NemcTanzania

NemcTanzania

Share

Karibu katika ukurasa rasmi wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC). Pamoja tulinde na kutunza mazingira kwa maendeleo endelevu.

Photos from NemcTanzania's post 05/05/2026

NEMC KANDA YA MOROGORO-RUFIJI NA MABALOZI WA MAZINGIRA WAFANYA ZIARA SHULE YA SEKONDARI MWEMBESONGO

๐Ÿ“ŒWatoa Elimu ya Mazingira ya Mazingira

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa Kushirikiana na Mabalozi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Grit Godfrey Mwimanzi na Chage Alex Chage wamefanya ziara katika Shule ya Sekondari ya Mwembesongo na kutoa elimu ya Mazingira katika Shule hiyo hususan kuhusu fursa zilizopo kwenye taka, Utunzaji wa Mazingira pamoja na kupanda miti.

Tukio hilo liliongozwa na mwenyeji ambaye ni Meneja wa NEMC Kanda ya Morogoro - Rufiji
Ndugu Arnold Mapinduzi akiambatana na Maafisa wa Kanda hiyo.

Aidha tukio hilo lilihusisha Afisa Mazingira wa Manispaa ya Morogoro na wadau wengine wakiwemo Masai wa Maji (Tone la Maji lihifadhiwe) Kipaji changu Foundation na Wananchi kwa ujumla.

Aidhaa Maafisa wa NEMC pamoja na mabalozi wa Mazingira walisisitiza juu ya namna ambavyo taka si uchafu tena bali zinaweza kubadilika Kuwa Fursa.

Aidha, Mabalozi wa Mazingira Waliahidi kupeleka Dustbins kwenye Shule Hiyo Walau watoto waanze kwa vitendo swala la utenganishaji Wa Taka kwenye Shule Hiyo lakini pia na kuwatafutia Mdau kwa ajili ya kupata kizimba Cha utenganishaji Wa Taka.

Pia Pongezi Kubwa zilitolewa Kwa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi sambamba na timu nzima ya NEMC Nchini kwa muendelezo wa kampeni ya Taka ni Fursa kwa nchi nzima, kwa mlengo wa kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa Safi lakini pia Kuhakikisha Madampo sasa hayatafurika uchafu badala yake Taka Nyingi zitatumika k**a ni Fursa Kwa kuzirejeleza au kwa Matumizi Mengine

04/05/2026
04/05/2026

MIAKA 40 YA UHIFADHI WA MAZINGIRA๐Ÿ’ช๐Ÿฝ

#๐‘ด๐’‚๐’›๐’Š๐’๐’ˆ๐’Š๐’“๐’‚๐’€๐’†๐’•๐’–๐‘ผ๐’‰๐’‚๐’Š๐‘พ๐’†๐’•๐’–

04/05/2026

#๐‘ด๐’‚๐’›๐’Š๐’๐’ˆ๐’Š๐’“๐’‚๐’€๐’†๐’•๐’–๐‘ผ๐’‰๐’‚๐’Š๐‘พ๐’†๐’•๐’–

03/05/2026

#๐‘ด๐’‚๐’›๐’Š๐’๐’ˆ๐’Š๐’“๐’‚๐’€๐’†๐’•๐’–๐‘ผ๐’‰๐’‚๐’Š๐‘พ๐’†๐’•๐’–

Photos from NemcTanzania's post 03/05/2026

๐—ก๐—˜๐— ๐—– ๐—ฌ๐—”๐—ฆ๐—›๐—œ๐—ฅ๐—œ๐—ž๐—œ ๐— ๐—”๐—™๐—จ๐—ก๐—ญ๐—ข ๐—ฌ๐—” ๐—˜-๐— ๐—ฅ๐—˜๐—๐—˜๐—ฆ๐—›๐—ข ๐——๐—ข๐——๐—ข๐— ๐—”

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki mafunzo ya mfumo jumuishi wa e-mrejesho (shared system) yaliyotolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yaliyofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dodoma

Mafunzo hayo yalilenga kuwanoa watumishi namna Mfumo huo unavyotumika kutuma, kufuatilia, na kupokea majibu ya malalamiko, mapendekezo, maoni, pongezi na maulizo kwa taasisi za umma nchini.

