NemcTanzania

Directions Website

NemcTanzania Karibu katika ukurasa rasmi wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC). Pamoja tulinde na kutunza mazingira kwa maendeleo endelevu.

19/10/2026

KUTANA NA SHUJAA IRENE ALIYEJITOLEA MUDA WAKE NA NGUVU ZAKE KUSAFISHA MAZINGIRA AMBAYO WEWE UNAYACHAFUA KWA MAKUSUDI KABISA

🌳

18/10/2026

ZIARA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAJI NA MAZINGIRA ILIPOTEMBELEA DAMPO LA PUGU NA MTO NG'OMBE

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAJI NA MAZINGIRA YAKAGUA HALI YA MAZINGIRA DAMPO LA PUGU NA MTO NG’OMBE DAR ES SALAAMKamat...
17/10/2026

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAJI NA MAZINGIRA YAKAGUA HALI YA MAZINGIRA DAMPO LA PUGU NA MTO NG’OMBE DAR ES SALAAM

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Oktoba 17, 2026, imefanya ziara ya kukagua hali ya mazingira katika Dampo la Pugu Kinyamwezi na Mto Ng’ombe, Dar es Salaam, kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, Septemba 18, 2026, kuhusu hatua za kukabiliana na changamoto za kimazingira katika maeneo hayo.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Prof. Pius Zebhe Yanda (Mb) ameelekeza kuwepo kwa mpango madhubuti wa kudhibiti na kusimamia Dampo la Pugu na kusisitiza umuhimu wa kutathmini afya za wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka uzio ili kuhakikisha makazi ya Wananchi hayasogei karibu na dampo hilo

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa ameeleza kuwa Serikali haina budi kuweka mwekezaji atakayeshughulikia uchakataji wa taka katika Dampo la Pugu, hatua inayotarajiwa kuboresha usimamizi wa taka na kupunguza athari za kimazingira kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo.

Aidha, ameielekeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kushirikiana kwa karibu na taasisi zote zinazohusika, ikiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ili kuhakikisha mradi wa dampo hilo haukwami.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mhe. Albert Chalamila, akiwasilisha taarifa fupi kuhusu hali ya Mazingira amesema Mkoa wa Dar es Salaam una takribani kilomita za mraba 1300 na watu zaidi ya Milioni tano na laki tatu kwa mujibu wa sensa ya Mwaka 2022 hali inayopelekea uzalishaji mkubwa wa taka kwa siku na kutokana miundombinu kupelekea kiwango kidogo cha taka kupelekea dampo.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeshiriki mkutano wa 6 kuhusu usimamizi wa taka zinazotok...
17/10/2026

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeshiriki mkutano wa 6 kuhusu usimamizi wa taka zinazotokana na bidhaa za kielektroniki, uliofanyika Diani, Kaunti ya Kwale Nchini Kenya kuanzia tarehe 15 hadi 16 Oktoba, 2026.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Kituo cha WEEE (WEEE Centre) lililokuwa na Kauli Mbiu "From Policy to Practice", lilijadili kwa kina namna ambavyo nchi mbalimbali zinaweza kushirikiana ili kuimarisha usimamizi wa taka hizo.

Aidha, kupitia mkutano huo washiriki walipata fursa ya kujionea na kujifunza teknolojia na mifumo ya kisasa ya kurejeleza, kuteketeza, kurekebisha (refurbish), kutumia vinginevyo (repurpose) taka za kielektriniki.

JUKWAA LA USIMAMIZI WA BAHARI LAHITIMISHWA RASMI📌NEMC NA IUCN zasisitiza Ushirikiano wa Uhifadhi wa BahariBaraza la Taif...
17/10/2026

JUKWAA LA USIMAMIZI WA BAHARI LAHITIMISHWA RASMI

📌NEMC NA IUCN zasisitiza Ushirikiano wa Uhifadhi wa Bahari

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na International Union for Conservation of Nature (IUCN) zasisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika uhifadhi wa bahari na rasilimali zake ili kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali hizo, hasa katika muktadha wa Uchumi wa Buluu na kulinda mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Msisitizo huo umetolewa wakati wa kuhitimisha Jukwaa la Taifa la Usimamizi wa Bahari (Tanzania Ocean Governance Forum), lililofanyika katika ukumbi wa Ramada Hotel, jijini Dar es Salaam Oktoba 16, 2026. Katika jukwaa hilo, wadau walijadili fursa za Uchumi wa Buluu, zikiwemo utalii, maendeleo ya teknolojia ya kibayoteknolojia, kaboni ya buluu na nafasi ya uhifadhi wa mazingira katika kukuza uchumi wa taifa.

Majadiliano hayo yalisisitiza umuhimu wa kuimarisha uratibu baina ya taasisi, kubadilishana ujuzi na uzoefu, pamoja na kuwezesha tafiti za kimkakati za bahari na maeneo ya pwani. Ushirikiano huo ni muhimu katika kuongeza uelewa wa pamoja na kuboresha maamuzi yanayohusu usimamizi endelevu wa rasilimali za bahari.

Aidha, wadau walisisitiza umuhimu wa kushirikisha jamii katika kupanga na kutekeleza miradi ya Uchumi wa Buluu, kuelekeza tafiti katika utekelezaji wa Dira za Maendeleo za Tanzania Bara na Zanzibar. Vilevile, ilielezwa kuwa mamlaka za serikali za mitaa zinapaswa kujengewa uwezo ili ziwe tayari kutumia fursa zinazotokana na masoko ya kaboni, huku zikihakikisha kuwa juhudi za uhifadhi wa mazingira zinawanufaisha wananchi.

