Mwl Japhet Power of God

Mwl Japhet Power of God

Share

Healing and Deliverlence......

10/03/2025

*TAFAKARI YA MWANZO WA WIKI:*

Nimesikia kukuombea siku ya leo, sijui unapitia nini kwenye maisha yako, sijui hilo pito unalopitia limedumu kwa miaka mingapi

Ninakuombea Mungu akakuonekanie na kukuvusha kwenye hilo pito kwa jina la Yesu. Na wakati ninaomba niliona mtu ambae moyo wake umechoka sana kutoka na mlima uliosimama mbele yake

Niliona mtu ambae anapovuka hili linaibuka lingine, niliona mtu ambae mateso yale yale kwenye familia yaliyo kwamisha wengine kwenye familia yameinuka na kwake pia

Mwanzoni alifikili yeye hawezi kuwa k**a wao,lakini ghafla na yeye amejikuta k**a wao kwenye eneo la kichumi, eneo la kimahusiano, kwenye Eneo la Afya.

Wakati naomba Mungu alinipa huu mstari wa

*Nahumu 1:9*
Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.

Ndipo akaniambia

Mwambie ninaenda kuyakomesha kabisa hayo mateso yaliyomtesa kwa miaka mingi hayatainuka tena mala ya pili kwa jina la Yesu.

Mtoto wa Mungu huu ujumbe hauusomi kwa bahati mbaya unausoma kwa makusudi kabisa ikiwa utaamini wakati unaendelea kusoma kuna kitu Mungu anafanya kwenye maisha yako

Amini tu huo msiba, hilo jambo lilikotesa kwa muda mrefu, amini tu hicho kinachokunyima usingizi kwa muda mrefu,hicho kinachokukosesha amani na furaha.

Hicho kinachokufanya uwe mtu wa kulia kila wakati, Ninakuombea Bwana akakikomeshe kwa jina la Yesu na kwa jina la Bwana wa Majeshi nakutamkia hakitainuka mara ya pili tena.

Amini tu utavuka wala hutaaibika nimekuombea katika jina la Yesu.

Unahitaji kuamini tu na kujisemea moyoni mwako kwamba haya mateso hayatainuka mara ya pili. BARIKIWA

Mtumishi Japhet
0625467840
KGR

05/03/2025

Joint Mass Kusanyiko kubwaaa....

01/03/2025

MWANZO WA MWEZI WA TATU

Hongera sana kwa neema uliyopata ya kuingia mwezi wa tatu, Ninakuombea kwa Bwana mwezi huu ukawe ni mwezi wako wa kuinuka kuangaza tena katika jina la Yesu

Nikiwa katika maombi Bwana aliniambia kuna watu wengi atawainua mwezi huu,kuna watu wengi atawafungua na kuwaachilia huru ili wainuke na kuangaza tena

Nikiwa katika maombi niliona mtu aliyekuwa katikati ya jangwa na Bwana akaniambia hilo ni jangwa la kiuchumi hakuna kinachosogea, mwingine ni jangwa la ndoa

Ndoa haina amani tena, mwingine ni jangwa la utasa,mwingine ni jangwa la mahusiano huoni mwanga tena, mwingine ni kesi huoni k**a utapata haki yako tena

Katika kuomba niliona Bwana akifunua mito katikati ya lile jangwa, gafla likabadirika na kuwa bustani ya Bwana na yule mtu akaanza kutabasamu na kufurahi, Na Bwana akaniambia mwache afurahi maana ndio majira yake

Ndipo Bwana aliponipa neno hili
Isaya 60:1,10
Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja,Na utukufu wa BWANA umekuzukia.

It is your time to shine, ni majira yako ya kuinuka na kuangaza tena, ninakuombea Mwezi wa tatu Bwana ageuze kila jangwa ulilolipitia kwa muda mrefu akupe neema ya kuinuka na kuangaza tena katika jina la Yesu

Nataka ukili maneno haya kwa imani na uamini kabisa moyoni na yatatokea kwako katika mwezi huu wa tatu

Kili kwa kuandika hapo na kisha share na watagi marafiki na ndugu zako wapokee neema hii ya mwezi wa tatu

"Mwezi wa tatu ninainuka na kuangaza tena AMEN"

