Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala-WRRB

Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala-WRRB

Share

WRRB ni Bodi ya Usimamiz wa Stakabadhi za Ghala ambao hutoa ufikiaji wa masoko rasmi ya mikopo na bidhaa.

05/05/2026

Tunajivunia kuwa na Union of Warehouse Operators (UWO) k**a mdhamini, wakichangia katika kuimarisha mifumo ya uhifadhi na kukuza uchumi endelevu.

Jiunge nasi katika maadhimisho ya miaka 20 ya WRRB!
📅 17–19 Mei 2026
📍 Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), Dodoma

Kaulimbiu: Mfumo Imara, Uchumi Endelevu

05/05/2026

Tunafurahia kushirikiana na – Smart Farming k**a exhibitor, wakileta suluhisho bunifu katika sekta ya kilimo.
Kaulimbiu: Mfumo Imara, Uchumi Endelevu

Karibu ujionee ubunifu kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya WRRB!
📅 17–19 Mei 2026
📍 Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), Dodoma

Photos from Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala-WRRB's post 05/05/2026

Leo, Mei 4, 2026, Mhe. Mwanamvua Mlindoko, Mkuu wa Mkoa wa Katavi , amezindua msimu mpya wa mauzo ya zao la ufuta na mazao mengine kupitia mfumo wa stakabadhi za ghala kwa mwaka 2026/2027.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Mlindoko amewataka wadau kuhakikisha malipo ya wakulima yanafanyika kwa wakati na kuzingatia vipimo sahihi ili kulinda maslahi yao na kuimarisha uaminifu wa mfumo.

Aidha, Bw. Asangye Bangu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), amesema kwa kushirikiana na taasisi nyingine wataendelea kuboresha mfumo huo na kutafuta wanunuzi wengi zaidi ili kuongeza ushindani na hatimaye wakulima wapate bei nzuri.

Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali, Pamoja na Wakuu wa Taasisi Wakiwemo Afisa Mtendaji Mkuu Soko la Bidhaa Tanzania (TMX)Bw.CPA Godfrey Malekano Pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko(COPRA) Bi.Irene Mlola ambao wamekubaliana kusimamia ipasavyo mazao yanayoingizwa kwenye mfumo, kuzuia utoroshwaji, na kuhakikisha wakulima wanalipwa kwa wakati kulingana na bei ya mnada

.hmwinyi

Photos from Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala-WRRB's post 01/05/2026

Leo,Mei 1,2026 watumishi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) wameungana na watumishi wengine kusherehekea Siku ya Wafanyakazi Duniani, katika maadhimisho yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Kitaifa, maadhimisho hayo yamefanyika mkoani Njombe, yakiwakutanisha watumishi kutoka sekta mbalimbali nchini kuadhimisha mchango wao katika kuleta maendeleo ya taifa
Maadhimisho hayo yamebeba Kaulimbiu isemayo “kazi zenye Staha ni Nguzo Imara Kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelesaji wa Dira ya Taifa 2050”

01/05/2026

HERI YA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI MEI MOSI


.hmwinyi

01/05/2026

MFANYAKAZI HODARI


.hmwinyi

Photos from Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala-WRRB's post 29/04/2026

TAARIFA KWA UMMA

Photos from Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala-WRRB's post 29/04/2026

TAARIFA KWA UMMA


.hmwinyi

Photos from Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala-WRRB's post 28/04/2026

*WRRB na Mwananchi Communications Limited Waweka Mikakati ya Kuimarisha Elimu kwa Umma Kuhusu Mfumo wa Stakabadhi za Ghala*

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Bw. Asangye Bangu, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited, Bi. Rosalynn Mworia, katika makao makuu ya WRRB jijini Dodoma, kwa lengo la kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika kuendelea kutoa elimu kwa wadau kuhusu matumizi sahihi ya mfumo wa stakabadhi za ghala.

Katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited aliambatana na Bw. Edson Sostenes kutoka Idara ya Masoko, pamoja na Aretes Mrosso na Bi. Halima Twalbu, ambao ni maafisa masoko na matangazo wa kampuni hiyo mkoani Dodoma.

Mazungumzo hayo yamelenga kuongeza uelewa kwa umma na wadau mbalimbali kuhusu umuhimu na manufaa ya mfumo huo katika kukuza biashara na uchumi. Aidha, pande zote mbili zimejadili mikakati ya kutangaza mafanikio yaliyotokana na matumizi ya mfumo wa stakabadhi za ghala, ili kuhamasisha ushiriki mpana zaidi wa wadau nchini.

.hmwinyi

Photos from Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala-WRRB's post 27/04/2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw Asangye Bangu ,leo Aprili 27, 2026 amekutana na kufanya kikao na Bw Anton Samsonov kutoka Chemba ya Biashara na Viwanda ya Bulgaria pamoja na Bw Petar Klisarov kutoka kampuni ya Rodina-Haskovo JSC, inayojihusisha na usindikaji wa vyakula, udhibiti wa ghala na usafishaji wa maji kwa lengo la kujadili maandalizi na ushiriki wa maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala yanayotarajiwa kufanyika tarehe 17-19 Mei 2026.

Aidha kikao hicho kimejadili mashirikiano ya muda mrefu baina ya taasisi za Serikali ya Tanzania na nchi hiyo katika sekta ya Viwanda pamoja na wafanyabiashara wa ndani kwa lengo la kuimarisha uwekezaji, teknolojia na maendeleo ya viwanda na Biashara.

Photos from Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala-WRRB's post 27/04/2026
26/04/2026

Heri ya Sikukuu ya Muungano Tanganyika na Zanzibar


.hmwinyi

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Dar Es Salaam
P.OBOX38093

Opening Hours

Monday 08:00 - 15:30
Tuesday 08:00 - 15:30
Wednesday 08:00 - 15:30
Thursday 08:00 - 15:30
Friday 08:00 - 15:30