Siri Za Biblia

Siri Za Biblia

Share

Mafundisho ya neno la Mungu na Maombi�

14/11/2023

JINSI YA KUJENGA NDOA NA MAHUSIANO BORA💥

Nyumba hujengwa na vitu vingi ikiwemo msamaha na matumizi ya kinywa. Mama anapojua kutumia vizuri kinywa chake anayo nafasi kubwa sana kuiponya na kujenga hata kuimarisha ndoa yake.
MITHALI 9: 13💥 MITHALI 14: 1 - 5💥

Hili hutokana na majibu yake pale anapoongea na mume wake kwa kauli nzuri njema zenye kuvutia na kubembeleza; hulka ya mwanamke ni upole na kauli zake ni za kipole maneno matamu yenye kuvutia na kubembeleza hata k**a mtu kapandisha hasira kwa jibu na kauli yako ya upole

Unamshusha sawa na Neno la Mungu lisemavyo katika MITHALI 15: 1 💥ya kwamba "Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu."

Sio kila jambo unatakiwa kulitolea ufafanuzi ama kuongea, wakati mwingine jishushe tu omba msamaha hata uonapo umekosewa na kuonewa kisha nyamaza kimya maana kazi ya utetezi si yako bali ya Mungu wako yeye atasimama kukutetea kwa njia yake mwenyewe.

Kunyamaza ni hekima, maana maandiko yanasema kwamba "Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na mwenye roho ya utulivu ana busara. Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu." (MITHALI 17:27-28) na AYUBU 13:5 💥inasema kwamba "Laiti mngenyamaza kabisa! Hilo lingekuwa hekima kwenu."

kumbe basi kuna muda inakupasa kunyamaza kimya tu si kwa kiburi au dharau ila kuipisha ghadhabu tu.

Sote twafahamu ya kwamba ulimi ni kiungo kidogo lakini kina madhara makubwa sana kulingana na Neno la Mungu kutoka YAKOBO 3:5-6; 💥hivyo basi k**a mke chunga ulimi wako
▪Jishushe
▪Omba tu msamaha ubebe ubaya
▪Nyenyekea na kujishusha
▪Nyamaza kimya usifumbue mdomo wako kuongea ukiwa na hasira maana hasira haifanyi kazi na hekima hata siku moja.
▪Usiwe mwanamke wa kupiga piga kelele tu na kuongea sana

MITHALI 10:19 💥inasema kwamba "Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili." angalia katika kuongea kwako sana unakwaza na kukosea na WAEFESO 4:31💥 inatuonya ya kwamba "Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya"

Wewe ni mke jenga ndoa yako kwa kutumia kinywa chako na msamaha mwombe Roho wa Mungu akusaidie kujishusha, kuachilia, kusamehe, akupe hekima ya kiMungu ambayo ni safi, yenye amani, upole,iliyo tayari kusikiliza, imejaa rehema (msamaha), yenye kutenda mema isiyo na unafiki wala fitina (YAKOBO 3:17-18💥)

✍🏼 Mtumishi Fahim 0716 822126 Whatsapp 💥

Maombi na ushauri Whatsapp 0716 822126 🙏

26/05/2023

YAFAHAM MAISHA YA MAHUSIANO💓 NA NDOA❣

Maisha ya ndoa ni safari na ninayafananisha na mtu/watu wanapoanza safari kwa gari/ndege /meli nk.

Kwenye safari yoyote kuna mambo mengi hata k**a aina ya usafiri ulioutumia ni bora namna gani hutakosa changamoto mbali mbali kwenye safari yako mpaka ufike.

Unapoanza safari yoyote ile ndio maana tunashauri usianze safari pasipo maombi,maombi sio kwamba yatazuia changamoto za safari bali maombi yatakushindia dhidi ya changamoto za Safari.

Kwenye safari kuna changamoto za matuta wakati mwingine yumkini hukuona kuwa mbele kuna tuta mara unashangaa umelivamia.
Kwenye ndoa yaweza kuwa tuta ni changamoto ya Uchumi au kuchelewa kupata mtoto/watoto.
Ni jambo ambalo wengi tunapoingia kwenye ndoa hatujui k**a Uchumi wetu utakuwaje , hatujui muda gani tutapata watoto,hili linaweza kuwa Tuta, lakini tuta haliwezi kukuzuia kuendelea na safari yako.

