29/04/2024
TANGAZO
Ubungo Manispaa Page
29/04/2024
TANGAZO
27/04/2024
26/04/2024
HERI YA MIAKA 60 YA MUUNGANO
25/04/2024
Bodi ya Vileo ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam inategemea kutoa leseni za nyongeza ya muda wa kufunga biashara za bar na grosari kutoka saa sita usiku mpaka saa tisa alfajiri lengo ikiwa ni kuongeza mapato ya Halmashauri kupitia chanzo hicho na wateja kufurahia huduma hiyo masaa 24
Maamuzi hayo yametolewa leo Aprili 25, 2024 kwenye kikao cha bodi hiyo kilicholenga kujadili na kupitisha maombi ya leseni za vileo kwa kipindi cha kwanza cha mwezi Aprili hadi septemba 30, 2024 ambapo jumla ya maombi ya leseni 1131 yameridhiwa na bodi hiyo na kusisitiza kuwa utoaji wa elimu uendelee ili wafanyabiashara wengi wapatiwe leseni.
Mwenyekiti wa kikao hicho, Mhe Omary Yusuph Yenga amesema leseni hiyo itakayotozwa shilling 50,000 kwa mwezi, bodi imeamua kuanzisha utaratibu huo baada ya bar na grosari nyingi katika Manispaa hiyo kutofuata sheria ya leseni zao za kawaida zinazowataka kufunga biashara hiyo saa tano usiku kwa siku za kazi na saa sita usiku kwa siku za wikiendi hivyo utaratibu huo utawawezesha kufanya bishara kwa kufuata sheria tofauti na sasa ambapo bar zinakesha bila kibali.
Akifafanua umuhimu wa kuanzisha utaratibu huo, Mhe. Yenga amesema kwasababu biashara nyingi katika jiji hilo zinafanyika masaa 24, utoaji wa leseni za nyongeza ya muda wa kufunga Bar na Grosari ni mhimu ili watu wasivunje sheria lakini pia halmashauri isipoteze mapato.
Kwa mujibu wa takwimu, Manispaa ya Ubungo inajumla ya bar na grosari 800 ambapo kupitia maamuzi hayo halmashauri inatarajia kukusanya zaidi ya milioni 480 kwa mwaka kutoka kwenye chanzo hicho kipya cha leseni kiasi ambacho ni zaidi ya makisio ya bajeti ya shilingi milioni 200 kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 kwa leseni zote za biashara.
Katika kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa, bodi imeielekeza idara ya biashara kutaarifu wamiliki wote kulipia leseni ya kibali cha muda wa nyongeza wa kufunga biashara hizo na atakayebainika kukesha na biashara hiyo bila kibali hicho atatozwa fine ya shilingi 1,000,000.
24/04/2024
MAZINGIRA SAFI HUVUTIA WATEJA, BABA NA MAMA LISHE WASISITIZWA KUZINGATIA
Baba na mama lishe kutoka katika kata na mitaa mbalimbali iliyopo katika Manispaa ya Ubungo wamepatiwa mafunzo kuhusu masuala ya lishe, kilimo mjini pamoja na masuala ya afya katika maeneo ya biashara
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya kilimo, mifugo na uvuvi Manispaa ya Ubungo Archie Mtambo amewataka mama na baba lishe kuendana na wakati kwa kuzingatia mazingira safi ya uandaaji wa chakula wanapokuwa katika biashara zao sambamba na kuzingatia makundi sahihi ya vyakula kwa wateja yenye mlo kamili bila ya kuacha mbogamboga
Mtambo ameendelea kusisitiza na kuwataka kuzingatia afya ya mlaji na usafi wakati wa kuandaa vyakula kwani maradhi ni mengi
"Vionjo katika mapishi ni muhimu lakini ubunifu ni muhimu pia, pika chakula kuendana na usasa weka chakula katika mazingira safi wateja watakuja kwa wingi" amesisitiza Mtambo
Akitoa elimu kuhusu masuala ya lishe, Afisa lishe Manispaa ya Ubungo Beatrice Mossile amewasisitiza kuzingatia ulaji unaofaa kwa kuwapikia wateja vyakula vyenye mchaganyiko wa makundi sahihi yenye mlo kamili
"Vyakula vyenye chumvi na sukari kwa wingi ni hatari, muweke maji ya kunawa yaliyo safi na salama na pia mazingira yawe safi. amesisitiza Mossile
Aidha, Afisa afya Manispaa ya ubungo Goodluck Mselle amewasitiza uzingatiaji wa usafi katika maeneo yao ya biashara na kufuata kanuni za afya ikiwemo kuweka vitunzia taka, sehemu ya kuhifadhia maji na kutokumwaga maji machafu ovyo
Nae, afisa kilimo-lishe Stela Nzelu amewata kuzingatia upishi wa vyakula kwa kuzingatia mbogamboga na matunda kwaajili ya wateja na kuwapa elimu ya uzingatiaji wa mlo uliokamilika
Mmoja wa mama lishe Shakira George ameishukuru Manispaa kwa kuwawezesha kupata mafunzo ambayo yamemnufaisha na kumsaidia na kuahidi kwenda kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora yenye makundi sahihi ya vyakula
Wakiwa katika mafunzo hayo mama na baba lishe wamefundishwa kwa vitendo namna ya kupika vyakula mbalimbali ili kuwaongezea ujuzi zaidi
22/04/2024
UBUNGO YAADHIMISHA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANZANIA
Tukielekea katika maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania tarehe 26/4/2024 Ubungo imefanya kongamano la kuliombea taifa katika ukumbi wa Noble hall uliopo Kimara Leo tarehe 22 April,2024
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na kauli mbiu isemayo, "Miaka 60 ya Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania,Tumeshikamana na Tumeimarika, kwa maendeleo ya Taifa letu.
Akifungua kongamano hilo Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ambaye pia ni Katibu Tawala Wilaya hiyo Hassan Mkwawa amesema kuwa, vijana wanajukumu la kuenzi Muungano kwa kuhakikisha wanafata yote ambavyo wazee wetu waliyafanya
Aliendelea kueleza kuwa,toka waasisi wetu walivyosimamia Muungano huu ambao taifa linaenda kusherekea siku hiyo ifikapo tarehe 26/4/2024 ambayo ni siku muhimu ni jukumu la Kila mtanzania kuulinda na kuuenzi Muungano.
Aidha, akitoa historia fupi toka Muungano ulivyofanyika na mpaka Sasa ambapo taifa linaenzi Muungano huo luteni kanali mstaafu Ali Shamte amesema kuwa, watanzania tunapaswa kujivunia Muungano wetu na kuulinda na tunapaswa kushikana kwa pamoja kudumisha Muungano huu
Wazee waliokuwepo kipindi Cha muungano wanaelewa faida zake na moja nikuleta umoja,mshikamano na pia ulinzi.alisema Shamte
Nae, kanali mstaafu Massanja Sunday ambaye ni msemaji Taasisi ya kizalendo Tanzania (TPO) amesema kuwa, Muungano unapaswa kuendelea kulindwa, tunapaswa kujivunia Muungano huu ambao sasaivi watu wote tunaweza kukutana na kukaa pamoja na kila mmoja akawa na amani
Wazanzibar wanakaa bara na sisi tunaenda zanzibar na kila mmoja ana amani katika eneo la mwenzie, amani imetawala baina yetu
"Asitokee mtu akatamani kuuvunja Muungano wetu" amesisitiza