Mtumishi Japhet
Kagera
0625-46-78-40
Tanzania

01/02/2025

ULINZI WA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO

Kuna watu wanashangaa kwanini mpaka sasa yuko hai, kwanini mpaka sasa bado yupo kwenye hicho cheo kwanini mpaka sasa yupo kwenye hii ofisi
Kwanini mpaka sasa bado yuko kwenye ndoa
Kwanini mpaka sasa biashara yake haijafa

Kwanini mpaka sasa biashara yake inachanua, kwanini mpaka sasa ndoa yake ina amani, kwanini mpaka sasa bado anakibari

Hawajui ya kwamba Mungu anakusaidia na kukutetea, pamoja na mabayaaa yoote waliyokufanyia bado uko hai, pamoja na vikao vyote vya uovu walivyokukalia aaaaah bado uko hai

Pamoja na uchawi woote waliokuloga bado uko hai maana mtetezi wako yu hai. Ni kweli wanakazana kukulaani njia panda, kwenye madhabahu zao za kichawi na Mungu nae anakazana kukubariki maana wewe ni mtoto wake last born wake

Hawajui kwamba amekuchora kwenye vitanga vya mikono yake, wao wamekujua ulipozaliwa ila Mungu alikujua wewe hata kabla ya misingi ya ulimwengu kuumbwa, hawajui mlikotoka na huyu Mungu, hawajui maagano mliyowekeana na Mungu

Niko hapa kukwambia Mtu wa Mungu wala usiogope hawawezi kukulaani ikiwa umebarikiwa na Bwana utamlaanije aliyebarikiwa na Mungu.

K**a unaamini Andika "NIMEBARIKIWA HAKUNA WA KUPINGA"

Usiache kushare ujumbe huu.....

Mtu wa Mungu umebarikiwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mtumishi Japhet
0625-46-78-40
KGR

24/01/2025

Somo: MBINU ZA SHETANI KWA
MTU ALIYEOKOKA

Lazima ujue kwamba shetani ana mbinu zake anazozitumia ili kuwarudisha watu waliookoka nyuma. Hutumia mbinu hizo kuwafanya watu wengi waiache imani halisi ya wokovu. Na ndiyo maana Mungu anatuambia katika 2WAKORINTHO 2:11“Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.” Neno fikra kwa lugha nyingine ni mbinu au mipango. Siku zote na wakati wote Shetani ana mipango miovu na iliyojaa hila na mbinu kinyume na watu wa Mungu.

SASA TUONE MBINU ZAKE

1. Atakuzuia usiifahamu kweli ya Neno la Mungu. Shetani anayajua makanisa yanayofundisha kweli ya Neno la Mungu, hivyo atahakikisha watu wanaenda sehemu ambazo hakuna kweli ya Neno la Mungu, na atawazuia wasiende mahali penye kweli ya Neno la Mungu. Maana anajua mtu akiijua kweli ya Neno la Mungu, anawekwa huru, YOHANA 8:32,36.

2. Utashangaa siku ya ibada vikwazo vingi vinaibuka ili tu usihudhurie ibada. Siku ya ibada anakuletea wageni kuja kukutembelea, ili usihudhurie ibada. Namna ya kushinda mbinu hiyo, wakaribishe wageni wako kanisani na uje nao ibada; waambie tutaongea baada ya kurudi kanisani. Muda wa kwenda kanisani unafika, anaanza kukuonyesha kazi za nyumbani, “ona hujaosha vyombo, unatakiwa ufue, unatakiwa upike sasa N.k” Au utashangaa tumbo, kichwa, miguu imeanza kuuma ghafla, anakuletea dalili zote za homa. Au unashangaa umejaa hasira ghafla na hutamani kuja kanisani. Usikubaliane na mbinu zake. Jiandae njoo ibada/kanisani.

3. Atakushawishi uiache njia ya kweli. Kushawishi ni kubadili nia ya mtu kwa kumuumbia mawazo mengine tofauti na mawazo aliyokuwa nayo. Aliitumia mbinu hii kumshawishi Daudi kuwahesabu Israeli, kinyume na nia/mawazo ya Mungu, 1MAMBO YA NYAKATI 21:1 “Tena shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli.”

Ni rahisi kuanza kuona unakuwa na mawazo mengine juu ya wokovu, au anakushawishi kwa kukuumbia mawazo ya dhambi zile za zamani; au wakati mwingine atakushawishi kupitia watu, MITHALI 1:10-16.

