22/05/2026
Wizara ya Viwanda na Biashara Yaomba Bilioni 137.8 Kuimarisha Uchumi wa Viwanda.
Wizara ya Viwanda na Biashara imeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla ya Sh. Bilioni 137.8 kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 kwa ajili ya kutekeleza mipango ya kuendeleza Sekta ya Viwanda na Biashara nchini ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukuza uchumi wa viwanda na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo Mei 22, 2026 bungeni jijini Dodoma, Mhe. Judith Kapinga (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara amesema kati ya fedha hizo Sh. Bilioni 104.1 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Serikali.
Waziri amesema kuwa kati ya fedha hizo, za matumizi ya kawaida, Sh. Bilioni 78 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi wa Wizara, Sh. Bilioni 26 zimetengwa kwa ajili ya matumizi mengine ya uendeshaji wa shughuli za kila siku.
Aidha, Waziri amebainisha kuwa Sh. Bilioni 33.6 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo yote ikiwa ni fedha za ndani ya Serikali, hatua inayoonesha dhamira ya kuongeza Uwekezaji katika Sekta ya Viwanda na Biashara.
Waziri ameongeza kuwa Bajeti hiyo inalenga kuimarisha mazingira ya uwekezaji, kuongeza uzalishaji wa viwanda vya ndani, kukuza biashara na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na kimataifa.
"FCC Kwa utendaji wa haki katika uchumi wa soko".

22/05/2026
22/05/2026
22/05/2026
22/05/2026