katika Skuli hiyo Bi..Shuwekha Said Rashid amewahakishia Wana jamii hao kuwa Elimu itakayo tolewa hapo ni nzuri na mazingira yapo vizuri kwa watoto na uagalifu muzuri kwa watoto wao.
Hata hivyo Mkuu huyo amewataka wana chanjaani kuitunza Skuli hiyo,na kuongeza mashirikiano katika kutokomeza uzalishaji na wizi badala yake kuishi kwa amani na kuonesha upendo kati yao.
.....MWISHO........
15/11/2021
WILAYA YA CHAKE
NA IPTISAM KASSIM MOHD
AFISA HABARI
WILAYA YA CHAKE CHAKE
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Bw Abdalla Rashid Ali amefika katika kijiji cha Ziwani Kiwapwa kusikiliza changamoto za wana kijiji hao kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi.
Kwa pamoja Wana jamii hao wameiomba Serekali kumaliziwa Skuli yao ya Tutu pamoja na huduma ya maji safi na salama kwani kwa sasa imekuwa ni changamoto kubwa kwao na ni la muda mrefu sasa.
Mkuu wa Wilaya huyo amewahidi kwa kuzipatia ufumbuzi wa changamoto zao,hivyo anewataka Wanajamii hao kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi chote cha ufatiliwaji ya changamoto hizo.
Aidha Mkuu huyo amewataka Wanajamii hao kuongeza mashirikiano kwa pamoja ili kupambana na uzalilishaji wa watoto na kuendelea kudumisha amani na utulivu pamoja na upendo katika kipindi chote cha kusubiri
....... MWISHO
15/11/2021
WILAYA Ya CHAKE CHAKE
Na SABRINA KHAMISI
AFISA HABARI
WILAYA YA CHAKE CHAKE.
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Bw Abdalla Rashid Ali amekabizi Nyumba ya Makaazi kwa ndugu Said Roben Solilo bada kukamilika kwa ujenzi ya nyumba hio iliojengwa na jumuia ya WISH FOUNDATION huko katika kijiji cha Ziwani Wilaya ya Chake Chake .
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya hiyo Bw.OMAR Juma Ali amewashukuru Wana jumuia hao kwa kufika Kisiwani Pemba kwa ajili ya kutoa msaada kwa Jamii zinazohitaji mahitaji maalumu,hivyo ameahidi kwa Uongozi wa Wilaya kutoa mashirikiano yao na ametoa wito kwa wawekezaji na Jumuiya nyengine zinazotaka kuwekeza Kisiwani Pemba milango nipo wazi na Serikali ipo tayari kushirikiana nao.
Jumuiya ya WISH FOUNDATION ni Jumuiya inayotoa msaada kwa Watu wenye mahitaji maalumu, na wamefadhili Nyumba hiyo baada ya kuchakaa na kuanguka .
Nae ndugu Said Roben Solilo ameushukuru Uogozi wa Wilaya pamoja na Jumuiya hiyo kwa kumjengea nyumba hiyo, hivyo ameahidi kuitunza ili kuishi muda mrefu
Mwisho Mkuu huyo amewataka Wana jamii wa Ziwani kuishi kwa upendo na kuongeza mashirikiano katika kupambana na vitendo vya uzalilishaji katika Jamii
....... MWISHO
11/11/2021
WILAYA Ya CHAKE
Na IPTISAM KASSIM MOHD
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Bw Abdala Rashid Ali amewataka Wanajamii wa kijiji cha Matale Mlemele kuutumia mradi huo pindi utakapokamilika kwa ajili ya kujipatia manufaa na kukuza kilimo .
Ameyasema hayo mara tu alipofika katika eneo la mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji maji kwa ajili ya kuangalia hali halisi ya mradi huo unavoendelea.