4. Atakufanya usiwe mtii kwa Mungu. YAKOBO 4:7 “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.” Utaona nia ya shetani wakati wote hapendi watu wamtii Mungu ili iwe rahisi yeye kushinda. Kumtii Mungu ni kuyatii maagizo yake katika neno lake, hivyo uwe tayari kumtii Mungu.

5. Atakufanya uyapende zaidi mafundisho ya mashetani kuliko Neno la Mungu la kweli. Kwa kutumia mbinu hii Shetani amewakokota watu wengi sana na kuwatoa kwenye kweli ya Neno la Mungu na kuwapeleka kwenye mafundisho ya mashetani, 1TIMOTHEO 4:1.

6. Atakuja k**a malaika wa nuru. Shetani haji k**a Shetani moja kwa moja kwa mtu. Maana akija k**a Shetani ni rahisi mtu kujua kwamba huyu ni Shetani. Ila anakuja kwa njia mbalimbali ambazo mtu wakati mwingine ni vigumu kutambua k**a huyu ni Shetani.

Anaweza kuwatumia watu wa karibu nasi, au hata watu wanaojiita mitume, manabii, wachungaji, wainjilisti n.k. Usikubali mbinu za Shetani zifanikiwe kwako, 2WAKORINTHO

Mtumishi Japhet
0625-45-78-40
KGR

20/01/2025

👇👇👇
*NENO LA WIKI*
Nasikia haya Maneno yakipiga kelele ndani yangu Mchana huu sijui ni kwa ajili ya nani. Ila najua kuna mtu unahitaji kusikia Maneno k**a haya mchana wa leo.

Hayo maumivu uliyonayo moyoni mwako kutokana na pito unalolipitia yataisha tu. Hukuumbwa uwe mtu wa kulia na kuumia tu kila wakati

Ni kweli pito ulilonalo linakunyima usingizi na kukufanya uwe mtu wa kulia, Mungu amenituma kukwambia hayo machozi yataisha tu

Ufunuo wa Yohana 7:17
Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.
Hata k**a huna Bega la kulilia, Bwana amenituma kukwambia yeye atakufuta machozi katika macho yako hutalia tena kwa maana yeye atakuchunga na tena atakuongoza kwenye chemichemi za maji ya uhai

Amenituma kukwambia usiogope na wala usikate tamaa. Milango itakufungukia tu, Ile Milango ya kazi, Milango ya Biashara, Milango ya kiuchumi itakufungukia tu katika jina la Yesu

Nimekuombea na kukubariki naam nawe umebarikiwa na wiki yako imebarikiwa katika jina la Yesu. No more tears again in Jesus might Name.

Jiandae na wewe kushuhudia. Mwaka huu hautaisha naona ushuhuda mkubwa sana kwenye maisha yako ambao masikio ya watu yatawasha katika Jina la Yesu.

