10/02/2025
TAASISI YA NYOTA YA FARAJA KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA DARUL ISTIQAMA FOR ISLAMIC DEVELOPMENT
TUMEANZA KUPOKEA VIFAA MBALIMBALI KWA AJILI YA FUTARI KWA MAGEREZA YA UKONGA NA SEGEREA KWA AJILI YA FUTARI NA DAKU
UKONGA
WALIOTIA NIA NI - 620
- Kwa Siku watakula Mchele Kg. 155.
- Kwa Mwezi Watakula Mchele Kg. 4,650.
- Maharage Kg. 300
- Sembe Mifuko 10
- Tende Box 10
- Sukari Mifuko 5
- Tambi Box 5
- Mafuta ya Kula Dumu 3
- Viazi Mbatata Loba 2
- Kanzu Balo 2
SEGEREA
WALIOTIA NIA NI - 600
- Kwa Siku Watakula Mchele Kg. 150
- Kwa Mwezi Watakula Mchele Kg. 4,500
- Maharage Kg. 300
- Sembe Mifuko 10
- Tende Box 10
- Sukari Mifuko 5
- Tambi Box 5
- Ngano Mifuko 5
- Mafuta ya Kula Dumu 3
MAHITAJI MENGINE MUHIMU:
- MISAHAFU YA MATINI - 500
- JUZUU AMMA - 1,000
- MIKEKA YA KUSWALIA - 100
FIKISHA DUKANI KWA AL-HAJJ SAIMU GWAO MKABALA NA MSIKITI WA MTORO MKABIDHI USTADH. MUHIDINI
MICHANGO YOTE IPITIE: TANZANIA COMMERCIAL BANK AKAUNT NAMBA - 341204000409 AU LIPA NAMBA 7425770 JINA: DARUL ISTIQAMA FOR ISLAMIC DEVELOPMENT
AU WASILIANA NASI KWA NAMBA
0752249858
0785949076
(Hussein Mchomolo)
0715580807
(Kudura Sama)
FIKISHA SADAKA YAKO MASJID HAQQA BUGURUNI ROZANA MUULIZIE IMAMU HAMISI
NYOTA YA FARAJA
_Mwangaza kwa waliokata tamaa_
https://www.instagram.com/p/DF5BPbPIkCN/?igsh=MWd2YmdiYnhtMWwzOQ==
04/08/2022
Assalam alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh
Habarini la Majukumu
Kampeni yetu ya MSAHAFU WANGU bado inaendelea tusikose fadhila hizi, NUNUA MSAHAFU wako Fikisha Dukani kwa USTADH SAIMU GWAO Kariakoo Mkabala na Msikiti wa Mtoro
Wabillahi Tawfiq
30/11/2021
Assalam Alaykum Waramatullah wabarakatuh
NYOTA YA FARAJA
OMBI LA JUZUU AMMA NDOGO 300 NA MISAHAFU YA TAFSIRI YA KISWAHILI 10
Thamani ya Juzuu 1 @ ndogo ni 300 × 300 = 90,000/= na thamani ya Msahafu mmoja @ 10,000 × 10 = 100,000/=
Tunaomba tuendelee Kuchangia kwa ajili ya Vijana wetu, faida ya Kusomesha tena Qur'an fadhila zake sote tunazifahamu, tuwekeze kwa ajili ya Makaburi yetu na akhera yetu (Swadaqatul Jaalia)💰
Fikisha moja kwa moja Dukani kwa Ustadh. Saimu Gwao Mkabala na Msikiti wa Mtoto Kariakoo Mkabidhi Mwihidini
Au tupigie tutafwata ulipo Inshaa'allah, kwa namba zifuatazo:
0752249858, au 0776758241.