Kwenye safari waweza kukutana na Traffic akakwambia usimame labda umeovertake ,labda gari inadaiwa,labda gari limejaza watu wengi nk.
Na kwenye ndoa kuna vitu tutakutana navyo vinaweza kutusimamisha na kuchelewesha ndoto zetu za ndoa, inaweza kuwa Madeni, yaweza kuwa kukosa kazi lakini hakuna aliyeahirisha safari kwasababu amek**atwa na Traffic,lazima ufanye ufanyavyo ili safari yako iendelee

Mambo k**a magonjwa,mambo k**a madeni,mambo k**a kukosa kazi ni Traffic kwenye ndoa lakini chonde chonde usiruhusu ndoa yako iishie hapo kwasababu ya Ugonjwa, kwasababu ya madeni, kwasababu ya kukosa kazi.Safari lazima iendelee

Kwenye safari kuna vitu k**a barabara mbaya,vumbi,mashimo nk haya nayo yanaleta karaha, lakini hakuna aliyeamua kusitisha safari kwasababu ya vumbi , mashimo na tope vilivyowahi kuzuia watu wasifike.Vumbi likizidi watu wanafunga madirisha, mashimo yakizidi watu wanafunga mikanda,tope likizidi watu wanaweka S,au gari likikwama wanatafuta majembe,kulitoa gari lakini hakuna aliyewahi kuliacha gari lake kwenye tope.

Kwenye ndoa Kuna wakati mtaingia kwenye tope, kuna wakati ndoa itapata upepo na vumbi la kutosha yaweza kuwa maneno ya watu,ndugu kutaka kuwagombanisha tafadhali vaeni mikanda,uwezo wa kuinusuru ndoa yenu uko mikononi mwenu.

SIKIA
Ndoa yako imedumbukia kwenye tope,imeingiliwa na kahaba,katafute nyenzo itoe ndoa yako usikubali kuitupa kwenye tope na kuiacha.

Safari ya ndoa ni ndefu sana lakini ukijua kuwa ndoa ni safari na kwenye kila safari kuna changamoto mbali mbali lakini changamoto hazituzuii kufika salama, jitahidi sana usishuke kwenye gari kabla ya mwisho wa safari yako

Nakuombea safari yako iwe njema hata k**a utakutana na magumu kwenye hiyo safari usiache kuvaa mkanda,boots, kufunga vioo ili Mradi ufike salama

Je ni changamoto gani unapitia kwenye ndoa yako? nakuombea usikubali kuacha ndoa yako kwasababu ya huo upepo wa muda, kwasababu ya hilo tope, kwasababu ya hilo vumbi,nk.
Neema ya Mungu ikubebe nakuona ukifika Mwisho salama Tena kwa ushindi.

Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. (Mithali
24:3-4)💥

K**A UNAPITIA CHANGAMOTO YOYOTE KWENYE MAHUSIANO NA NDOA YAKO😭 NJOO NIOMBE NA WEWE NA MUNGU ATAKUTOA KWENYE HAYO MATESO NAKUKUPA FURAHA KWA JINA LA YESU 🙌

Maombi na ushauri 💚Whatsapp 0716822126

By Mtumishi Fahim 💥 Whatsapp 0716822126 🙏

24/05/2023

USIKUBALI KUUA NDOTO ZAKO KWA SABABU YA KUKOSEA AU KUKWAMISHWA😓

📌 K**a bado upo hai, unaweza kuwa chochote wakati wowote.

✅ INUKA TENA, JARIBU TENA, SUKUMA TENA, OMBA TENA, JIELEZE TENA, ANZA TENA.

Kuanguka siyo mwisho wa safari inuka uendee ushindi wako,

Hata Yesu alianguka na msalaba lakini akainuka tena mpaka akashinda 💪

Maneno husemwa ili kukupunguzia mwendo, wanao kulaan kunasiku watakubariki

Shetani hukuonyesha makosa ili ukate tamaa ushindwe kusonga mbele maana anajua mbele yako kuna ushindi.

Kukosea hakumanishi wewe hufai laa! Inuka mtazame Mungu mwisho utashinda.

📌 Mungu akiweka shauku fulani ndani yako, hakuna kitu chochote nje yako kinachoweza kuua hiyo shauku isipokuwa WEWE mwenyewe ukubali shauku ife. Kwa kukata tamaa

Kumbuka: “Yote Yanawezekana Kwake Aaminie” (Marko 9:23).