Comment AMEN

10/11/2024

SOMA MPENDWA MUNGU ANAKUPENDA USIKATE TAMAA
Biblia inasema
Zaburi 34:18
BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na waliopondeka roho huwaokoa.
K**a anasema Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, maana yake wapo wanaotembea kwa jinsi ya kibadamu utawaona wako sawa ila mioyo yao imevunjika na kupondeka
Tuna watu wengi sana ambao wako maofisini ni kweli wanafanya kazi ila mioyo yao imevunjika na kupondeka sana kiasi ambacho wanajilazimisha sana kuendelea na hiyo kazi
Tuna watu wengi sana ambao wako kwenye ndoa, wengine wako kwenye mahusiano, wengine wako kwenye partnership lakini mioyo yao imevunjika, wanajitahidi sana kujilazimisha kucheka ila moyoni wana majeraha makubwa na mazito sana
BAADHI YA MAMBO YANAYOVUNJA MIOYO YA WATU
kuna mambo mengi sana ambayo yanaweza kuvunja moyo wa mtu leo nataka tuangalie jambo moja tu :-
1.Maneno
Ni hatari sana kwa taasisi, kikundi, kampuni, familia,ndoa au mahusiano kuruhusu maneno ndio yawaongoze ni hatari sana sana
Mithali 15:1
Jawabu la upole hugeuza hasira;
Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
Biblia inataka tujue kuwa kuna Neno liumizalo, au kuna maneno yaumizayo na hili neno liumizalo ni watu wachache wanaweza kuhandle pressure inayokuja na hilo neno
Waliowengi hilo neno liumizalo huwa linachochea gadhabu, hasira na chuki inayotokana na moyo kuvunjika, na ndio maana sikila anaecheka na wewe kazini anamaanisha upendo, mwingine anajilazimisha tu ila moyoni ana gadhabu
Ayubu 34:6
Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo;
Jeraha yangu haiponyeki, nijapokuwa sina makosa.
Waliowengi mioyo yao imevunjika baada ya kuhesabiwa kuwa waongo wakati ni wenye haki, wengi mioyo yao imejikuta na majeraha mazito sana yasiyoponyeka
Wamehesabiwa makosa kwenye familia, kwenye maofisi wanakofanya kazi wakati hawana kosa, ni wenye haki ila wamehesabiwa kuwa waongo
K**a Mungu asipokuponya moyo wako madhara yake ni makubwa hata kwenye afya yako na kwenye afya ya akili na maisha yako kwa ujumla
Leo ninakuombea katika jina la Yesu, Bwana auponye moyo wako kwa namna ambayo utaendelea mbele, Taifa linakuhitaji Bado, familia yako inakuhitaji bado
Usikubali kufia hapo, Bado lingalipo tumaini, pokea uponyaji kwenye moyo wako leo kwa jina la Yesu. Kumbuka Yesu alipokutoa, kumbuka ni mangapi Yesu amekutetea.
K**a hakukuacha kule hata hapo hata kuacha inuka songa mbele kwa jina la Yesu.

MTUMISHI JAPHET
0625 467 840
KGR

02/10/2024

*MWEZI HUU WA KUMI, UKAWE MWEZI WAKO WA KUONA FURSA*

Mungu alipowaadhibu watu kwa maji katika nyakati zile za Nuhu biblia inatwambia yakuwa safina aliyokuwemo Nuhu na familia yake na baadhi ya wanyama ilielea juu ya maji, ardhi yote ilijaa maji kwa mda wa siku Mia na hamsini, kwahiyo kwa kipindi chote ambacho maji yalikuwa juu ya nchi Nuhu na familia yake waliishi kwenye safina lakini biblia inasema hivi👇🏻

*👉Mwanzo 8:5 Maji yakapunguka-punguka hata mwezi wa kumi; mwezi huo wa kumi, siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.*

👆🏻Kwenye haya maandiko utaona yakuwa matumaini ya maji kukauka na maisha mengine ya Nuhu na familia yake kuendelea baada ya ile gharika dalili zake zilianza kuonekana TAREHE YA KWANZA YA MWEZI WA KUMI hasa vilipoanza kuonekana vilele vya milima..

*▶️Kwanini nimekupitisha kwenye hili andiko? Ni ili uone yakwamba mwezi wa kumi umebeba dalili ya maisha yako kwenda viwango vingine kwa jinsi ya kiroho, kuonekana kwa vilele vya milima katika mwezi wa kumi kwa Nuhu ilikuwa ishara ya kuanza maisha mengine ya viwango zaidi ya walivyokuwa navyo ndani ya safina, kwenye safina walipata kila kitu lakini hawakuwa na uhuru wa kuendesha shughuri za kawaida za kila siku za kimaisha, walitamani viwango vingine lakini haikuwezekana kwa kipindi hicho ambacho maji yalitanda juu ya nchi, lakini milima ilipoanza kuonekana katika mwezi wa kumi ilikuwa ni ishara ya Nuhu kukaribia kwenda viwango vingine kimaisha..*

✔️K**a mwezi wa kumi ulibeba ishara ya Nuhu na familia yake kwenda viwango vingine vya maisha hasa baada ya kuonekana milima maana yake nikuwa mwezi huu wa kumi umebeba ishara ya wewe kwenda viwango vingine vya kimaisha, mwezi huu wa kumi unaenda kuviona vilele vya milima (fursa) iliyokuwa haionekani katika miezi iliyopita..