Au anayetaka kuchangia moja kwa moja, basi tuma Mchango wako kupitia
M - PESA 0752249858
: "Hussein Mchomolo"
Wabillahi Tawfiq
NYOTA YA FARAJA
Mwangaza kwa waliokata tamaa
24/11/2021
Assalam Alaykum Waramatullah wabarakatuh
TAARIFA YA ZIARA ZETU GEREZANI
Kwa ajili ya kuendelea kuutumikia Ummah hasa ndugu zetu walioko Mahabusu, Viongozi wa NYOTA YA FARAJA tumefanya Ziara katika Magereza ya Singida Mjini na Dodoma
Changamoto ni nyingi sana, kiasi tunalazimika wakati wote kuwaomba Waislamu waendelee Kutuunga Mkono kwa kujitolea kile walichojaaliwa ili walau kwa uchache tupunguze kwani hali iliyopo ni Mtihani
Bado kuna hitajio Kubwa la vitu Mbalimbali kwa ajili ya Mahabusu na Wafungwa, k**a vile
NGUO ZA KIUME NA ZA K**E, SABUNI ZA KUFULIA NA ZA KUOGEA, MISWAKI, DAWA ZA MENO
YA
Kuna mahitaji ya dharura yanatakiwa yawafikie ndugu zetu walioko Gereza la Singida, mahitaji hayo yako Dar, hivyo tunaomba Tupate fedha Tsh. 56,000/= kwa ajili ya Nauli ya Mtu mmoja ya kwenda tu, na nauli ya Mzigo
Vitu hivi vinatakiwa kesho kwa Tawfiq yake ALLAH vifike Singida Inshaa'allah, hivyo TUNAKUOMBA EWE NDUGU KATIKA IMANI kutuwezesha kiasi hicho cha Tsh. 56,000/=
Bado tunapokea vifaa mbalimbali kwa ajili ya ndugu zetu waliko Magerezani, vifaa hivyo ni:
NGUO ZA K**E NA KIUME (Kanzu/Hijabu) MADILA, VIATU, SABUNI, NK.
Kwa mawasiliano:
0752249858
0715580807
Wabillahi Tawfiq
NYOTA YA FARAJA
Mwangaza kwa waliokata tamaa
14/11/2021
Assalam alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh
MAOMBI YA KUPATIWA (Laptop)
Bado hatujapata!!
Ndugu zangu Waislamu tunaomba kwa yeyote Allah aliyemjaalia Uwezo na wasaa wa Kuifanya Kheri hii Muhimu kwa ajili ya wepesi wa Harakati zetu basi akimbilie kheri hii.
Tunashida sana ya ya aina yoyote, si lazima iwe MPYA hapana, tunataka hata Mtumba ila iwe mzima tu, itakuwa umetusaidia sana kwa Majukumu yetu
Allah anatunasihi:
"Na toeni katika tulivyo kupeni kabla hayajafikia mmoja wenu Mauti, tena hapo akasema: Mola wangu mlezi! Huniakhirishi muda kidogo nipate kutoa Sadaka, na niwe katika Watu wema?" (Q. 63:10)
Kwanini Ndugu yangu ufike wakati wa kujilaumu na Kujuta? Wakati ni sasa ukiwa Hai wekeza kwa ajili ya Nafsi yako na Akhera yako.
KWA YEYOTE ATAKAYEJAAIWA NA KHERI HII TUWASILIANE KWA NAMBA:
+255752249858
Wabillahi Tawfiq
NYOTA YA FARAJA
Mwangaza kwa waliokata tamaa
06/11/2021
BAADA YA KUTOKA MATOKEO YA DARASA LA SABA, WAZAZI AMBAO WATOTO WAO WAMEFAULU WAMEANZA KUHAMA MIJI KWA KUHOFIA KUSHIKWA ENDAPO WATOTO HAWATOENDA SHULE!!
NYOTA YA FARAJA
Tunaendelea Kukuomba wewe ambaye Mwenyezi Mungu amekujaalia nafasi basi tuwasaidie watoto Masikini na Mayatima
Hadi sasa tuna idadi ya Watoto 129 ambao Wazazi wao wamesema Bayana kuwa: "Wanahama Mjini na kwenda Mashambani kwani hawana uwezo wa Kuwasomesha watoto wao."
"Huyu mtoto amenileta Majanga, nilimwambia akifaulu atanifungisha, sina uwezo wa Kumsomesha, leo Majibu yametoka AMEFAULU!! Huyu mtoto!!" Alisikika Mzazi mmoja akimlaumu mtoto wake kwa nini amefaulu kwenda Sekondari.
Mwenye Jukumu la Kuwasaidia MAYATIMA na WASIO JIWEZA ni langu mimi na Wewe, tushirikiane ili watoto hawa January waweze kwenda Shule
Tunapokea Misaada kwa aina tatu
.
- TUNAPOKEA VIFAA K**A JOLA ZA VITAMBAA VIZITO KWA AJILI YA KUSHONA SKETI NA SURUALI, NA JOLA ZA VITAMBAA VYEUPE KWA AJILI YA KUSHONA MASHATI NA MAJUBA (SHUNGI) NA NUSU KANZU
- COUNTER BOOK, Q. II & III, MIKEBE, BIC, RULLA, PENSEL NK. GODORO 2½ × 6, TRANKA, SOKSI NYEUPE NA NYEUSI,
KWA YEYOTE MWENYE NIA YA KUMSIMAMIA MTOTO YATIMA KWA KUMSOMESHA (Kusimamia gharama zake zote hadi ana maliza kidato cha nne) IWE MMOJA AU WAWILI NA ZAIDI, , TAARIFA ZOTE ZA MTOTO ATAKUWA ANAPATIWA KILA HATUA.
