18/04/2026
K**a ilivyo ada. Kila mwaka ACT Wazalendo lazima tuchambue Ripoti ya CAG na kuweka wazi madudu na ufisadi unaofanywa serikalini.
Kesho saa 5:00 Asubuhi katika Jengo la Maalim Seif kutafanyika uchambuzi wa Ripoti ya CAG.
Waandishi wote mnakaribishwa
18/04/2026
Kesho Aprili 19, 2026 Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu atashiriki kwenye uwasilishaji wa uchambuzi wa Ripoti ya CAG kwa mwaka fedha 2024/2025.
Uwasilishaji utafanyika Makao Makuu ya ACT na utarushwa mubashara na vyombo vya habari.
18/04/2026
Kesho Aprili 19, 2026 Makamu Mwenyekiti Bara, Ndugu Isihaka Mchinjita atashiriki kwenye uwasilishaji wa uchambuzi wa Ripoti ya CAG kwa mwaka fedha 2024/2025.
Uwasilishaji utafanyika Makao Makuu ya ACT Wazalendo na utarushwa mubashara na vyombo vya habari.
18/04/2026
Kesho Aprili 19, 2026 Chama cha ACT Wazalendo kitafanya Uchambuzi wa Ripoti ya CAG.
KC Dorothy Semu ataongoza uwasilishaji wa uchambuzi wa ripoti hiyo kwa umma kupitia vyombo vya habari.
17/04/2026
Aprili 19, 2026 Chama cha ACT Wazalendo kitafanya Uchambuzi wa Ripoti ya CAG.
KC Dorothy Semu Makamu Mwenyekiti Bara, Isihaka Mchinjita na Katibu Mkuu Ado Shaibu watawasilisha uchambuzi huo kwa umma kupitia vyombo vya habari.
05/01/2026
UELEKEO WA CHAMA CHA ACT WAZALENDO
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Ndugu, Dorothy Semu leo 05 Januari, 2026 ameanza ziara yake katika majimbo ya mikoa ya kusini ya kukutana na viongozi juu ya kupata maoni na kufafanua hatua zilizochukulia pamoja na msimamo wa chama baada ya uchaguzi mkuu 2025 kumalizika. Ziara hiyo imeanza katika majimbo ya Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini katika Mkoa wa Kichama Selous.
Kwenye kikao hicho kiongozi wa chama amepokea maoni ya viongozi wa chama waliohudhuria kikao hicho kwamba uchaguzi haukuwa wa huru, haki na kuaminika. Mbali na maoni hayo wapo wameoshauri chama kiende kwenye maridhiano kuwaeleza uso Kwa macho ubadhirifu uliofanyika na wapo ambao wameshauri mapambano ya kusaka katiba mpya hayapaswi kuwa na mbadala.
Baada ya kupokea maoni ya viongozi kiongozi wa chama amehutubia na kutoa ufafanuzi juu ya msimamo wa chama baada ya uchaguzi mkuu ambapo amesema;
Kwanza, tulisema tutashiriki huku tukipambana na tutapambana huku tukishiriki katika hili ni wajibu tuliubeba viongozi tukitambua kuwa tunaenda kuyakabili mapambano katika uwanja usiokuwa huru na haki. Hatutakata tamaa tutaendelea kupambana bila kurudi nyuma kwa kusimama na Wananchi, kusimama na haki mpaka hapo mabadiliko ya kweli na kuaminika yatakapopatikana.
Mbili, Bado tunasisitiza juu ya serikali kusitisha mara Moja vitisho na kamatakamata watu na kuwaweka ndani viongozi wa upinzani bila kufuata Sheria.
Tatu, Sauti za watu wanaodai haki na manadiliko zinapaswa kusikilizwa na kuleta majawabu ya kupatikana Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
Nne, wito wetu ni serikali kuwaachia huru viongozi wote wa kisiasa na wananchi wote waliobambikiziwa kesi za uchaguzi
Tano, iundwe Tume huru ya Uchuguzi njee ya serikali iweze kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2025. Tume hii inapaswa kuwa yenye uwezo wa kuhoji bila ya maelekezo ili iweze kutupa taarifa zenye ukweli juu ya kilichojili Oktoba 29. Tume hiyo ya Jaji Chande tuliikataa na sasa tunaikataa na hatutaipa ushirikiano kwasababu imekosa uhalali.
Sita, tume ya maridhiano iliyo huru na sio ya Serikali. Tume hiyo iundwe njee ya Serikali. Ituite pamoja wadau wote tuweze kutengeneze mazingira bora ya kuleta mabadiliko yenye kuaminika.
Saba, tunahitaji Katiba Mpya itakayokuja na Tume huru na kutoa uhuru wa mihimili itayotoa haki sawa kwa wote.
Nane, Uporaji wa haki za wananchi kuchagua viongozi wao tulisema tutaipeleka INEC na Serikali Mahakamani na sasa tumefungua kesi 25 kwa upande wa Zanzibar na 30 kwa upande wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hitimisho
Kiongozi amehitimisha kwa kusema Tanzania haitajengwa kwa hofu na risasi bali kwa uadirifu na uongozi unaoleta majawabu kwa watu wake. CCM wamebadilisha uchaguzi kuwa uwanja wa vita badala ya kuwa uwanja wa kupata viongozi bora.
01/07/2025
TAARIFA
Naibu Waziri Kivuli wa Mifugo wa , Ndugu Thomas Nkola ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa siku zisizopungua tatu kwa tuhuma za kumkashifu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.
30/06/2025
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya , Ndugu Said Salim Njuki (kulia) amechukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Babati Mjini, Mkoa wa Manyara. Fomu hiyo amekabidhiwa leo Juni 30, 2025 na Kaimu Katibu wa Jimbo hilo ndugu John Faustine Gilagwen.
Oktoba
30/06/2025
TAARIFA KWA UMMA
"Tunalaani kukamatwa na kushikiliwa kwa Naibu Waziri Kivuli wa Mifugo wa , Ndugu Thomas Nkola."
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani
Dahlia Majid
30/06/2025
Salamu za pole za ACT Wazalendo kwa ajali ya mabasi iliyotokea Same Kilimanjaro.
27/06/2025
"Chama cha ACT Wazalendo tunawatakia Waislamu wote wa Tanzania na Duniani kote, Heri ya mwaka mpya wa Kiislamu 1447 Hijria."
Kiongozi wa
Dorothy Semu