Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Share

Commission for Human Rights and Good Governance is an Independent Government Institution as per Article 129 of the URT Constitution and Act No.3 of 2000

Photos from Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.'s post 03/08/2025

THBUB yapongezwa kutoa elimu nanenane.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bi Victoria Mwanziva wakati alipotembelea banda la THBUB katika Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Ngongo lindi Agosti 2,2025.

Mhe.Mwanziva amesema kuwa wananchi wengi hawajui haki zao,uwepo wa THBUB hapa itasaidia wengi kupata elimu hiyo.

"Ni muhimu kila mtu kujua haki zake na wajibu pia elimu"amesema Bi.Mwanziva

Photos from Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.'s post 03/08/2025

WANAFUNZI WAPATIWA ELIMU YA HAKI ZA BINADAMU

Haki za binadamu zinaendana na wajibu,

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Uchunguzi Mkuu Bw. Fadhili Muganyizi wakati akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari St Gabriel Tech walipotembelea Banda Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika Maonesho ya Kitaifa ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

Bw. Muganyizi amesema kuwa watoto wana haki ya kuishi, kusikilizwa, kutoa maoni, kupata taarifa na haki ya kupata elimu

"Haki zote ni muhimu kuzipata na THBUB pia ina jukumu la kutoa elimu kwenu ili muweze kuzijua" amesema Bw. Muganyizi

Pia Bw. Muganyizi amewaeleza wanafunzi hao kuhusu wajibu wao wanapokuwa shuleni na katika Jamii kwani wao ni viongozi wa baadae.

"Pamoja na kuwa na haki ya kupata elimu, pia mna wajibu wa kusoma ili muweze kufaulu sambamba na kuheshimu jamii inayowazunguka ili kuwa viongozi bora wa baadae" amesema Bw. Muganyizia

Aidha, wanafunzi hao walielezwa pia majukumu ya THBUB ambapo pia walipata fursa ya kuuliza maswali kuhusu haki za binadamu na utawala bora .

Kwa wapande wake Anthonia Vendeline Mwanafunzi wa Kidato cha Nne kutoka Shule hiyo ameishukuru THBUB kwa kuwapatia elimu hiyo ambayo imewasaidia kutambua haki na wajibu wao sambamba na kuijua THBUB.

"Tumefurahi, asanteni sana" amesema Anthonia

Photos 25/07/2017

Mafanikio na changamoto za matumizi ya TEHAMA katika masuala ya haki za binadamu.

Tume ya haki za binadamu na utawala bora nchini Tanzania inazidi kufanya kazi zake kwa kujiimarisha kutokana na maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA nchini Tanzania na duniani kwa ujumla.
Katika kuzidi kujiimarisha tume ya haki za binadamu na utawala bora tarehe 11 mwezi Aprili, 2017, ilikutana na waandishi wa habari na wawakilishi wa vikundi mbalimbali ili kuwapa elimu ya haki za binadamu na utawala bora waandishi wa habari na kuwashauri watumie weledi wao katika kuripoti na kuandika taarifa zao kwa jicho la haki za binadamu
Katika semina/warsha hiyo iliyofunguliwa na kamishina wa haki za binadamu na Utawala bora Salma Ali Hassan mambo mengi yalijadiliwa lakini kubwa zaidi ilikuwa nafasi ya vyombo vya habari katika kuelimisha umma wa watanzania kuhusiana na haki za binadamu.

Wakati akifungua warsha hiyo iliyofanyika jijini Mwanza , kamishina wa tume hiyo Salma Ali Hassan alisema kuwa ni wazi kuwa waandishi wa habari, wapiga picha na watengenezaji wa vipindi mara nyingi wamekuwa wakiweka wazi masahibu wanayopata watu k**a kudhalilishwa na kuonewa na watu wengine. Hivyo, aliwataka waandishi wa habari kutumia weledi na umakini wao katika kuyaripoti na kuyaandika masahibu hayo
Mafanikio ya TEHAMA katika masuala ya haki za binadamu
Ikiwa tume hiyo sasa inajiweka karibu na vyombo vya habari , lakini pia kutokana na maendeleo ya teknolojia ya habari na mwasiliano TEHAMA,masuala muhimu ya haki za watu katika jamii yetu yaliweza kujadiliwa na washiriki.