- TUNAPOKEA PESA TASILIMU KWA LENGO LA KUFANIKISHA KUPATIKANA KWA GHARAMA ZA WATOTO HAWA MASIKINI.
SANA SANA KILA ALIYEJAALIWA CHOCHOTE BASI TUWASILIANE ILI TUWAWEZESHE HAWA WATOTO WATIMIZE NDOTO ZAO
KWA MICHANGO NA MAWASILIANO TUPIGIE:
0752249858 - M-PESA
Wabillahi Tawfiq
NYOTA YA FARAJA
Mwangaza kwa waliokata tamaa
13/10/2021
SAIDIA WASIO JIWEZA ILI WAENDE SEKONDARI KIDATO CHA KWANZA.
Siku chache zijazo, tutaanza pilikapilika za Maandalizi ya Watoto wetu kujiunga kidato cha kwanza, Imekuwa ni Kawaida kwa wale ambao hali zao za maisha ni duni kuhangaika huku na kule kutafuta misaada ya watoto wao waweze kwenda shule
NYOTA YA FARAJA kwa kulitambua hilo, tumeanza kukusanya vifaa mapema kwa ajili ya kuwasaida watoto Yatima na wale wasio na uwezo, vifaa vya shule ili na wao waripoti shule kwa wakati k**a wenzao.
: MAJOLA YA VITAMBAA VIZITO VYA RANGI TOFAUTI, NYEUSI, BLUE, DARK BLUE, KIJANI, NYEKUNDU, KIJIVU, RANGI YA UGOLO, DAMU YA MZEE NK
Pia : MADAFTARI, MIKEBE, KALAMU, BIKI, BEGI, VIATU, COUNTER BOOK Q. II pamoja na vifaa vingine muhimu pia pesa Taslimu.
Kwa yeyote atakayejaaliwa kuwa na nafasi ya kuchangia chochote basi wasiliana nasi kwa namba: 0752249858. Whatsapp na Kawaida
01/10/2021
Habari za Ijumaa
Tuendelee kushirikiana kusaidia jamii
Sisi tupo kwa ajili yako
Karibu sana
28/09/2021
Naam Wadau wetu habari za majukumu
Sisi tuko salama tunaendelea na jukumu la kuusaidia Ummah, karibu tushirikiane
12/08/2021
WEMA (SADAKA) UNALIPA, HAUPOTEI
SOMA KISA HIKI HALAFU CHUKUA HATUA.
Bilionea MNigeria Femi Otedola alipoulizwa kwenye interview, ya Simu na Mtangazaji wa Radio, "Sir ni kitu gani unachokumbuka kilichokufanya uwe na furaha maishani?"
Femi alijibu:
"Nimepitia hatua nne za furaha katika maisha yangu na mwishowe nilielewa maana ya furaha ya kweli."
Hatua ya Kwanza ilikuwa ni kutafuta Mali na kulimbikiza. Lakini katika hatua hii sikupata furaha niliyoihitaji.
Nikaingia hatua ya pili ya kujinunulia vitu vya thamani. Lakini niligundua kuwa vitu vyote hivi vinakupa furaha ya muda tu ambayo haidumu.
Nikaingia hatua ya tatu ya kufanya miradi mikubwa. Ni katika hatua hii nilikuwa ninasambaza 95% ya Diesel Nigeria yote na Africa Kwa ujumla. Pia nilikuwa mmiliki mkubwa wa Vessel Africa na Asia. Lakini pia hapa sikupata furaha niliyokuwa nimeifikiria.
Hatua ya nne ilikuwa ni kipindi ambacho Rafiki aliniomba kununua Wheelchairs Kwa ajili ya watoto walemavu. Walikuwa k**a watoto 200 hivi.
Baada ya kuombwa na rafiki yangu nilinunua Wheelchairs 200 mara moja.
Lakini pia aliniomba niambatane naye ili nikawakabidhi watoto zile wheelchairs. Nilijiandaa nikaambatana naye.
Nikawagawia zile wheel chairs Kwa mikono yangu mwenyewe. Niliona furaha ikitawala kwenye nyuso za hawa watoto. Nikawaona wamekaa kwenye wheelchairs, wakizunguka na kufurahia.