K**a unapitia changamoto ya kushindwa jambo fulani kila wakati njoo niombe na wewe ufunguliwe kwa jina la Yesu 🙌

Maombi na ushauri Whatsapp 0716822126🙏

📌By Mtumishi Fahim +255716822126 Whatsapp

11/03/2023

SIRI YA KUPENDWA💓 NA UNAEMPENDA💞 NI HII
✍by Mtumishi Fahim💥

Ndoa nyingi na mahusiano mengi yanavunjika siyo kwa sababu watu hawa jui kupenda laa! Wengi wanupendo wa kweli kwa wale wanao wapenda lakini wao hapendwi k**a wanavyo penda❣😪

Maana kupendwa ni kibali maalum mtu hupewa na Mungu, kinaenda kukaa kwenye moyo wako kinakuwa na nguvu kubwa ya ushawishi ukimpenda mtu kile kibali kinaena na upendo wako ndani ya moyo wa huyo mtu kinamtafasiria upendo wako kwake, hivo anashawishika kukupenda zaidi na kukuamini na kuridhika na wewe asione mwingine zaidi yako hapo ndipo utaona raha ya kupenda.🤝

UPENDO NI NINI ❣

Upendo wa mahusiano ya kimapenzi au uchumba ni k**a nguvu ya mwanga wa tochi 💥 unapo mulika unatakiwa ugonge sehem kisha ukurudie, lakini unapo mulika mwanga ukaenda tu ndiyo unakuta hupati maana ya kuwasha tochi

Moyo ni k**a tochi na upendo ndiyo mwanga💥 wake, unapo penda, moyo unatamani upendo ugonge kwenye moyo mwingine ili urudishe upendo, upendo unapo kurudia ndiyo unaona thamani ya ndoa au mahusiano.

Lakini ukipenda na usipendwe unakuwa k**a mtu alie mulika mwanga angani, maana mwanga haumrudii hivo unakuwa hauna maana kwake. Hivyo hata moyo ukikosa upendo kwa unae mpenda una umia na kupoteza ujasiri wakupenda na unakata tamaa.

KWANINI IMEKUWA NGUMU KUPENDWA❤️ NA UNAE MPENDA💓?

Jibu ni kwamba watu wengi wamepoteza kibali au mvuto wa kupendwa na wanao wapenda kwasababu shetani au wachawi wamewaibia nyota au kibali katika ulimwengu wa roho ili kuharibu hatima za watu katika mahusiano na ndoa💘 ili ukipenda usipendwe ili umizwe moyo uchukie kupenda😭.

Niki biblia kabisa wewe kupendwa na unae mpenda 📕YOHANA 13: 34💥 ukisoma hapo utaona Biblia inasema amri mpya nawapeni pendaneni kwahiyo wewe kupendwa na unae mpenda ni haki yako na Mungu asingesema hivo k**a alijua hilo jambo haliwezekani alisema hivo kwakuwa alijua inawezekana, na kunakitu amekiumba ndani ya moyo wa mtu kinacho sababisha apendwe na anae mpenda💯

Wetu wengi wanalia kwenye mahusiano na ndoa kwa sababu hawapati upendo kamili kutoka kwa wale wanao wapenda🤦‍♀️, unaona k**a kuna nguvu iko moyoni mwako unajaribu kuionyesha kwa hisia na matendo lakini unaona k**a yule unaempenda haelewi ile nguvu ya upendo ulio nao kwake💓

Nikwasababu huna nguvu au kibali moyoni mwako kinachoenda na upendo wako moyoni mwa yule unaempenda kikamtafasiria upendo wako kwake, kisha kikazalisha upendo ndani ya moyo wake na yeye akakulipa upendo 💞 matokeo yake unalipwa maumivu na kusaritiwa😭 na kuchukiwa na yule unae mpenda💘 wakati mwingine ana kuona k**a huna thamani wala maana yoyote kwake.
Mpendwa hakuna mtu ambae hana thamani wala maana yoyote maadam yuko hai

