PbpaTanzania

PbpaTanzania

Share

Ukurasa Rasmi wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA)

26/03/2026
Photos from PbpaTanzania's post 29/01/2026

PBPA YAFUNGUA ZABUNI ZA UAGIZAJI MAFUTA KWA PAMOJA

Kamati ya Zabuni ya Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (BPS) chini ya Mwenyekiti wake, Bw. Ali Saeed, leo imefungua zabuni ya ununuzi wa mafuta kwa ajili ya matumizi ya mwezi Machi, 2026.

Katika zabuni hiyo, jumla ya 6 zikifanikiwa kuibuka washindi baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa taratibu na sheria zinazosimamia ununuzi wa mafuta kwa pamoja.

Ufunguzi wa zabuni hiyo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wazabuni, maafisa wa serikali pamoja na wawakilishi wa taasisi husika.

Photos from PbpaTanzania's post 29/01/2026
Photos from PbpaTanzania's post 16/12/2025

PBPA YAFUNGUA ZABUNI ZA UAGIZAJI MAFUTA KWA MWEZI FEBRUARI 2026 JIJINI DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Wetu- Dar es Salaam

Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) leo, Desemba 16, 2025, imetekeleza zoezi la ufunguzi wa zabuni za uagizaji mafuta kwa ajili ya mahitaji ya mwezi Februari, 2026 ambapo kampuni 8 kati ya 11 zimeshinda zabuni hizo katika vipengele tofauti.

Zoezi hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa PBPA jijini Dar es Salaam, likihusisha wazabuni wa kimataifa na wa ndani, pamoja na wadau wa sekta ya nishati.

Ufunguzi huo ni sehemu ya utaratibu wa kisheria na kikanuni wa kuhakikisha nchi inakuwa na nishati ya Mafuta ya kutosha na ya uhakika, huku ikizingatia misingi ya uwazi, ushindani wa haki, na gharama nafuu kwa mlaji wa mwisho.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa PBPA, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Petroli, Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Mhandisi Bruno Tarimo amewapongeza washindi wa zabuni hizo.

"Nawapongeza wazabuni wote mlioshinda. Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, ninasisitiza kwa wasambazaji wote walioshinda zabuni zao kukamilisha taratibu na masharti ya mikataba ili kufanikisha uingizaji wa mafuta kwa mfumo wa uagizaji wa pamoja (BPS) kwa mwezi Februari 2026 unafanyika kwa ufanisi." amesema.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya zabuni ya Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (BPS), Bw. Ali Saeed aliongoza zoezi la ufunguaji wa Zabuni na kuwatangaza washindi kisha kuwapongeza kwa ushindi huo.

Zoezi hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Wazabuni waliokidhi vigezo vya awali, Wawakilishi wa kampuni za uuzaji wa mafuta (OMCs) na Wadau wengine muhimu.

Photos from PbpaTanzania's post 28/10/2025

Kamati ya Zabuni ya Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (BPS) chini ya Mwenyekiti Bw. Ali Saeed leo imefungua Zabuni ya Ununuzi wa Mafuta kwa matumizi ya mwezi Desemba, 2025. Ufunguzi huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi ya Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wazabuni mbalimbali.

Photos from PbpaTanzania's post 21/10/2025

PBPA yakutana na Wadau kujadili mpangilio wa meli na usafirishaji wa mizigo ya mafuta kwa mwezi Desemba, 2025

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Tanzania Ports Authority (TPA) Tower, 11th Floor, Plot Number 1/2, Sokoine Drive P O BOX 2634
Dar Es Salaam