Ilikuwa ni k**a wako Picnic wakisherehekea ushindi wa bahati nasibu.
NiIihisi furaha ya kweli ndani yangu. Nilipotaka kuondoka mtoto mmoja alinishika miguu yangu. Nilijaribu kujinasua taratibu lakini alinikazia macho akinitazama usoni.
Niliinama chini nikamuuliza, kuna kitu kingine unahitaji?
Jibu alilolitoa mtoto huyu sio tu kwamba lilinipa furaha bali pia lilinifanya nibadili kabisa mtazamo wangu juu ya maisha. Mtoto huyu alisema:
"Ninakuangalia ili niikumbuke Sura yako, siku nikikukuta mbinguni niweze kukutambua na kukushukuru tena."
Je Wewe mwenzangu, utakumbukwa Kwa lipi utakapoondoka kwenye hiyo Kampuni, Ofisi, Biashara, Kazini au mahali unapoishi?
Je kuna Mtu atatamani kuuona uso wako tena siku za usoni?.
27/07/2021
Assalam alaykum warahmatullah wabarakatuh
NYOTA YA FARAJA
HARAMBEE YA SIKU 10. YA UKUSANYAJI WA NGUO ZA K**E NA ZA KIUME, TAULO ZA K**E, JUZUU KUBWA NA NDOGO, SABUNI ZA KUOGEA, SABUNI ZA UNGA, SABUNI ZA USAFI, DAWA ZA MENO, MISWAKI NA DAWA ZA U.T.I
Leo tarehe 04/08/2021 ni Siku ya Tisa (9) ya Harambee. SHIME tuendee Kuchangia
Tumeanza kupokea vitu tajwa hapo juu kwa ajili ya ndugu zetu katika Imani WAFUNGWA na MAHABUSU
Tunapokea Kanzu, Misuli, Mashati, Suruali, Fulana (zisiwe za picha na Maandishi)
**E
Tunapokea Hijabu, Majuba, Madila, Mitandio, Taulo za K**e (Hitajio kubwa sana)
VITU VINGINE ni pamoja na MISAHAFU ya Matini na Tafsiri, JUZUU kubwa na ndogo, Sabuni za Kuogea, Sabuni za Usafi, Dawa za Meno, Miswaki.
MISAHAFU na JUZUU zifikishwe Kariakoo Dukani kwa Ustadh Saimu Gwao Muulize Muhidini
NGUO na Vitu vingine vifikishwe MASJID HAQQA Buguruni ROZANA Mkabidhi IMAMU HAMISI.
FAHAMU KUWA: "Nguo unayofikiria kuifanya Dekio, basi kwa wenzio ni Mpya"
AU TUPIGIE TUTAFWATA POPOTE ULIPO MZIGO KWA DAR ES SALAAM
KWA MWENYE NIA YA KUTOA CHOCHOTE ALICHO JAALIWA BASI TUMA KATIKA MOJA YA NAMBA HIZI HAPA CHINI
M - pesa - 0752249858 - Sheikh Mchomolo
Tigo Pesa - 0715580807 - Kudura Sama.
Wabillahi Tawfiq
NYOTA YA FARAJA
Mwangaza kwa waliokata tamaa
02/07/2021
Assalam alaykum warahmatullah wabarakatuh
NYOTA YA FARAJA
MCHANGO! MCHANGO!
✍🏻 VIFAA VYA UJENZI WA MSIKITI.
Mtume (s.a.w) amesema:
Mwenye Kujenga Msikiti kwa sababu ya Kumpenda Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamjengea JENGO Kubwa Peponi" (Muslim)
TUNAWASHUKURU MNAO CHANGIA ILI KUPATA VIFAA TUENDELEE KUCHANGIA TUKAMILISHE
🌸MAHITAJI KWA SASA NI K**A IFUATAVYO:
1. BORITI
▶️ Boriti - 2/4. - 50 @ 4,800 Sawa 480,000/=
▶️ Boriti - 2/2. - 100 @ 4,000 Sawa Tsh. 400,000/=
2. BATI
▶️ Bati 35 (G' 30) @ 19,000 Sawa Tsh. 760,000/=
3. MIKEKA
▶️ Mikeka ya Kuswalia 96 @ 15,000. Sawa Tsh. 1,440,000/=
✍🏻 TUPIGIE/TUMA MCHANGO WAKO:
Mpesa 0752249858
Airtel Money 0785949076
Wabillahi Tawfiq
NYOTA YA FARAJA
Mwangaza kwa waliokata tamaa