Maendeleo ya TEHAMA yamekuja na mabadiliko mengi katika kusaidia utoaji wa taarifa za masuala ya haki za binadamu nchini Tanzania. Kwa mfano, tukio la mwaka jana 2016 la mwanafunzi aliyeshambuliwa na walimu mkoani Mbeya liliweza kurekodiwa kwa kutumia simu ya mkononi jambo lilisababisha taarifa zile kusambaa nchi nzima.

Lakini pia maendeleo ya TEHAMA yamekuwa na mchango mkubwa sana katika usalama wa watu kwa njia ya mitandao. Kutokana na maendeleo ya TEHAMA nchini Tanzania watu mbalimbali wamekuwa wakitumia uhuru wao na haki yao ya kujieleza na kutoa maoni yao kwa kutumia mitandao ya kijamii. Yote haya yanaifannya Tume ya haki za binadamu na utawala bora nchini Tanzania kuwa karibu na watanzania kwa kupata taarifa nyingi zinazohusiana na masuala ya haki za binadamu na utawala bora.

Mbali na hilo, kutokana na kuimarika kwa teknolojia ya habari na mawasiliano tume ya haki za binadamu pia imekuwa ikipokea malalamiko mbalimbali kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi yaani SMS kwa namba 0754 460259. Kwa kutumia mfumo huu, tume imekuwa ikipokea malalamiko mbalimbali na kuyafanyia kazi kwa mujibu wa taratibu za uendeshaji wake.
Lakini pia katika warsha iliyofanyika jijini Mwanza , waandishi wa habari walifundishwa kuhusu Human Rights Based Approach(HRBA) ambayo inawataka waandishi wa habari kuzingatia haki za binadamu katika kila habari wanayoandika na wanayoripoti.

Katika uwasilishaji wake Bwana Albert Kakenki alisema kwa kutumia dhana ya HRBA waandishi wa habari wanatakiwa wazingatie maeneo matatu muhimu ambayo ni nia ya kuandika habari(goal), mchakato wa kuandika habari(process) na matokeo yanayotegemewa baada ya habari kuandikwa au kuripotiwa (outcome).

Baada ya uwasilishaji wake bwana kakenki alisema kuwa tume sasa hivi inajitahidi kutoa semina mbalimbali kwa waandishi wa habari katika kanda na mikoa mbalimbali ili kuzingatia haki za binadamu kwa namna habari zinavyoandikwa na kuripotiwa
Changamoto za TEHAMA katika masuala ya haki za binadamu
Katika masuala ya haki za binadamu kumekuwa na matukio mengi yanayoashiria changamoto za TEHAMA katika kuripoti matukio haya. Mengi ya matukio haya ni yale ya uvunjifu wa haki za binadamu kutokana na maendeleo ya TEHAMA hasa kwa kutumia simu za mkononi za kupangusa(smartphones)
Kwanza, kumekuwa na usambazaji wa picha za watu waliokufa kwa ajali mbaya . picha hizi zimekuwa hazizingatii haki ya wanaozitazama kwa sababu si kila mtu ana uwezo wa kuangalia picha za mtu aliyekufa kwa ajali mbaya huku zikitoa kabisa utu (dignity)

Pili, kumekuwa na uingiliaji wa faragha za watu (privacy) kwa kuingilia uhuru wa mtu na maisha yake binafsi. Haya yamekuwa yakifanyika kwa watu kupiga picha au kurekodi sauti za watu bila ridhaa yao na kuvunja haki yao ya faragha ambayo inatambulika kikatiba.

Tatu, kumekuwa na udakaji (hacking) wa taarifa za watu kwa kutumia simu za kupangusa(smartphone) jambo ambalo pia limekuwa likiingilia uhuru wa mtu katika kuwa na taarifa zake. Hii inahatarisha hadi usalama wa taarifa za watu katika barua pepe yaani e-mail zao.

Nne, kumekuwa na utoaji wa taarifa za uchochezi (seditious information) kwa kutumia simu za mkononi ni kuondoa haki za upande mmoja unaolemewa. Haya yamesababisha hadi baadhi ya watu kukumbwa na adhabu kutokana na sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2016 yaani Cyber Crime Act of 2016
Hatimaye washiriki na waandishi wa habari katika warsha hiyo walipata nafasi ya kuuliza maswali ambayo yalijibiwa na maafisa mbalimbali wa tume wakiwemo wanasheria na viongozi. Miongoni mwa mambo yaliyozua mjadala ni uhuru wa chombo hicho kilichoanzishwa kwa sheria na. 7 ya mwaka 2001 ambapo maelezo yaliyotolewa ni kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo tume ya haki za binadamu ni chombo huru japo iko chini ya ofisi ya rais.

Mwisho

Chanzo: Semina ya tume ya haki za binadamu na utawala bora Mwanza

Imeandikwa na Yohani Gwangway

Photos 01/06/2017

Machapisho na mada yalitolewa kwa washiriki kwa nia ya kufanya marejeo na kueneza zaidi elimu ya haki za binadamu kwa umma. Machapisho yaliyotolewa zaidi ya mada zilizowasilishwa ni pamoja na:
• Kipeperushi cha kuelezea njia ya kuasilisha malalamiko kwa njia ya ujumbe wa simu ya kiganjani (SMS)
• Azimio la ulimwengu juu ya haki za Binadamu nakala 40
• Mkataba wa Kimataifa wa haki za Kiraia na Kisiasa nakala 100
• Mkataba wa Kimataifa wa haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni nakala 100
• Kijitabu_Mambo 101 Unayohitaji Kuyafahamu Kuhusu Polisi Lakini Unaogopa Kuyauliza nakala 100
• Kipeperushi_Zijue Haki zako Kubali wajibu wako nakala 100
• Kipeperushi_Utawala Bora (Dhana, misingi na umuhimu) nakala 100
• Kipeperushi_Utaratibu wa Kuwasilisha Malalamiko Tume nakala 100
• Kijitabu_Zijue Haki za Raia Katika Mfumo jinai nakala 100

Photos from Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.'s post 01/06/2017

Warsha hiyo ilihudhuriwa na washiriki wanawake na wanaume kutoka katika Vyombo mbali mbali vya habari vikiwemo Televisheni, Redio na magazeti.

Photos 01/06/2017

Warsha Kuhusu Elimu Ya Haki Za Binadamu Na Utawala Bora Kwa Wanahabari Iliyofanyika Hoteli Ya Lakairo Jijini Mwanza Tarehe 11/4/2017.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ofisi ya kanda ya ziwa iliandaa na kuendesha warsha kuhusu Elimu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa wanahabari Tarehe 11.04.2017 katika hoteli ya Lakairo jijini Mwanza. Warsha hiyo ilifunguliwa na Mhe. Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi.Salma Ally Hassan na kufungwa na Afisa Mfawithi Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kanda ya Ziwa Bw.Albert Kakengi. Warsha hiyo ilifanyika chini ya Programu ya Mfumo unaotumika kuwasilisha malalamiko kwa njia ya Kielektroniki inayotumia ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani SMS (Support for SMS for Human Rights System) ambao unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA).

Photos from Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.'s post 29/09/2016

Lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwaongezea washiriki wa mafunzo uelewa kuhusu haki ya afya, upatikanaji wa huduma za haki ya afya kwa makundi maalumu na matumizi ya mfumo wa kielektroniki katika kuwasilisha malalamiko yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora mbele ya Tume.
Mafunzo hayo yalihudhuriwa na jumla ya washiriki 44 wakiwemo wanawake 32 na wanaume 12. Washiriki hawa walitoka katika Manispaa ya Lindi na wawezeshaji kutoka THBUB Ofisi ya Lindi na Makao Makuu Dar es Salaam.

