13/05/2026
Mapipa 80 ya Lita 16,048 za kemikali za Cyclohexanone zilizokamatwa jijini Dar es salaam. Kemikali hizo ziljingizwa nchini na kampuni ya Kinglion Investment Company LTD kinyume na matakwa ya mifumo ya udhibiti ikiwemo kibali kutoka Mamlaka husika.
13/05/2026
Magari aina ya scania yaliyokamatwa yakiwa yamebeba kemikali aina ya Extra Neutral Alcohol (ENA) zenye ujazi wa lita 50,000.
11/05/2026
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Ziwa imehitimisha zoezi la utoaji elimu Kinga dhidi ya dawa za kulevya Wilayani Mbogwe na kufanikiwa kuwapa elimu waumini wa Kanisa lawadventist Wasabato, Maafisa usafirishaji(Bodaboda)pamoja na askari wa Jeshi la Magereza pamoja na wafungwa wa gereza la Kanegele Masumbwe.
Aidha Mkuu wa gereza hilo SP Maginga ameishukuru Mamlaka kwa kuona kuna umuhimu wa kuwapa elimu wafungwa na kuahidi ataendelea kushirikiana na Mamlaka katika mapambano ya dawa za kulevya ikiwemo kutoa taarifa za wanaojihusisha na dawa hizo kupitia namba ya bure 119
11/05/2026
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Ziwa imehitimisha zoezi la utoaji elimu ya kinga dhidi ya dawa za kulevya Wilayani Mbogwe ambapo waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Miembeni walipatiwa elimu kuhusu athari za dawa za kulevya na namna ya kujikinga nazo.