APRM Tanzania

Directions Website Contact the organization

APRM Tanzania African Peer Review Mechanism Tanzania is a specialized agency of the African Union.

APRM Tanzania na UONGOZI Institute kujadili maeneo ya ushirikianoAPRM Tanzania na UONGOZI Institute wamefanya kikao kazi...
21/08/2026

APRM Tanzania na UONGOZI Institute kujadili maeneo ya ushirikiano
APRM Tanzania na UONGOZI Institute wamefanya kikao kazi kwa lengo la kujadili na kubainisha maeneo ya ushirikiano kati ya taasisi hizo, hususan katika kuimarisha uongozi na utawala bora.
Kikao hicho pia kilijikita katika namna ya kutumia utaalamu na uzoefu wa taasisi hizo katika kujenga uwezo, kuimarisha utendaji wa viongozi na taasisi, pamoja na kuchochea mijadala ya kisera yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.
Ushirikiano huo unatarajiwa kufungua fursa zaidi za mafunzo, mijadala ya sera na kubadilishana maarifa na uzoefu, kwa lengo la kuongeza thamani na kuleta matokeo chanya katika uongozi na utawala nchini.

Mheshimiwa Prosper Bazombanza, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Burundi, amefungua Jukwaa la Vijana wa Afrika, “African Yout...
11/08/2026

Mheshimiwa Prosper Bazombanza, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Burundi, amefungua Jukwaa la Vijana wa Afrika, “African Youth Charter @ 20” lenye kaulimbiu “From Promise to Prosperity”
Akikumbusha kwamba vijana wanaunda karibu 70% ya idadi ya watu barani Afrika, amesisitiza kuwa kipaumbele cha muhimu ni kutekeleza wajibu wao na kuchukua hatua madhubuti ya kufikia mahitaji na matarajio yao kuwa hatua zinazotekelezwa.

11/08/2026

APRM ni zaidi ya Taasisi yenye dhamira ya kuhamasisha Utawala Bora kwa manufaa ya kila mwananchi Barani Afrika.
Tufuatilie, ujifunze namna Utawala Bora huleta Maendeleo Endelevu

Je, wajua nini kuhusu APRM? Tufuatilie ili kupata habari na kujifunza zaidi
03/08/2026

Je, wajua nini kuhusu APRM? Tufuatilie ili kupata habari na kujifunza zaidi

APRM Tanzania imempongeza na kumshukuru Mhe. Badria Masoud, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, kufuatia uteuzi w...
19/07/2026

APRM Tanzania imempongeza na kumshukuru Mhe. Badria Masoud, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, kufuatia uteuzi wake kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Zanzibar.

Katika kipindi chake cha utumishi , Mhe. Badria alitoa mchango mkubwa katika kuimarisha mawasiliano ya taasisi na kusaidia utekelezaji wa majukumu yake kwa weledi.

Tunampongeza kwa kuaminiwa kulitumikia Taifa katika nafasi yake mpya na tunamtakia mafanikio, hekima na utumishi wenye tija katika majukumu yake mapya.

15/07/2026

Maridhiano ni uwekezaji katika utawala bora, amani na mshik**ano wa kimataifa. APRM Tanzania inaamini kuwa mazungumzo ya...
10/07/2026

Maridhiano ni uwekezaji katika utawala bora, amani na mshik**ano wa kimataifa. APRM Tanzania inaamini kuwa mazungumzo ya kujenga maridhiano, ushirikishwaji wa wadau na utekelezaji wa makubaliano ni miongoni mwa misingi muhimu ya utawala bora, amani na maendeleo endelevu. Maridhiano k**a haya ni msingi wa kujenga Tanzania imara, uchumi imara na mustakabali wenye matumaini zaidi kwa vizazi vijavyo.

Pichani ni matukio ya utiaji saini wa ajenda zilizokubaliwa na pande zote mbili kwa ajili ya kufanyiwa kazi kufuatia Tamko la Pamoja la Muafaka wa Kisiasa Zanzibar kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo.