Mungu hawezi kukupa uhai k**a maana yako na thamani yako imeisha hapa duniani, bali umepoteza kibali au nyota ya kupendwa😢 ndiyo maana unateseka Kwenye ndoa na mahusiano, ukipoteza hicho kibali cha kupendwa unaweza kushanga hata vitu vya kawaida k**a biashara pesa mafanikio kazi huvipati, vinakukataa kwakuwa unavipenda lakini vyenyewe havi kupendi. Unatakiwa maombi ya kurejesha kibali chako au nyota yakupendwa💓

Moyo ni k**a sumaku na upendo ni nguvu yake, yule unaempenda anatakiwa awe k**a chuma ukitupa upendo kwake yeye anatupa upendo wa nguvu k**a ya chuma ana tafasiri ile nguvu ya upendo wako kwake hivo moyo unanasa kwa nguvu ya upendo

Yeyote unae mpenda anaweza kukupenda lakini unahitaji nguvu ya Mungu iumbe nguvu ya ushawishi ndani yako ili unapo mpenda mtu, ile nguvu iingee ndani ya moyo wa yule unae mpenda na imshawishi kukupenda zadi k**a unavyo mpenda, yani upendo wako uwe k**a mbegu unapo mpenda mtu uingie kwenye moyo wa huyo mtu unae mpenda na kuzalisha upendo zaidi na ajikute amekupenda wewe k**a unavyo mpenda au zaidi.

K**A UMEPOTEZA KIBALI AU NYOTA YA KUPENDWA, UNAPENDA WEWE HUPENDWI NJOO NIKUOMBEE MUNGU AKUPE AU AKUREJESHEE KIBALI NYOTA💥 YA KUPENDWA NA KILA UNACHO KIPENDA❣
Maombezi Whatsapp📲 0716822126🙏

✍️ by Mtumishi Fahim💥
Whatsapp 0716822126

Mungu akubariki sana

21/02/2023

KILA MKONO MBAYA
Ulionyooshwa juu yako kukudhuru
Kukuletea magonjwa
Kukuletea mafarakano, kwenye ndoa yako, mahusiano yako,
Kila mkono wa chuma ulete kwenye kazi yako, kwenye mifuko yako
KWA JINA LA YESU TUNAUKATA,
HAUTAFANIKISHA MAKUSUDI YAKE JUU YAKO,
k**a unaaamini pokea kwa jina la Yesu 🙏

Maombezi Whatsapp 📲+2550716822126

21/02/2023

Mungu akubariki mno mtumishi wa Mungu pastor Lilian Kadodo 🙏

02/12/2022

Ni seme nini siwezi kueleza baba nina kushukuru_by Dr. Ipyana

02/12/2022

WEWE AMBAYE BADO HUJAINGIA KWENYE NDOA💞
USIKATE TAMAA😢
👉Usikate tamaa kisa bado hujapata mtu wa kuingia 💥naye kwenye ndoa

👉Usikate tamaa kisa wote uliokutana nao walikuacha 💥kwa maumivu makali

👉Usiwe na maneno ya kukata tamaa eti wanaume au 💥wanawake wote ni wabaya

👉Nikuambie tu sio watu wote ni wabaya ,Watu wazuri 💥wapo wengi ni bado wewe hujakutana nao

👉Lakini namna nzuri zaidi ya kumpata mtu mzuri
💥unayemtaka wewe ni kwanjia ya maombi 🙏

👉Unataka mwanamke mwenye sifa njema mwombe 💥Mungu mshilikishe Mungu maana Mungu anamtu 💥sahihi kwa ajili yako,, kwa macho tu huwezi
💥kumtambua alie sahihi kwako

📕Mithali 5:18
👉Ni maombi yangu siku ya leo Mungu akukutanishe 💥na mtu ambaye utamfurahia katika ujana wako na 💥mpaka katika uzee wako 🙏🙏🙏🙏

✍️By Pastor Lilian Kadodo 💥

Tuandikie inbox 📥 majina yako mahali unapoishi namba yako ya cm na mahitaji yako tukuombee 👏

01/12/2022

JIFUNZE MBINU🤔 ZA MAISHA NA UFANIKIWE KWA KILA JAMBO LAKO💥💥
Ufanikiwe kazini👉ufanikiwe kwenye ndoa👉ufanikiwe kwenye mahusiano👉ufanikiwe kwenye maisha ya kiroho👉ufanikiwe kwenye elimu yako🙏

Tuandikie inbox 📥 majina yako mahali unapoishi namba yako ya cm na mahitaji yako tukuombee 👏

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Dar Es Salaam