NSSF Tanzania

NSSF Tanzania

Share

The National Social Security Fund is a fully funded scheme running under defined benefit principles.

02/06/2026

SERA YA UBORA

02/06/2026

QUALITY POLICY STATEMENT

01/06/2026

Okoa Muda tumia Lango la Huduma la NSSF

31/05/2026

Uliye jiajiri umejiunga na kujisajiri na Hifadhi Scheme? Fahamu namna ya kujiunga na kuchangia

Namna ya kujiunga kupitia mitandao ya simu;

1.⁠ ⁠Piga *152*00 #

2.⁠ ⁠Bonyeza 9 Ajira na Utambuzi

3.⁠ ⁠Bonyeza 6 NSSF

4.⁠ ⁠Bonyeza 1 Jisajili kisha fuata maelekezo

Namna ya kuchangia kupitia mitandao ya simu;

1.⁠ ⁠Piga *152*00 #

2.⁠ ⁠Bonyeza 9 Ajira na Utambuzi

3.⁠ ⁠Bonyeza 6 NSSF

4.⁠ ⁠Bonyeza 2 malipo

5.⁠ ⁠Bonyeza 2 mwanachama kisha fuata maelekezo


.evalinemunisi

28/05/2026

Mwananchi yeyote aliye jiajiri anaweza kujiunga na NSSF kupitia Hifadhi Scheme kwa ajili ya kujichangia kidogo kidogo kuanzia Tsh 30,000 na kuendelea ili baadaye naye NSSF ije kuwa Staa wa mchezo wake kwa kuwa na uzee uliobora kwa kupata Mafao, Mwanachama akichangia miezi 3 anaanza kupata fao la matibabu bure, lakini anatakiwa awe anachangia kila mwezi TZS 30,000 kwa mtu mmoja au 52200 kwa Mke/Mume na watoto wanne walio chini ya umri wa miaka 18 au 21 k**a wanasoma.

Namna ya kujiunga kupitia mitandao ya simu;

1.⁠ ⁠Piga *152*00 #
2.⁠ ⁠Bonyeza 9 Ajira na Utambuzi
3.⁠ ⁠Bonyeza 6 NSSF
4.⁠ ⁠Bonyeza 1 Jisajili kisha fuata maelekezo

Namna ya kuchangia kupitia mitandao ya simu;

1.⁠ ⁠Piga *152*00 #
2.⁠ ⁠Bonyeza 9 Ajira na Utambuzi
3.⁠ ⁠Bonyeza 6 NSSF
4.⁠ ⁠Bonyeza 2 malipo
5.⁠ ⁠Bonyeza 2 mwanachama kisha fuata maelekezo

FAIDA YA MWANACHAMA ANAYEJICHANGIA BINAFSI

Kuna faida nyingi za Mwanachama binafsi kujiunga na Mfuko huu,

1. kujiwekea akiba kwa ajili ya kesho yako iliyo njema yaani kuja kuishi kifahari kwa kupata Pensheni ya Uzeeni
2. Mwanachama akichangia miezi 3 anaanza kupata fao la matibabu bure, lakini anatakiwa awe anachangia kila mwezi TZS 30,000 kwa mtu mmoja au 52200 kwa Mke/Mume vise versa na watoto wanne walio chini ya umri wa miaka 18 au 21 k**a wanasoma.
3. Mafao ya urithi
4. Mafao ya ulemavu
5. Msaada wa Mazishi
6. Mafao ya kujitoa ( Kuchukua sehemu ya Michango au kuchukua michango yote)
7. Mafao ya uzazi

Photos from NSSF Tanzania's post 27/05/2026

Uwekezaji wa NSSF Mkulazi Wachochea Ajira, Wapunguza Nakisi ya Sukari

Na Mwandishi Wetu,
Morogoro.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amesema mradi wa kiwanda cha sukari Mkulazi ni mradi wa kimkakati unaotekeleza kwa vitendo maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga uchumi imara, shindani na shirikishi, sambamba na kufikia Dira ya Taifa ya 2050 na kuongeza fursa za ajira.

Akizungumza Mei 23, 2026, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ilipotembelea mradi huo mkoani Morogoro, Mhe. Sangu aliipongeza k**ati hiyo kwa ufuatiliaji wake, akibainisha kuwa maelekezo 11 yaliyotolewa awali tayari yameingizwa katika utekelezaji, hatua inayoimarisha uwajibikaji na ushirikiano kati ya Bunge na Serikali.

Aidha, alisema mradi huo umeanza kurekodi mafanikio kwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 2,176 katika msimu huu, huku ukitarajiwa kufikia ajira 2,315 za moja kwa moja na 9,000 zisizo za moja kwa moja kadri uzalishaji unavyopanuka. Uzalishaji wa tani 50,000 za sukari unatarajiwa kupunguza nakisi ya bidhaa hiyo nchini kwa takribani asilimia 20.

Katika kuongeza tija, Serikali imepanga kupanua mashamba ya miwa kutoka hekta 4,156 hadi 6,000, hatua itakayoongeza uwezo wa uzalishaji hadi tani 75,000. Alisisitiza kuwa uwekezaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii, ikiwemo NSSF, unaelekezwa kwenye miradi yenye manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi na uchumi wa taifa.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hawa Mchafu Chakoma, alipongeza kazi kubwa inayofanywa na Serikali kupitia NSSF kwa kushirikiana na SHIMA katika mradi huo, akieleza kuwa umeendelea kuleta tija kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake, akizungumza kwa niaba ya k**ati, Mhe. Kafiti Kafiti alisema mradi huo ni ushahidi wa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, akibainisha kuwa viwanda vina mchango mkubwa katika ajira, kipato na ukuaji wa uchumi. Aliongeza kuwa zaidi ya wakulima 3,500 wanaonufaika na mradi huo wanachochea maendeleo ya kiuchumi katika maeneo ya vijijini.

Mhe. Kafiti alibainisha kuwa matarajio ni kiwanda kuanza kupata faida katika mwaka wa fedha ujao, jambo litakaloongeza mapato ya Serikali na kulinda uwekezaji wa fedha za wanachama wa NSSF, huku k**ati ikiendelea kusimamia mradi huo ili kuhakikisha unafikia malengo yaliyokusudiwa.

Akihitimisha kikao hicho, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Dkt. Aveline Munisi alihakikishia k**ati hiyo kuwa ushauri na mapendekezo yao yataendelea kufanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya mradi huo.

Wajumbe wa k**ati walimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, kwa uongozi wake thabiti, wakieleza kuwa amefanikisha kufufua na kusukuma mbele miradi iliyokuwa imesimama, huku mafanikio ya Mkulazi yakidhihirisha maono yake ya kuongeza uzalishaji, kuvutia uwekezaji na kupanua fursa za ajira.

Walisisitiza umuhimu wa kuendeleza nidhamu, uwazi na uaminifu ili miradi hiyo iendelee kuleta manufaa mapana kwa wananchi na uchumi wa taifa.

26/05/2026

Eid al Adha Mubarak

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


P. O. Box 1322, Azikiwe Street
Dar Es Salaam
0255