Heri ya Siku ya Sabasaba
07/07/2026

Heri ya Siku ya Sabasaba

APRM Tanzania yashirikiana na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana na Wadau kufanikisha Vijana Uchumi Challenge 2026Taasi...
06/07/2026

APRM Tanzania yashirikiana na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana na Wadau kufanikisha Vijana Uchumi Challenge 2026
Taasisi ya African Peer Review Mechanism (APRM) Tanzania imeshirikiana na Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, National Social Security Fund (NSSF), UTT Asset Management and Investor Services (UTT AMIS), Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), WCF, Save the Children Tanzania, African Leadership Initiatives for Impact, CRDB Bank Foundation, NMB Bank na iMbeju kufanikisha Vijana Uchumi Challenge 2026 kupitia udhamini na ushiriki katika mchakato mzima wa mashindano kuanzia hatua za awali hadi fainali. Mashindano hayo yalilenga kuibua na kukuza bunifu za vijana zenye uwezo wa kutoa suluhisho kwa changamoto za maendeleo, kuchochea ubunifu na kuimarisha ukuaji wa uchumi nchini.
Vijana Uchumi Challenge imeendelea kujidhihirisha k**a shindano linalowapa vijana nafasi ya kuwasilisha mawazo bunifu yanayoweza kutoa suluhisho kwa changamoto za maendeleo katika sekta mbalimbali za uchumi. Mashindano hayo yalivutia maelfu ya vijana kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ambapo zaidi ya waombaji 7,800 waliwasilisha bunifu zao, huku washiriki 100 bora wakichaguliwa kuendelea katika hatua za juu za mashindano. Hatimaye, katika fainali za mashindano hayo, Geofrey Samuel Sanga aliibuka mshindi wa kwanza.
Kwa kushiriki katika ufadhili wa shindano hilo, APRM Tanzania imeonesha kwa vitendo umuhimu wa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kujenga mazingira yanayowawezesha vijana kutumia maarifa, ubunifu na teknolojia k**a nyenzo za maendeleo. Ushiriki huo ulihusisha mchakato mzima wa mashindano pamoja na kutoa udhamini wa kufanikisha utekelezaji wa programu hiyo.
‘Tunaamini vijana si wanufaika wa maendeleo pekee, bali ni washiriki wakuu wa kuyabuni na kuyaendesha. Ndiyo maana APRM Tanzania inaendelea kuunga mkono majukwaa yanayowawezesha vijana kuonesha uwezo wao na kutoa suluhisho kwa changamoto za maendeleo.’ Katibu Mtendaji - APRM Tanzania
Akizungumza wakati wa kufunga rasmi Vijana Uchumi Challenge 2026, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliwataka vijana kuendelea kutumia ubunifu, maarifa na teknolojia kutatua changamoto za maendeleo na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa. Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayowasaidia vijana kuendeleza bunifu zao, kuzigeuza kuwa biashara zenye tija na kuongeza fursa za ajira nchini. Aidha, aliwataka vijana kuthubutu kutumia fursa zilizopo na kuendelea kubuni suluhisho zitakazoongeza thamani katika uchumi wa Tanzania.
Katika fainali hizo, Geofrey Samuel Sanga aliibuka mshindi wa kwanza, Jacob Fabian Lugwisha akashika nafasi ya pili, huku Robert Malonga akimaliza katika nafasi ya tatu. Mbali na kutambuliwa kwa ubunifu wao, washindi hao walitunukiwa zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuhamasisha vijana kuendelea kubuni suluhisho zenye mchango katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

   On  , APRM salutes the vibrancy and resilience of young Africans who are championing good governance, democracy, and ...
12/08/2024


On , APRM salutes the vibrancy and resilience of young Africans who are championing good governance, democracy, and sustainable development. We recognize the critical role youth play in shaping the continent's future and call for their active participation in decision-making processes.

Let's harness the energy and creativity of young people to drive positive change and build a more inclusive and prosperous Africa.




n









Address

Shaaban Robert Street
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when APRM Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to APRM Tanzania:

Shortcuts

Share