12/05/2026
πππππ πππππππππ ππππππ ππ ππππππ ππ ππ
ππ ππ ππππππππ ππππππππ 1.8 πππ πππππ 2026/27
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Wizara ya Afya ya Shilingi trilioni 1.8 kwa mwaka wa fedha 2026/27, ikiwa ni hatua muhimu katika kuendelea kuimarisha huduma za afya nchini.
Bajeti hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Afya, ππ‘π. ππ¨π‘ππ¦π¦ππ πππ‘ππ§π ππ«π°π (ππ), inalenga kuongeza ubora wa huduma za afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kuendeleza miundombinu ya hospitali pamoja na kusogeza huduma bora kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.
Kati ya fedha zilizopitishwa, Shilingi trilioni 1.148 sawa na asilimia 64 zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo huku Shilingi bilioni 652.236 zikitumika kwa matumizi ya kawaida ya wizara hiyo.
Aidha, kupitia bajeti hiyo serikali itaendelea kusimamia maboresho makubwa katika sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa hospitali, vituo vya afya, upatikanaji wa wataalamu pamoja na kuimarisha huduma za kibingwa na ubingwa bobezi nchini.
12/05/2026
za watanzania ziko mikono salama
11/05/2026
Vipaumbele vya Wizara ya Afya 2026/2027
11/05/2026
KAMATI YA BUNGE YAISHAURI SERIKALI KUTOA BILIONI 300 KUIWEZESHA MSD
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imeishauri Serikali kutenga zaidi ya shilingi bilioni 300 kwa ajili ya kuiwezesha Bohari ya Dawa (MSD), hatua inayolenga kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba unaendelea kuwa wa uhakika kwa hospitali na vituo vya afya nchini.
Ushauri huo umetolewa bungeni na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Zeyana Abdallah Mei 11, 2026 jijini Dodoma wakati akiwasilisha maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2026/27.
Dkt. Zeyana ameitaka Serikali kuongeza uwekezaji katika mifumo ya kinga pamoja na kuzijengea uwezo taasisi zake ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za afya, hatua inayokwenda sambamba na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Ilani ya CCM 2025β2030 na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030.
Katika eneo la rasilimali watu, Kamati imeishauri Serikali kuendelea kutoa vibali vya ajira kwa kada zenye upungufu mkubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya, huku ikisisitiza ajira hizo zitolewe kwa kuzingatia mahitaji halisi ya taasisi pamoja na kuwapa kipaumbele wataalam wanaojitolea katika hospitali mbalimbali nchini.
βTunaitaka Serikali kuongeza ufadhili wa masomo kwa wataalam wa afya ili kupata mafunzo ya ubingwa na ubingwa bobezi ndani na nje ya nchi, hatua itakayo ongeza wataalam wenye ujuzi wa hali ya juu katika sekta ya afyaβ amesema Dkt. Zeyana.
Pamoja na ushauri huo, Kamati imeipongeza Serikali kwa maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika kwenye sekta ya afya ikiwemo kuanza kwa utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote, kuimarisha Hospitali za Rufaa za Mikoa na Kanda pamoja na mpango wa ujenzi wa Hospitali mpya ya Taifa ya Muhimbili.
Makamu mwenyekiti huyo ameonesha kuridhishwa na hatua ya Serikali kuendelea kununua vifaa tiba vya kisasa k**a mashine za PET CT Scan, MRI, Angio Suite na Mammography, hatua inayochangia kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi