dcea_tz

dcea_tz

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from dcea_tz, Government Organization, 8 Kivukoni Road, Dar es Salaam.

The Drug Control and Enforcement Authority (DCEA) has the functions of define, promote, coordinate, and implement all measures geared towards control of drugs, drug abuse and trafficking in drugs.

Photos from dcea_tz's post 13/05/2026

Mapipa 80 ya Lita 16,048 za kemikali za Cyclohexanone zilizokamatwa jijini Dar es salaam. Kemikali hizo ziljingizwa nchini na kampuni ya Kinglion Investment Company LTD kinyume na matakwa ya mifumo ya udhibiti ikiwemo kibali kutoka Mamlaka husika.

13/05/2026

Kwa upande wa dawa za kulevya, Mamlaka ilifanya operesheni katika mikoa ya Dodoma, Mtwara, Njombe, Ruvuma, Kilimanjaro, Arusha, Dar es Salaam, Morogoro na Mwanza na kukamata bangi tani 5.733, mirungi tani 1.67, he**in gram 48.23, co***ne gramu 113.35 na kuteketeza ekari 38.5 za mashamba ya bangi. Aidha, magari manne (04) pamoja na pikipiki 14 zilizohusishwa na biashara hiyo haramu zilikamatwa huku watuhumiwa 84 walikamatwa kusuana na ukamataji huo.

Photos from dcea_tz's post 13/05/2026

Magari aina ya scania yaliyokamatwa yakiwa yamebeba kemikali aina ya Extra Neutral Alcohol (ENA) zenye ujazi wa lita 50,000.

13/05/2026

Mamlaka itaendelea kushirikiana na taasisi za kitaifa na kimataifa kuimarisha udhibiti wa kemikali bashirifu zinazoweza kutumika katika utengenezaji wa dawa za kulevya. Hivyo, wadau wote wa kemikali wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. Kinyume na hapo, hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

13/05/2026

Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani Sura 182, usafirishaji wa kemikali unahitaji kufuata taratibu maalum ikiwemo kuwa na vibali vya kuingiza na kusafirisha. Matumizi ya vibali vya kughushi pamoja na utoaji wa taarifa za uongo kuhusu matumizi yaliyokusudiwa ya kemikali husika ni kosa kisheria.




13/05/2026

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kushirikiana na pamoja na imefanikiwa kukamata lita 66,048 za kemikali bashirifu zilizoingizwa na kusafirishwa nchini kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 13, 2026 katika Makao Makuu ya DCEA jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema kemikali zilizokamatwa ni Cyclohexanone pamoja na Extra Neutral Alcohol (ENA).




Photos from dcea_tz's post 13/05/2026

TAARIFA KWA UMMA

12/05/2026
Photos from dcea_tz's post 11/05/2026

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Ziwa imehitimisha zoezi la utoaji elimu Kinga dhidi ya dawa za kulevya Wilayani Mbogwe na kufanikiwa kuwapa elimu waumini wa Kanisa lawadventist Wasabato, Maafisa usafirishaji(Bodaboda)pamoja na askari wa Jeshi la Magereza pamoja na wafungwa wa gereza la Kanegele Masumbwe.

Aidha Mkuu wa gereza hilo SP Maginga ameishukuru Mamlaka kwa kuona kuna umuhimu wa kuwapa elimu wafungwa na kuahidi ataendelea kushirikiana na Mamlaka katika mapambano ya dawa za kulevya ikiwemo kutoa taarifa za wanaojihusisha na dawa hizo kupitia namba ya bure 119

Photos from dcea_tz's post 11/05/2026

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Ziwa imehitimisha zoezi la utoaji elimu ya kinga dhidi ya dawa za kulevya Wilayani Mbogwe ambapo waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Miembeni walipatiwa elimu kuhusu athari za dawa za kulevya na namna ya kujikinga nazo.

09/05/2026

Kataa Dawa za Kulevya, Timiza Malengo Yako

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


8 Kivukoni Road
Dar Es Salaam
S.L.P80327

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30