Bakitatz

Call Directions Website Contact the organization

Bakitatz Baraza la Kiswahili la Taifa ni taasisi ya Umma ambayo inasimamia shughuli za ukuzaji wa Kiswahili

BAKITA YAPATA ELIMU KUHUSU MATUMIZI YA NISHATI SAFI NA SALAMAWatumishi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) wamepata...
30/09/2026

BAKITA YAPATA ELIMU KUHUSU MATUMIZI YA NISHATI SAFI NA SALAMA

Watumishi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) wamepata elimu kuhusu umuhimu na faida za matumizi ya nishati safi na salama, hususani matumizi ya umeme, ikiwa ni pamoja na mchango wake katika kupunguza moshi na uchafuzi wa mazingira.

Akizungumza na watumishi wa BAKITA, Bw. Juma Msuya, Afisa Huduma kwa Wateja kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Kinondoni, ameeleza kuwa matumizi ya umeme kwa ajili ya kupikia ni nafuu ikilinganishwa na baadhi ya aina nyingine za nishati, huku yakichangia kuboresha mazingira ya kupikia na kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Aidha, Bw. Msuya amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama kutokana na faida zake katika kulinda mazingira, kuboresha afya na kuchangia ustawi wa jamii.
Elimu hiyo imetolewa leo tarehe 30 Septemba 2026, katika ukumbi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Makumbusho, Dar es Salaam.

27/09/2026

𝐏𝐚𝐩𝐚 𝐧𝐚 𝐊𝐒𝐬𝐰𝐚𝐑𝐒π₯𝐒…

Papa Leo XIV alipokaribishwa kwa Kiswahili na mtumishi wa Ubalozi wa Tanzania Ufaransa akajibu β€œAhsante”

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limeendesha mafunzo ya Waandishi Waendesha Ofisi (WWO) yaliyoanza tarehe 21 Septem...
23/09/2026

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limeendesha mafunzo ya Waandishi Waendesha Ofisi (WWO) yaliyoanza tarehe 21 Septemba 2026 katika ukumbi wa hoteli ya New Kiboko iliyopo jijini Tanga , mafunzo hayo yanalenga kuwaongezea washiriki ujuzi wa matumizi fasaha na sanifu ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano na utoaji wa huduma kwa wananchi.


Akifungua rasmi mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa BAKITA, Bi. Consolata P. Mushi, amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuwajengea Waandishi Waendesha Ofisi uwezo wa kutumia Kiswahili kwa usahihi na kuimarisha ujuzi wa Lugha ya Alama ili waweze kuwasiliana na kutoa huduma kwa ufanisi zaidi kwa wananchi wenye changamoto za kusikia na kuzungumza Hatua hii inalenga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma kwa usawa na bila vikwazo vya mawasiliano. Vilevile maarifa ya matumizi akiliunde katika Kiswahili yatawasaidia kuharakisha na kurahisisha majukumu yao ya kazi za kila siku husasan uhariri na uandishi wa vyaraka mbalimbali ili kuongoza ufanisi na tija katika taasisi.
Mafunzo hayo yanayofanyika kuanzia tarehe 21 hadi 25 Septemba 2026 yanalenga kukuza huduma jumuishi katika taasisi, kwa kuwawezesha Waandishi Waendesha Ofisi kuwa na uelewa na stadi za msingi za Lugha kwa kuzingatia maadili katika mazingira ya kazi. Hatua hii inalenga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma kwa usawa na bila vikwazo vya mawasiliano na kuepusha migogoro.

Aidha, Bi. Mushi amewahimiza Waandishi Waendesha Ofisi ambao bado hawajapata mafunzo hayo kujisajili na kutumia fursa ya mafunzo yatakayoendelea kutolewa katika kanda mbalimbali nchini, ili kuongeza ujuzi, kuimarisha weledi na kuchangia katika kuboresha mawasiliano na utoaji wa huduma katika taasisi zao.

23/09/2026
Je, wajua neno hili la Kiingereza lina Kiswahili chake sanifu?
21/09/2026

Je, wajua neno hili la Kiingereza lina Kiswahili chake sanifu?

Address

S. L. P 4766, Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
14107

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Telephone

+255222762243

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bakitatz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Bakitatz:

Shortcuts

Share