17/05/2024
TLSB kupitia Maktaba ya Mkoa wa Dodoma imefanya ziara katika shule mbili ambazo ni; Shule ya Msingi Nzuguni na Shule ya Sekondari Viwandani kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi matumizi bora ya Maktaba na umuhimu wa kujisomea vitabu, tarehe 9 Mei, 2024.
17/05/2024
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Buronge Mkoani Kigoma wametembelea Maktaba ya Mkoa wa Kigoma kujifunza matumizi ya Maktaba na kusoma vitabu tarehe 13 Mei, 2024.
17/05/2024
TLSB kupitia Maktaba ya Mkoa wa Dodoma imetembelea shule ya Msingi Chidachi ya jijini humo kuhamasisha wanafunzi matumizi bora ya Maktaba na umuhimu wa kujisomea vitabu, tarehe 14 Mei, 2024.
17/05/2024
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Utengule wametembelea Maktaba ya Mkoa wa Rukwa ili kujifunza matumizi sahihi ya Maktaba na kujisomea vitabu tarehe 11 Mei, 2024.
17/05/2024
Pichani: Matukio mbalimbali katika ziara ya Wanafunzi na Walimu wao kutoka shule saba za jijini Dar es Salaam, tarehe 15 Mei, 2024.
17/05/2024
WANAFUNZI 70 NA WALIMU 14 WA SHULE SABA (7) ZA SEKONDARI DAR ES SALAAM WATEMBELEA BODI YA HUDUMA ZA MAKTABA TANZANIA, MAKAO MAKUU – DAR ES SALAAM
Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) Makao Makuu Dar es Salaam, imepokea ugeni wa Wanafunzi 70 na Walimu 14 kutoka shule saba (7) za Sekondari za jijini Dar es Salaam tarehe 15 Mei 2024.
Wanafunzi na Walimu hao wametembelea TLSB kwa uratibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Realizing Education for Development (READ Tanzania) ili kujionea shughuli na huduma zinazotelewa na Bodi, vilevile kujifunza matumizi sahihi ya Maktaba.
Akizungumza katika mapokezi hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Uendeshaji Huduma za Maktaba TLSB Dkt. Rehema Ndumbaro, ametoa rai kwa wanafunzi hao kujisajili katika maktaba ili wapate huduma za kujisomea vitabu vya kiada na ziada na kujiongezea maarifa, vilevile, kunufaika na huduma za kuazima vitabu mbalimbali.
Aidha, Dkt. Ndumbaro amewasisitiza wanafunzi hao kutumia Maktaba wakati wa likizo kujisomea na kuazima vitabu kwani ndio wakati sahihi wa kujikumbusha yote waliyosoma shuleni.
Kwa upande wake Mratibu na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya READ Tanzania Bi. Naemy Sillayo, ameushukuru Uongozi wa TLSB kwa mapokezi mazuri na kusema moja ya majukumu ya taasisi yao ni kuhamasisha wanafunzi kupenda kujisomea vitabu kupitia Maktaba zilizopo katika shule wanazosoma na kwenda katika maktaba mbalimbali ikiwemo Maktaba zilizopo chini ya TLSB kwa ajili ya kujifunza.
Kwa upande mwingine, Wanafunzi na Walimu wao pia wameshukuru mapokezi na taarifa mbalimbali walizozipata kuhusu Maktaba na baadaye kuzunguka katika Vitengo mbalimbali vilivyomo ndani ya Maktaba Kuu ya Taifa vikiwepo; Kitengo cha Watoto na Shule (CSSD), Kitengo cha Bibliografia ya Taifa (NBA), Kitengo cha Ufundi (TSD) na Kitengo cha usomaji cha Watu wazima (RSD) na kujionea shughuli na huduma mbalimbali zinazotolewa na vitengo hivyo.
Wanafunzi na Walimu hao wakiongozwa na taasisi ya READ Tanzania wametoka shule za Sekondari Goba, Fahari, Twiga, Makumbusho, Mugabe, Maramba na Kiluvya zote za jijini Dar es salaam.
Pichani: K/Mkurugenzi Mkuu Dkt. Rehema Ndumbaro (wa pili kushoto) akimkabidhi mwanafunzi Kitabu.
02/05/2024
Pichani: Watumishi wa TLSB kutoka Maktaba za Mikoa ya Arusha, Iringa, Mwanza na Dodoma wakisherehekea Sikukuu ya Mei Mosi tarehe 1 Mei, 2024.
01/05/2024
TLSB inawatakia Watanzania wote kheri ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) 2024.
26/04/2024
TLSB inawatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya sikukuu ya Muungano wa Tanzania.
15/04/2024
Pichani: Mwendelezo wa matukio mbalimbali katika kikao cha 64 cha Baraza la Chuo SLADS.
15/04/2024
Pichani: Matukio mbalimbali katika Kikao cha 64 cha Baraza la Chuo SLADS kilichofanyika tarehe 04 April, 2024.