04/06/2017
Thank u to all the fans. 2 my teammates. 2 everyone at and CFA. A class football club to play for. Enjoyed every bit of it and it was an experience of a lifetime.
TWFA ni Chama cha Mpria wa Miguu kwa Wanawake Tanzania kilichosajiliwa katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Chini ya Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa
04/06/2017
Thank u to all the fans. 2 my teammates. 2 everyone at and CFA. A class football club to play for. Enjoyed every bit of it and it was an experience of a lifetime.
18/03/2016
Kila lenye kheri Twiga Stars, matokeo ya Moira ni popote, tunaamini mnaweza sana tu, tuchapieni hao Zimbabwe .
03/09/2015
Kila la kheri timu yetu Twiga Stars huko Congo Brazzavile! tunawaamini, tunajua mnaweza
08/04/2015
Timu yetu Twiga Stars Ijumaa hii ya Aprili 10 itakuwa na kazi ya kumalizia kibarua chake dhidi ya Zambia, mechi ya kwanza tuliwapiga 4-2 kwao Lusaka, sasa ni zamu yetu nyumbani, tuungane kuishangilia timu yetu, kiingilio buku tano VIP, buku mbili kawaida, mechi hii ni ya mwisho baada ya hapo tunafuzu All African Games, Congo Brazzavile Septembe, Kauli mbiu, 'Tumefika Congo, bado ubingwa Afrika, we need your Support'
Kazi ya kwanza Lusaka imekwisha, tumeshinda mechi 4-2 dhidi ya Shipolopolo, kazi ya pili itakuwa mechi ya marudiano Dar esSalaam, kila la kweli Twiga Stars, tuungane kuwasapoti wasichana wetu
Timu yetu ya taifa ya soka ya wanawake Twiga Stars leo ipo Lusaka, Zambia ikimenyna na Shipolopolo uwanja wa Nkoloma, kuwania kufuzu michezo ya Afrika, mechi hii ni muhimu mno, dua zetu zote zielekee kwao tafadhali, Kila la Kheri Twiga Stars!
11/03/2015
Mabingwa wa kwanza wa michuano ya kombe la Taifa la soka kwa wanawake TEMEKE (TMK QUEEN) baada ya kukabidhiwa kombe lao ilipoifungwa Pwani bao 1-0 kwenye fainali zilizofanyika Azam Complex Chamazi mwanzoni mwa mwaka huu. Huu ni mwanzo tu, mashindano mengi ya wanawake yanakuja.
15/12/2014
Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzanite (U-20) na ile ya Tigwa Stars (Senior) Sheridah Boniface akipokea tuzo yake ya mwanamichezo bora wa mwaka 2013/2014 kutoka kwa rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein katika hafla ya kukabidhi tuzo hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Desemba 12. Mbali na tuzo hiyo Sheridah pia alitwaa tuzo ya mwanasoka bora wa k**e, na mwanamichezo chipukizi. Tunakupongeza Sheridah na usiishie hapo, uendelee, ujaze tuzo kwenye kabati lako.
Wadada wetu wa Twiga Stars leo watacheza na wadada wa Zambie, Shepolopolo, mechi ni bure uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuanzia saa kumi jioni, sote tuungane huko tukawape moyo wachezaji wetu
TIMU yetu ya taifa wa wakubwa, Twiga Stars inacheza na wenzao wa Zambia, Shepolopolo Ijumaa. Mechi hii ni ya kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa Wanawake, tunahitaji ushindi hata wa bao 1-0 kusonga mbele, mechi itachezwa uwanja wa Azam Comlpex Chamazi, hakuna kiingilio, tunaowamba sapoti yenu Watanzania, hii ni timu yetu sote, Mungu saidia Twiga Stars!
Timu yetu ya Twiga Stars imepoteza mechi na Zambia, tusikate tamaa, mapambano yanaendelea mechi ya marudiano nyumbani
Heri ya mwaka mpya wadau wa soka ya wanawake, tunawatakia kila la kheri katika mwaka huu wa 2014 na Inshallah uwe wenye mafanikio kwenu,