*▶️Nakuombea kwa Mungu wewe unayesoma ujumbe huu yakuwa mwezi huu wa kumi ukaanze kuviona vilele vya milima kwenye maisha yako, ukaanze kuona mpenyo katika hayo unayoyapitia, ukaone fursa zako za maisha kwa jina la Yesu, Bwana akakupe kuanza kuona fursa za kazi kwa jina la Yesu, Bwana akakupe kuona neema ya kuolewa kwako kwa jina la Yesu, Bwana akakupe kuona neema ya kuzaa kwako kwa jina la Yesu, Bwana akakupe kuona ndoa yako ikiwa na amani kwa jina la Yesu, ooh lakini pia Bwana akakupe kuona neema ya kupanda kiuchumi kwa jina la Yesu, Bwana akakuondolee mikosi na laana na mwezi huu wa kumi ukawe mwezi wako wa kwenda viwango vingine kwa jina la Yesu, k**a unaamini andika kwa imani 'AMEN, NINAPOKEA KWA JINA LA YESU..'*

Mwisho..

*👉Yeremia 17:7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.*

Mungu wa mbinguni awabariki sana 🙏

Mtumishi Japhet
0625467840
MZA

24/06/2024

Asantee Mungu Kwa Uzima na uhai Pongezi kubwa Kwa Mama Mzazi....
Happy birthday to me

Zaburi 108:1-7........

Zawadi zitumwe na Wishes....

07/06/2024

KWANINI UOMBEE FAMILIA YAKO!.

Zaburi 127:1
''BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure. ''

Kibiblia neno nyumba linasimama k**a mbadala wa neno familia, ndoa, ukoo au jengo la mahali ambako watu wanaishi,
Mfano,

Mwanzo 20:18
''Maana BWANA alikuwa ameyafunga matumbo ya watu wa NYUMBANI mwa Abimeleki, wasizae, kwa ajili ya Sara mkewe Ibrahimu.''

· KWANINI UOMBEE FAMILIA YAKO.

01. Familia inaweza ikabeba adhabu kwa sababu ya makosa ya mmoja kutoka katika familia hiyo.

Mwanzo 20:18
''Maana BWANA alikuwa ameyafunga matumbo ya watu wa nyumbani mwa Abimeleki, wasizae, kwa ajili ya Sara mkewe Ibrahimu.''

Familia ya Abimeleki yote yaani wote wa jamaa yake alioishi nao matumbo yao ya uzazi yalifungwa ili wasipate kuzaa kwa sababu tu ya kosa la Abimeleki kumchukua mke wa IBRAHIM akitaka kumuoa.

Je familia yenu au ukoo wenu unapata adhabu gani, na
Je ni kosa la nani?.

Mpendwa yaimarishe magoti yako kwaajili ya familia yako, maana kwa kukosekana mtu anayesimama kwaajili ya familia yenu ndiko kunakoifanya familia iyumbe.

Ezekieli 22:30-31
"Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.
Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao, asema Bwana MUNGU.

02. MUNGU anaweza kuizingira familia kwa sababu ya ucha MUNGU wa kiongozi wa familia.

Ayubu 1:10
''Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na NYUMBA yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.''

Ayubu k**a kiongozi wa familia alikuwa mcha MUNGU, na
Kwasababu ya ucha Mungu wake familia ilizungukwa na ukigo wa Mungu.

Ukiona ucha MUNGU umesababisha kuzingirwa na MUNGU basi ujue kwamba kuna familia au viongozi wa familia sio wacha MUNGU hivyo hakuna kuzingirwa na MUNGU ndio maana majanga hayaishi.

Ukiokoka wewe na ukajitambua, kiroho wewe unakuwa lango la familia na kiroho unakuwa kiongozi wa familia au ukoo hivyo familia yako wanaweza kukaa salama kwa maombi yako.

03. Nyumba/ukoo/familia inaweza kubeba laana.

Mithali 3:33
''Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki.''

Inawezekana unatokea familia iliyolaaniwa labda kwa sababu kiongozi wa familia alimwaga damu ya mtu asiye na hatia.

Inawezekana unatokea ukoo uliolaaniwa kwa sababu ya maovu mabaya yaliyokithiri kwa watu wanaotokea ukoo huo.

Wewe uliyepata neema ya kuokolewa na Bwana YESU inakupasa sana kujinasua kwenye laana za ukoo au familia au nyumba maana usipojua kuomba unaweza hata wewe ukashikiliwa na laana hiyo hiyo.