Photos from Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.'s post 29/09/2016

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora imeendesha mafunzo kuhusu upatikanaji wa huduma za afya (haki ya afya) na uwasilishaji malalamiko tume kwa njia ya ujumbe wa simu ya kiganjani kwa makundi yanayobaguliwa (makundi maalumu) Lindi tarehe 22-23/9/2016. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utabibu kilichopo Mkoa wa Lindi, Manispaa ya Lindi. Mafunzo hayo yaliandaliwa na kuratibiwa na THBUB Ofisi ya Lindi kwa ufadhili wa Shirika la Kimaendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA) chini ya mradi wa mfumo unaotumika kuwasilisha malalamiko kwa njia ya kielektroniki wa sms (Support for sms for Human Rights System). Mafunzo hayo yalilenga washiriki wa makundi maalumu katika jamii ngazi ya mitaa, vijiji na kata. Mafunzo hayo yalifunguliwa na kufungwa na Bw. Abdalah M. Majumba Mwenyekiti wa Chama cha Wastaafu na Wazee Lindi ambaye pia alikuwa ni mshiriki wa mafunzo hayo akiwakilisha kundi la wazee.

Photos from Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.'s post 12/09/2016

Utaratibu huu wa ujumbe wa Simu ya kiganjani unategemea kutaharakisha mawasiliano kati ya Tume na walalamikaji kwa upande mmoja na kati ya Tume na walalamikiwa, ukilinganisha na njia za awali ambazo bado zinaendelea kutumika ingawa zina changamoto mfano matumizi ya barua kwa njia ya posta ambayo inachukua muda mrefu na kukabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo kupotea kwa barua na wananchi wengi kutokuwa na anuani za posta za uhakika Utaratibu huu mpya unatarajia/unategemea kupunguza usumbufu na gharama kwa walalamikaji, hususan watokao pembezoni mwa nchi katika kuwasilisha malalamiko yao ofisi za Tume na kupata mrejesho

Photos from Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.'s post 12/09/2016

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeendesha warsha ya siku mbili katika halmashauri ya Arusha inayohusu elimu ya Haki afya na matumizi ya simu ya kiganjani katika kuwasilisha malalamiko na taarifa kuhusu uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya Utawala bora mbele ya Tume.
Lengo la warsha hiyo ni kuelimisha umma hasa kwa watu kutoka vijijini juu ya haki afya na matumizi ya teknolojia ya simu katika kutoa taarifa za matukio ya uvunjifu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora mbele ya Tume kwa urahisi. Warsha hii ililengwa kuwanufaisha zaidi washiriki wa makundi maalumu katika jamii wakiwemo wazee, watoto, wanawake, wakimbizi, watu wenye ulemavu na makundi madogo katika jamii.

Photos from Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.'s post 12/09/2016

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeendesha warsha kuhusu elimu ya Haki afya na matumizi ya ujumbe wa simu ya kiganjani kuwasilisha malalamiko mbele ya Tume. Warsha hiyo ililenga washiriki wa makundi maalumu katika jamii kutoka katika maeneo ngazi ya mitaa, vijiji na kata. Katika Mkoa wa Arusha warsha hii ilifanyika Tarehe 11-12/9/2016 katika kata ya Murieti, Wilaya ya Arusha, Shule ya King David, eneo lijulikanalo kwa jina maarufu la “kwa Mrombo” nje kidogo ya jiji la Arusha. Warsha Hiyo ilifunguliwa na na kufungwa na Bw. Wilfred Warioba Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ambaye pia ni mratibu wa Mradi wa Mfumo unaotumika kuwasilisha malalamiko kwa njia ya Kielektroniki ya Mfumo wa SMS (Support for SMS for Human Rights System) ambao unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA).

Photos from Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.'s post 08/09/2016

Mtoa mada/Mwezeshaji Philipo Sungu kutoka CHRAGG akiwasilisha mada ya kuhusu Uwasilishaji wa malalamiko Tume kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani katika warsha inayoendelea ya Haki ya Afya na uwasilishaji malalamiko mbele ya Tume kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani (SMS) inayofanyika katika ukumbi wa mikutano Lakairo Hotel tarehe 7/9/2016

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 19:00 - 03:30
Tuesday 19:00 - 03:30
Wednesday 19:00 - 03:30
Thursday 19:00 - 03:30
Friday 19:00 - 03:30