Mafunzo hayo pia yalifanyika kwa vitendo ambapo kila mtumishi aliyehudhuria mafunzo hayo alipaswa kuwasilisha mada namna alivyojifunza na kuelewa ili kupima uelewa na kuhakikisha watumishi hao wanauelewa vyema mfumo huo

Hatua hiyo ni juhudi za Serikali katika kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuendana na mabadiliko chanya ya teknolojia ambao utamwezesha mwananchi kutuma, kufuatilia na kupokea mrejesho wa malalamiko, mapendekezo, maulizo au pongezi

Photos from NemcTanzania's post 02/05/2026

Timu ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wanaofanya ukaguzi wa mazingira katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria, wakiongozwa na Meneja wa Utekelezaji wa Sheria, Mha. Luhuvilo B. Mwamila, waliadhimisha Sikukuu ya Wafanyakazi- Meimosi 2026 kwa kupanda miti katika Makumbusho ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Butiama.

Hatua hiyo ni ishara ya kuenzi dira ya Baba wa Taifa katika kuhifadhi mazingira na kusimamia utekelezaji wa sheria za utunzaji wa rasilimali za Taifa.

02/05/2026

#๐‘ด๐’‚๐’›๐’Š๐’๐’ˆ๐’Š๐’“๐’‚๐’€๐’†๐’•๐’–๐‘ผ๐’‰๐’‚๐’Š๐‘พ๐’†๐’•๐’–

02/05/2026

#๐‘ด๐’‚๐’›๐’Š๐’๐’ˆ๐’Š๐’“๐’‚๐’€๐’†๐’•๐’–๐‘ผ๐’‰๐’‚๐’Š๐‘พ๐’†๐’•๐’–

Photos from NemcTanzania's post 01/05/2026

NEMC YAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KUSHEREHEKEA MEI MOSI

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeungana na Watanzania wote kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ngazi ya Mkoa yaliyofanyika Mei 1, 2026 katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ambapo Kitaifa yamefanyikia Mkoani Njombe

Akizungumza katika maadhimisho hayo yenye kaulimbiu "๐™ ๐™–๐™ฏ๐™ž ๐™ฏ๐™š๐™ฃ๐™ฎ๐™š ๐™จ๐™ฉ๐™–๐™๐™– ๐™ฃ๐™ž ๐™ฃ๐™œ๐™ช๐™ฏ๐™ค ๐™ž๐™ข๐™–๐™ง๐™– ๐™ ๐™ฌ๐™– ๐™ข๐™–๐™š๐™ฃ๐™™๐™š๐™ก๐™š๐™ค ๐™š๐™ฃ๐™™๐™š๐™ก๐™š๐™ซ๐™ช ๐™ ๐™–๐™ฉ๐™ž๐™ ๐™– ๐™ช๐™ฉ๐™š๐™ ๐™š๐™ก๐™š๐™ฏ๐™–๐™Ÿ๐™ž ๐™ฌ๐™– ๐˜ฟ๐™ž๐™ง๐™– ๐™ฎ๐™– 2050" Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila alisisitiza umuhimu wa uwajibikaji, nidhamu kazini na uzalendo miongoni mwa wafanyakazi, akieleza kuwa mafanikio ya maendeleo ya mkoa na Taifa kwa ujumla yanategemea juhudi za kila mfanyakazi.

Aidha, alihimiza waajiri kuhakikisha wanaboresha mazingira ya kazi na kuwapatia wafanyakazi nyenzo stahiki ili kuongeza ufanisi na tija.

Kupitia risala ya vyama vya wafanyakazi, ilielezwa kuwa kuna umuhimu wa kuendelea kupigania ajira zenye staha kwa wote ili kuwawezesha wananchi kuishi maisha bora ikiwemo kulindwa kwa haki za wafanyakazi, kuboreshwa kwa maslahi yao pamoja na kuhakikisha mazingira salama ya kazi yanazingatiwa wakati wote.

Maadhimisho hayo yamekuwa fursa muhimu kwa wafanyakazi na waajiri kutafakari mchango wao katika maendeleo ya taasisi na Taifa, huku kaulimbiu ya mwaka huu ikisisitiza umuhimu wa kazi zenye staha, ulinzi wa haki za wafanyakazi na utekelezaji wa sheria za kazi k**a msingi wa maendeleo endelevu.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Regent Street
Dar Es Salaam
00000

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 09:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00