Daudi alikuwa ameokoka kuliko hata wewe, alikuwa muombaji kuliko wewe na alikuwa mtumishi wa MUNGU,
lakini ikulu au ofisi aliyoirithi ilikuwa na adhabu kwa sababu ya makosa ya mtangulizi wake,

Madhara ya adhabu ya ofisi hiyo yalimpata hadi Daudi ambaye hakuhusika katika kosa hilo,

2 Samweli 21:1
''Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa BWANA. BWANA akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni.''

Jifunze kuombea familia, nyumba au nafasi unayoiingia kuirithi baada ya alikuwepo kuondoka,

· Inawezekana Nafasi/ofisi yako ina laana hivyo hata anayeingia hapo laana inaambatana naye, Rafiki jitambue na omba ili kujiondoa kwenye agano/laana ya familia, ukoo au nyumba.

· Kuna nyumba zimejengwa juu ya ardhi iliyobeba laana hivyo lazima ujue kuomba ili kujitenga na laana iliyo katika ardhi kwa ajili ya watakaojenga juu yake.

Yoshua 6:26
''Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za BWANA mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.''

Vipi k**a unakaa katika ardhi ambayo kila mtoto wa kwanza kuzaliwa lazima afe?

Ndugu, unahitaji sana kuomba juu ya familia, nyumba au ukoo na ardhi yake.

04. Familia inaweza kubarikiwa na MUNGU kwa sababu ya uwepo wa Mtumishi wa MUNGU anayeishi maisha matakatifu.

Mwanzo 39:5
''Ikawa tokea wakati alipomweka awe msimamizi juu ya nyumba yake, na vyote vilivyomo, Bwana akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Mbaraka wa Bwana ukawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.''

Hizi ni dondoo chache kwaajili ya kukujengea msukumo wa kuombea familia yako.

Kristo Yesu na akusaidie kulielewa hili.

10/04/2024

SAFARI YA KANANI HAIJAWAHI KUWA RAHISI

Safari ya kuielekea Kaanani yako haijawahi kuwa nyepesi, hata safari ya Bwana wetu Yesu kristo ya kuuokoa ulimwengu haikuwa nyepesi ndio maana hata Yesu alifika mahali akaomba kikombe kimwepuke.

Wewe sio wa kwanza kukata tamaa, wewe sio wa kwanza kuchoka, wewe sio wa kwanza kutamani kuacha, wewe sio wa kwanza kuomba hicho kikombe kikuepuke,katika mambo hayo yote omba mapenzi ya Mungu yatimizwe.

Naongea na mtu ambae kila ukikalibia kuinuka lazima kuna vikwazo au vita vitainuka tu yaani hiyo ni lazima, naongea na mtu ambae ukikalibia kufika kaanani yako eidha utachukiwa na kila mtu bila sababu.

Mwingine utaandamwa na roho za magonjwa,mwingine vita vitainuka kila kona,na hali hii inakuumiza sana na unajiuliza mbona sioni k**a haya yanawatokea wengine?

Nimetumwa kukwambia hakuna aliyeingia Kaanani kirahisi ni vile tu wanakusimulia rahana za nchi ya ahadi bila kukwambia gharama za kuingia hapo kwenye nchi ya ahadi.

Nimetumwa kukwambia jambo hili hakuna aliyeingia kaanani au inchi yake ya ahadi bila kupigana na majitu, kila mtu ana majitu amepambana nayo kwanza kwanini wewe unafikili ni lelemama kiasi hicho?

Unafikili hayo majitu yatakuacha tu kirahisi uingie hapo kwenye maziwa na asali? Harafu hayo majitu yaende wapi sasa noooooo you have to fight!!!! Lazima upigane acha kujionea huruma.

Sasa unaweza kuelewa huu mstari leo

✍️Kumbukumbu la Torati 31:6
Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana BWANA, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.

