UVCCM Kata ya Kigogo

Directions Website

UVCCM Kata ya Kigogo Ukurasa Rasmi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Kigogo. Kauli Yetu: Kulinda na Kujenga Ujamaa

UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (UVCCM)UNAUNDWA KWA MUJIBU WA KATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI TOLEO LA MEI 2005 ( CCM) SEHEMU YA NNE, IBARA 129 (1) A

UTANGULIZI;

Umoa wa vijana wa CCM ni chombo kinachowaunganisha vijana wake wa Tanzania wanao unga mkono sera , siaasa na itikadi ya ya chama cha mapinduzi. Shabaha za chama cha mapinduzi zakuunda umoja wa vijana kuwa shule ya kuandaa wanachama safi na viongozi bora wa CCM . kwa msabaha huo, Umoja wa vijana wa ccm Utaandaa vijana kuwa raia wema wa Taifa letu na kwamba chombo hiki nisawa na tanuri la chuma la kuhokea makada wazuri. Kwahiyo umoja wa vijana wa CCM ,unawajibu wa kuongeza shughuli zinazohusu maendeleo na maslahi ya vijana nchini, chini ya uongozi wa CCM na unakiri jukumu lake katika historia ya Taifa ya kuimarisha umoja wa kitaifa , kuendeleza mapinduzi ya kijamaa ya kidemokrasia na mapambano ya ukombozi katika Afrika, na duniani kote. Umoja wa Vijana wa CCM unatambua kuwa harakati za kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kujenga jamii iliyo sawa nchini Tanzania, Afrika na duniani kwa ujumla kunahitaji chombo madhubuti kinacho unganisha fikra na vitendo vy vijana wote , wakulima na wafanyakazi ,wanafunzi, vyama vya hiari, wafanya biashara na vijana wengine wa sekta za binafsi. Kabla ya umoja wa vijana wa ccm kuundwa , Vijana wa CCM wa Tanzania walikuwa katika malezi ya vyama vya vijana vya afro Shirazi Part (ASPYL) na Tanganyika African national Union (TYL), kabla yakuwa jumuiya ya wananchi katika chama cha mapinduzi. Umoja wa vijana wa CCM tunaounda , unakusudia kurithi yale yote mazuri ya ASPYL na TYL pamoja na itikadi ya vyama vya ASP na TANU na hasa kwa kutambua nafasi ya kihistoria ya vyama hivyo katika kumuondoa mwafrika kwenye unyonge, kunyanyaswa na kudharauliwa ili kufikisha kwenye uhuru wa kuheshimiwa. Umoja wa vijana wa CCM tunaounda , unakusudiwa uwe madhubuti katika muundo wake , na hasa kifikra na vitendo vya kufutilia mbali aina zote maki ya ukoloni mamboleo , ubeberu, unyonyaji, dhuruma, uonevu na unyanyasaji nchini . kwakuwa umoja wa vijana CCM unazingatia kwamba nguvu za vyama ndio lasilimali kuu ya Taifa letu na kukubali kimsingi dhana kwamba vijana ni viongozi wa Taifa la leo na kesho, tunataka umoja wa vijana wa ccm, uongoze harakati za kutetea maslahi ya vijana na uwe kiungo kati ya vijana wanamapinduzi wa Tanzania na wanamapinduzi wenzetu duniani kote na kuhakikisha kwamba chini ya uongozi wa CCM azma tuliyojiwekea ya ujamaa na kujitegemea tunaifikia

Picha na matukio mbalimbali kutoka katika mkutano mkuu wa CCM kata ya Kigogo uliofanyika tarehe 27 Septemba 2026 katika ...
29/09/2026

Picha na matukio mbalimbali kutoka katika mkutano mkuu wa CCM kata ya Kigogo uliofanyika tarehe 27 Septemba 2026 katika ukumbi wa CCM kata. Ambao uliambatana na uchaguzi mdogo wa mwenyekiti wa CCM kata na katibu wa Siasa na uenezi kata.

Hongereni sana viongozi mliochaguliwa. UVCCM kata tunawatakia utekelezaji mwema wa majukumu yenu na tunaahidi kuwaunga mkono katika kulinda na kutetea maslahi ya chama na taifa kwa ujumla.


HERI YA SIKU YAKO YA KUZALIWA NDUGU RASHID MOHAMED Rashfody Wakanda Swahili - KATIBU WA HAMASA NA CHIPUKIZI (K) KIGOGO.
10/07/2026

HERI YA SIKU YAKO YA KUZALIWA NDUGU RASHID MOHAMED Rashfody Wakanda Swahili - KATIBU WA HAMASA NA CHIPUKIZI (K) KIGOGO.

Picha na matukio mbalimbali katika ziara ya kiutendaji ya katibu wa UVCCM wilaya ya Kinondoni ndugu Amos Richard  katika...
31/03/2026

Picha na matukio mbalimbali katika ziara ya kiutendaji ya katibu wa UVCCM wilaya ya Kinondoni ndugu Amos Richard katika kata ya Kigogo.

Hakika Kigogo ipo imara katika kulinda na kutetea maslahi ya Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
VIVA VIJANA VIVA.

Cc:

Address

Kigogo
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UVCCM Kata ya Kigogo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share