Kwa ujumla, jukwaa hilo limeonesha umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi na wadau katika kulinda mazingira ya bahari na pwani. Pia, msisitizo uliwekwa katika kufuatilia utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa ili kuhakikisha kuwa yanatekelezwa kwa vitendo na kuchangia maendeleo endelevu ya Uchumi wa Buluu, sambamba na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2050 na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2050.

NEMC NA IUCN ZAKUTANISHA WADAU KUJADILI MUSTAKABALI WA USIMAMIZI ENDELEVU WA BAHARI TANZANIABaraza la Taifa la Hifadhi n...
15/10/2026

NEMC NA IUCN ZAKUTANISHA WADAU KUJADILI MUSTAKABALI WA USIMAMIZI ENDELEVU WA BAHARI TANZANIA

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (IUCN), limeandaa mkutano wa Tanzania Ocean Governance Forum, unaofanyika Oktoba 15–16, 2026, katika ukumbi wa Ramada Hotel, Dar es Salaam. Mkutano huo unawakutanisha wadau kutoka taasisi za serikali na zisizo za kiserikali kujadili usimamizi na utawala endelevu wa bahari nchini Tanzania.

Mkutano huo unaongozwa na kaulimbiu isemayo “Towards Sustainable Governance in Tanzania: Strengthening Collaboration, Policy and Action”, inayosisitiza kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi, kuboresha utekelezaji wa sera na kuchukua hatua madhubuti katika uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za bahari, sambamba na kukuza uchumi wa buluu.

Washiriki wa jukwaa hilo wanatoka katika taasisi mbalimbali, zikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais (VPO), Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Zanzibar (ZAFIRI), MOBEF, Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA), ZEMA, pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine wa mazingira ya baharini. Ushiriki wao unalenga kuimarisha uratibu na kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa rasilimali za bahari.

Katika mkutano huo, mada kuu tatu zimejadiliwa, ambazo ni hali ya utekelezaji wa sera na mipango ya uchumi wa buluu, mipango ya matumizi ya maeneo ya bahari (Marine Spatial Planning – MSP) pamoja na uvuvi na uchumi wa buluu. Majadiliano hayo yanalenga kuimarisha utekelezaji wa sera, kuratibu matumizi ya maeneo ya bahari na kukuza sekta ya uvuvi kwa kuzingatia uhifadhi wa mifumo ikolojia na matumizi endelevu ya rasilimali.

Mgeni rasmi katika mkutano huo ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Bw. Zahor Kassim. Kupitia jukwaa hili, NEMC na IUCN zinalenga kuimarisha ushirikiano wa wadau, kubadilishana maarifa na kuwezesha maamuzi na hatua zinazozingatia sera na uhifadhi wa mazingira ya baharini, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya kikao na Jeshi la Polisi kikosi cha wanamaji kujad...
15/10/2026

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya kikao na Jeshi la Polisi kikosi cha wanamaji kujadili na kuweka mpango kazi wa mashirikiano ya kukabiliana na athari za kimazingira zinazoweza kutokea kabla, wakati na baada kipindi cha mvua za El niño

NEMC YAHIMIZA SOKO LA KABONI LENYE UADILIFU KWA MAENDELEO ENDELEVU YA TANZANIAMkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifa...
14/10/2026

NEMC YAHIMIZA SOKO LA KABONI LENYE UADILIFU KWA MAENDELEO ENDELEVU YA TANZANIA

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Immaculate Sware Semesi, anasisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi wa miradi ya kaboni ili kuhakikisha inalinda mazingira, inavutia uwekezaji na kuwanufaisha wananchi.

Akishiriki katika Mkutano wa Carbon Market Africa Summit 2026, uliofanyika Kigali Rwanda, Mkurugenzi Mkuu anasisitiza kuwa Tanzania ina fursa kubwa ya kukuza soko la kaboni kupitia uhifadhi wa misitu, mikoko, mifumo ikolojia ya bahari, urejeshaji wa ardhi na usimamizi bora wa taka.

NEMC ina jukumu muhimu katika usimamizi wa mazingira na ufuatiliaji wa uzingatiaji wa matakwa ya mazingira katika miradi ya maendeleo, ikiwemo miradi ya kaboni, kwa mujibu wa sheria na mamlaka yake.

NEMC inahimiza uwazi, uwajibikaji, ufuatiliaji wa matokeo ya kimazingira na ushirikishwaji wa jamii ili kuhakikisha kuwa miradi ya kaboni inachangia kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi bila kuathiri haki na maslahi ya wananchi.

“Soko la kaboni linapaswa kuwa fursa ya kulinda mazingira, kuvutia uwekezaji wa kijani na kuboresha maisha ya wananchi. Ni muhimu kuhakikisha kuwa kila mradi unazingatia sheria, unalinda mifumo ikolojia na kuleta manufaa yanayopimika kwa jamii.”

Kupitia usimamizi madhubuti wa mazingira, NEMC itaendelea kutekeleza wajibu wake katika kujenga mazingira wezeshi kwa uwekezaji endelevu na kuchangia maendeleo ya kijani nchini Tanzania.

14/10/2026
Je wajua?
13/10/2026

Je wajua?

Address

Regent Street
Dar Es Salaam
00000

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 09:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NemcTanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share