Mkuu huyo amewataka wakandarasi wanaoshughulikia mradi huo kufanya juhudi za haraka kwa ajili ya kuboresha mashamba hayo, ili Wanajamii waweze kuyatumia Mashamba hayo na kufaidika na mradi huo ,
Kwa upande wake Ijinia anaesimsmia Mradi huo Salum Mohd Juma amewataka Wanajamii kua na imani na mradi huo na amemuomba sheha wa shehia hiyo kuzidi kutoa taluma ya kilimo hicho kwa Wanajamii hao.
Aidha Mkuu huyo amewataka Jamii kudumisha amani na utulivu pamoja na mashirikiano katika kipindi chote cha kuboreshwa mashamba hayo ili lengo la mradi huo uweze kufikiwa na ulete tija pamoja na maendeleo .
..... MWISHO
26/10/2021
WILAYA YA CHAKE CHAKE
Na IPTISAM KASSIM MOHD
Walimu wa madrasa
wametkiwa kuongeza mashirikiano na Jamii ili kurekebisha tabia za vijana ili kujenga Jamii iliyokuwa bora.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Chake chake bw. Abdalla Rashid Ali alipokutana na Walimu wa Madrasa katika kikao chao cha Jumuiya ya Maendeleo ya Madrasa Chake chake.
Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza kuwa kutengenea kwa Jamii kutasaidia sana kuimarisha usalama kwa Taifa. Kwani jamii yenye maadili mema itaepukana na vitendo viovu k**a vile utumiaji wa dawa za kulevya, Wizi wa Mifugo na Mazao, Rushwa, Udhalilishaji na vitendo mbali mbali visivyo kubalika katika jamii.
Aidha, Bw. Abdalla ametoa wito kwa watu wenye uwezo na kujitolea kwa kuangalia uimarishaji wa madrasa pamoja na walimu na sio kuangalia ujenzi wa misikiti tu ,jambo ambalo linapelekea kukosa waumini wa kuifanyia ibada na hata wakijitokeza wengi wao hawafikii lengo la ibada hio kwa kutokuwa na elimu sahihi ya kila ibada.
Kwa upande wao Wanajumuiya hio ya Maendeleo ya Walimu wa Madrasa Chake wameahidi kutoa mashirikiano miongoni mwao, na taasisi mbali mbali za Serikali katika kuiokoa jamii kuingia katika janga la vitendo viovu ambapo ni hatarishi kwa amani ya Nchi yetu.
........MWISHO.......
24/10/2021
WILAYA YA CHAKE CHAKE.
NA IPTISAM KASSIM MOHD
Mkuu ya Mkoa kusini Pemba Mh.Mattar Masoud Zahor amewataka Wanakijiji wa Kukuchini kuchukua tahadhari pale wanapotumia daraja liliopo kijijini hapo kutokana na uchakavu wa daraja hilo.
Mkuu wa Mkoa huyo amewataka Wanajamii wawe makini wakati wakilitumia daraja hilo kwani kwa sasa daraja hilo linahitaji marekebisho kutokana uchakavu,hivyo Serikali ya Mkoa ipo mbioni kulifanyia ukarabati daraja hilo ili isiwe kikwazo katika kutekeleza shughuli zao za kuleta maendeleo.
Aidha Mkuu huyo amewaomba Wanakijiji hao kuwa wastahamilivu katika kipindi choote cha matengenezo na ameahidi kutumia Wakandarasi wazuri kwa ajili ya kuboresha Daraja hilo.
Kwa pamoja Wanakiji ji hao wamemshukuru Mkuu huyo kwa kwenda na kuweza kusikiliza changamoto na watashirikiana na wakandarasi kwa hali na mali wakati waujenzi ya daraja hilo.
Daraja hilo lipo katika Kijiji cha Kukuchini,Shehia ya Michungwani ambalo linaunganisha jumla ya Vijiji vitatu (3) limejengwamwaka 1961 hadi sasa halijawahi kufanyiwa marekebisho.
...... MWISHWO