06/03/2026
Mafunzo ya Mfumo wa NIIMS mkoani Morogoro
Mafunzo ya Mfumo wa Taarifa za Viwanda Tanzania (NIIMS) yanayotolewa na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO) yaliyofanyika tarehe 24 Februari 2026 kwa maafisa Biashara na TEHAMA wa mkoa wa Morogoro.
Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo maafisa Tehama na Biashara wa Halmashauri za Mkoa huo juu ya Mfumo ambao utasaidia kuhifadhi taarifa sahihi za viwanda vyote ndani ya Mkoa na hali yake.
26/04/2024
TIRDO inawatakia Watanzania wote maadhimisho mema ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
31/03/2024
Heri ya Sikukuu ya Pasaka.
18/03/2024
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Utawala katika Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) ambalo linatarajiwa kumalizika June 30,2024.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb) amesema serikali imeiongezea uwezo wa kimiundombinu upande wa vifaa na sasa jengo Shirika la TIRDO ili kuweza kutoa huduma bora kwa viwanda na kuendeleza atamizi mbalimbali shirikani.
Aidha Kamati hiyo imeiomba serikali kupitia Wizara kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa kutenga na kutoa bajeti iliyobakia.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)amesema kwa hatua zilizobaki kukamilisha ujenzi wa jengo hilo, TIRDO ilitengewa bajeti ya shilingi bilioni 3.4 ambapo mpaka sasa wameshapokea shilingi bilioni 1.54 kwaajili ya ukamilishani wa jengo hilo.
Mhe. Waziri ameishukuru Kamati hiyo kwa kuweza kuisukuma serikali na hatimae kupatikana kwa fedha hizo na ujenzi ukiendelea kutoka asilimia 50 iliyokuwepo mwaka jana na kufikia asilimia 72 kwasasa.
13/12/2023
Darasa la matengenezo ya mashine za kutoa nakala (photocopy machine) likiendelea TIRDO. Usikose fursa hii itakapotangazwa tena. Karibuni wote.
09/12/2023
TIRDO inawatakia maadhimisho mema ya Miaka 62 ya Uhuru.