Nimetumwa kukwambia uwe hodari na moyo wa ushujaa kanani lazima uingie uwe na jicho moja utaingia tu, iwe mvua utaingia tu, uwe na mguu mmoja utaingia tu pambana usijionee hurumaaa

Wewe endelea tu kuomba harafu baki na kiwoga chako na kujihurumia Kanani utaisikia tu, Biblia imesema uwe hodari na moyo wa ushujaa maana yake kuna nafasi ya maombi na kuna nafasi ya kupambana kusimama kiumeee

Ngoja niishie hapa kwa leo

K**a umenielewa jisemeshe tu kwa imani kwa kukoment "Kanaani yaangu lazima niingie katika jina la Yesu"

Kisha watag marafiki zako wambie kaanani lazima uingie.Harafu share ujumbe huu na kwa wengine na Mungu atakubariki

Mtumishi Japhet
Kagera
Tanzania

06/04/2024

FAHAMU MAMBO MATANO(5) YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUFANYA MAOMBI YENYE USHINDI.

*MAOMBI*;Ni Mawasiliano ya Kiroho Kati ya Mwanadamu na Mungu,Uhusiano wa pande mbili ambapo Mwanadamu asiongee tu Kwa Mungu bali pia Amsikilize Mungu yale anayomwambia!

✅Kwahiyo Maombi kwa Mungu ni Mazungumzo Kati ya mtoto na Baba yake!

✅Maana yake ni hii Unapoingia kwenye Maombi,Mtu unaongea au Unasema na Mungu,Na wakati huo Mungu yupo kimya Anakusikiliza,! Ukishamaliza ,Usiondoke kaa Kimya nawewe Msikilize Mungu nayeye aseme au Aongeee na Wewe,hii ndio maana ya Maombi!

*Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza*
(Zaburi 91 :15)

✅Sasa watu wengi wamezoea wakiingia tu kwenye Maombi wanazungumza wao tu wakishamaliza Wanaondoka!

Sikia Usikariri kuwa Mungu anapelekewa Maombi halafu anajibu baadae au kesho,hapana,Mungu ana weza Kujibu Maombi yako hata wakati ukiwa Kwenye Maombi!

*Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia*
(Isaya 65 :24)

✅Tatizo lako Umechomoka hata kabla Mungu hajakujibu!

Sasa basi kwa Kuwa Maombi ni Mazungumzo Kati ya Mtoto na Baba yake Kuna Vitu lazima uvizingatie Ili Mazungumzo hayo yaende vizuri;

1️⃣ Hakikisha Hali ya Moyo wako Imekaa vizuri!

*Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao*,nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. *Je! Ni laiki yangu niulizwe na wao katika neno lo lote?*
(Ezekieli 14 :3)

2️⃣Hakikisha Una Utulivu wa Mwili wako;

✅Maana yake Usizungumze na Mungu ukiwa Umechoka au unasikia Usingizi, Kwasababu hata Mungu akiongea na wewe hutasikia Wala kumwelewa!

3️⃣Ondoka Maeneo yenye watu au watoto au yenye Makelele!

✅Zina kabsa simu Yako,Redio,Tv nk

📌Angalia Mfano wa Yesu;

"" Naye Yesu aliposikia; hayo, aliondoka huko katika chombo, *akaenda mahali pasipo watu*, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka mijini mwao""
(Mathayo 14 :13)

""Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, *akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu* akaomba huko.""
(Marko 1 :35)

""Hata kulipokucha *alitoka akaenda mahali pasipokuwa na watu* makutano wakawa wakimtafuta-tafuta, wakafika kwake, wakataka kumzuia asiondoke kwao.""
(Luka 4 :42)

"" Lakini yeye alikuwa akijiepua, *akaenda mahali pasipokuwa na watu* akaomba.""
(Luka 5 :16)

4️⃣Tumia au Tenga Muda ambao utakuwa na Utulivu!

✅Mfano Asubuhi na mapema mara nyingi ni Muda Mzuri Sana uliotulia na hakuna Makelele na kwamba Unakuwa pia hujachoka Wala Hauna Usingizi kwani Umeshatoka kulala!

📌Yesu alitumia Fursa hii ya Asubuhi

📌Mussa pia Alikuwa na Muda tulivu wa kusemeshana na Mungu

K*t 33:7-11

5️⃣Fanya Maombi kwa Muda wa K*tosha Katika ROHO MTAKATIFU

✅Kadri Unapokuwa na Muda mrefu kwenye Maombi ndivyo na Mungu anapata Nafasi ya Kuongea na wewe na kukujibu Maombi yako yote!

*Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu*
(Waefeso 3 :20)

Mungu awabariki Sana

AMEN.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Category

Website

Address


Dar Es Salaam