12/04/2026
KATIBU WA HAMASA NA CHIPUKIZI MKOA WA DAR ES SALAAM ATEMBELEA VIJANA WA HAMASA TEMEKE
πTemeke,Dar es salaam
π 09-04-2023
Ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa uhuru unaotarajiwa kuwasili Dar es Salaam mnamo tarehe 13-04-2026 katibu wa hamasa na chipukizi mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Khassim Ngonyani amewatembelea vijana wa hamasa wa wilaya ya temeke na kushiriki nao mazoezi.
Ziara hiyo imelenga kutazama maandalizi ya hamasa ya Mwenge pamoja na changamoto zinazowakabili vijana wa hamasa.Ambapo katika ziara hiyo aliambatana na mjumbe wa baraza la UVCCM mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Elizabeth Mmonda sambamba na wajumbe wa baraza la UVCCM wa wilaya ya Temeke.
Alipukuwa akizungumza na vijana hao Ndg. Khassim Ngonyani alisema " Mwenyekiti wetu wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Nasra Mohamed amenituma niwape salaam zake za upendo wake juu yenu na kwamba amewasisitiza kutanguliza uzalendo,nidhamu na kutanguliza maslahi ya taifa lenu mbele kabla ya chochote".
07/04/2026
UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam inawataarifu wanachama na vijana wote kuwa Katibu wa Hamasa wa Mkoa, Ndugu Khassim Hassan Ngonyani , atafanya ziara maalum ya kutembelea vijana wa Hamasa katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Dar es Salaam.
Ziara hii ni sehemu ya kuendelea kuimarisha ushiriki wa vijana, mshikamano wa kichama na moyo wa uzalendo katika kulitumikia taifa.π°
30/03/2026
Teknolojia mkononi, Chama moyoni.
Tunahakikisha sauti ya vijana na mwangaza wa CCM unafika kila kona ya nchi. Hii ndio digitali ya ushindi! π°π
*
29/03/2026
KATIBU MKUU UVCCM, MWINYI KUFUNGA KAMBI YA UONGOZI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC) atakuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kambi maalum ya uongozi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni tarehe 29 Machi 2026 kuanzia saa 3:00 asubuhi.
04/03/2026
UVCCM MKOA WA DAR ES SALAAM
SAMIA NI SULUHU
Bilioni 200 zipo Zinapatikana
31/01/2026
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Hussein Egobano atashiriko katika Kongamano hili.
31/01/2026
Mgeni Rasmi ni Ndugu .ussi Mjumbe wa Halmashaur kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Jimbo la Malindi atakuwepo katika Kongamano hili.
31/01/2026
Mwenyekiti wa UVCCM MKOA WA Dar es Salaam atashiriko kwenye Kongamano la Kuadhimisha Miaka 49 ya CCM Wilaya ya Ilala. π°
27/01/2026
Heri ya Siku ya Kuzaliwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
egobano
13/01/2026
KATIBU MKUU CCM AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOA DAR ES SALAAM.
Ilala,Dar es Salaam.
π
13 Jan 2026
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Ndg. Balozi Dkt. Asha Rose Migiro leo amehitimisha ziara yake katika mkoa wa Dar es salaam kwa mkutano mkubwa ndani ya wilaya ya Ilala.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo umehudhuriwa na mamia ya viongozi wa CCM wakiwemo mabalozi na vipngozi wa matawi.Ziara hiyo imelenga kuhamasisha na kuwajengea uwezo mabalozi wa mashina katika kufanya kazi zao za kila siku sambamba na kuunga mkono jitihada za mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi taifa Ndg. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza ahazi zilizoahidiwa kwa wananchi kipindi cha Kampeni.
Ziara hiyo ilianza rasmi tarehe 07-01-2026 wilaya ya Temeke na Kigamboni ambapo walikutana ukumbi wa Sabasaba ikifuatiwa na wilaya ya Ubungo na Kinondoni siku ya tarehe 09-01-2026 na kutamatika leo kwa wilaya ya Ilala yenye kata 36 na majimbo manne ya 4 uchaguzi.