Uongozi na siasa

Uongozi na siasa

Share

uongozi ndani ya nchi ulivyo mezwa na siasa

27/01/2026

*SERIKALI KUENDELEA KUFANYA MAGEUZI YA SERA– DKT. MWIGULU*

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kufanya mageuzi ya sera zinazogusa moja kwa moja maslahi na ustawi wa maisha ya wananchi.

Amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia watendaji wa Serikali wanaotoa visingizio, wasiowajibika na wenye hulka ya kufanya kazi kwa mazoea, ujanja ujanja na kutoa taarifa za michakato badala ya majibu yanayotakiwa.

Amesema hayo Bungeni leo (Jumanne, Januari 27, 2026) wakati akitoa hoja ya kujadili hotuba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa jijini Dodoma wakati akizindua Bunge la 13 Novemba 14, 2025.

“Tunapozungumzia utendaji Serikalini, msisitizo ni uadilifu na uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi waliotuchagua ili kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali za nchi pamoja na kupata huduma wanazostahili.”

Dkt. Mwigulu amesema kuwa hotuba aliyoitoa Rais Dkt. Samia ilitoa mwelekeo na dira ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha pili. “Hotuba ya Mheshimiwa Rais ilitoa maelekezo na kubainisha changamoto pamoja na majukumu yanayotupasa kuyatekeleza kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa maendeleo.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kutekeleza vipaumbele vyote vilivyoainishwa. “Serikali imeainisha maeneo mbalimbali ya utekelezaji na kupanga mipango kazi ya utekelezaji wa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu, na tayari utekelezaji wake umeshaanza kutekelezwa kwenye maeneo kadhaa”.

27/01/2026

Baraka Tele na Mafanikio kwa Mama wa Taifa – Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Na: comrade David Michael mlope (Zola d King

Katika siku hii adhimu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, tunamwombea baraka tele, afya njema, na mafanikio yasiyo na kikomo Rais wetu mpendwa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan – mama wa taifa, kiongozi wa kipekee, na dira ya matumaini kwa Watanzania wote.

Mhe. Rais Samia ni mfano wa uongozi wa hekima, uvumilivu, na maono ya kweli. Tangu alipochukua hatamu za uongozi, ameendelea kuonyesha dhamira ya dhati ya kuijenga Tanzania mpya – yenye usawa, maendeleo jumuishi, na heshima kwa utu wa kila Mtanzania. Kupitia kauli mbiu yake ya “Kazi na Utu”, amekuwa akihimiza maendeleo yanayozingatia haki, mazingira, na ustawi wa jamii.

Kupanda mti wa Muembe katika ardhi ya Bungi Kilimo, Unguja, si tu tukio la kimazingira bali ni ishara ya uhai, urithi, na matumaini. K**a mti huo utakavyokua na kuzaa matunda, ndivyo pia uongozi wake unavyoendelea kuzaa matunda ya maendeleo, mshik**ano, na heshima kwa taifa letu.

Tunamwombea:

- Baraka za Mungu katika kila hatua ya maisha na uongozi wake
- Afya njema ili aendelee kulitumikia taifa kwa nguvu na ari
- Hekima na busara katika kufanya maamuzi ya kitaifa
- Upendo wa wananchi na mshik**ano wa kitaifa
- Mafanikio ya kudumu katika juhudi za kuijenga Tanzania ya kisasa na endelevu

Kwa niaba ya Watanzania wote wenye mapenzi mema, tunasema:

Heri ya kuzaliwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan – mama yetu wa pekee, kiongozi wetu wa kipekee. Mungu akulinde, akubariki, na akufanikishe zaidi.





07/09/2025

*Tumpe Miaka Mingine Mitano Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan*

Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania, imekuwa desturi kwa Rais anayeonyesha uongozi thabiti na mafanikio katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza kupewa fursa ya kuendelea kwa miaka mingine mitano, ili akamilishe miaka kumi ya kulitumikia taifa.

Kwa mwaka 2025 hadi 2030, Watanzania tunayo nafasi ya pekee ya kutambua na kuthamini mchango mkubwa wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Baada ya kuondokewa na mpendwa wetu, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, taifa letu lilipitia changamoto kubwa, lakini Mheshimiwa Rais Samia aliinua bendera ya matumaini na kuendeleza jitihada za maendeleo kwa umakini na hekima ya hali ya juu.

Uongozi wake umejikita katika mshik**ano wa kitaifa, diplomasia ya kimataifa, kukuza uchumi, na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika medani za kikanda na kimataifa. Kwa kazi kubwa alizozifanya na changamoto alizozishinda, ni wazi kabisa kwamba Rais Samia Suluhu Hassan anastahili kupewa miaka mingine mitano, ili kuendeleza dira ya maendeleo na kulitumikia taifa letu hadi mwaka 2030.

🖊️ Makala hii imeandaliwa na
✍️ Imehaririwa na

Photos from Uongozi na siasa's post 17/07/2025

Leo ni siku muhimu na ya kihistoria kwa nchi yetu ambapo tumehitimisha safari tuliyoianza miaka miwili iliyopita kwa kuzindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ikiwa ni mara ya pili kwa Taifa letu kufanya hivi tangu Uhuru. Dira hii ni maoni ya wananchi wote ambapo kwa miaka 25 ijayo wamedhamiria kujenga Taifa jumuishi, lenye ustawi, haki na linalojitegemea.

Tumefikiri wenyewe, tumepanga wenyewe, tumeandika wenyewe na hatua inayofuata ni utekelezaji. Hatua hii inahitaji kila mwananchi kufanya kazi kwa ari, nguvu, maarifa na bidii na kuwepo ushirikiano wa dhati kati ya serikali, sekta binafsi na wadau wa maendeleo. Aidha, hatuna budi kuendelea kudumisha amani, umoja, mshik**ano na utulivu nchini ili tufikie shabaha na malengo tuliyojiwekea.

Ninawapongeza wote, hasa wananchi, walioshiriki katika maandalizi ya dira hii, na hivyo kuipa umiliki na taswira ya kitaifa. Mmetimiza wajibu wenu, nami ninawahakikishia kuwa, tumeweza kutekeleza mengi, tutaweza kutekeleza dira hii.

15/07/2025
Photos from Uongozi na siasa's post 15/07/2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa salamu za shukrani kwa kupokea Tuzo ya Miaka 30 ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa niaba ya Familia ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 15 Julai 2025, katika hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya Baraza hilo iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) Arusha.

Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa tuzo hiyo ni uthibitisho wa mchango mkubwa wa Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi, aliyeruhusu kuanzishwa kwa vyombo vya habari binafsi na kutoa uhuru kwa wanahabari, hatua iliyochangia kwa kiasi kikubwa kujenga na kuimarisha tasnia ya habari nchini Tanzania.

07/07/2025

Mwisho Mwampamba agombea nafasi ya udiwani katika Kata ya Boma, hiyo itakuwa hatua mpya katika maisha yake . Hapa kuna *wasifu wa kina wa Mwisho Mwampamba*, mmoja wa Watanzania waliowahi kupata umaarufu mkubwa kupitia kipindi cha Big Brother Africa:makala hii imeandaliwa na Ungozi na Siasa na CDE. David Michael Mlope.

Jina Kamili: Mwisho Mwampamba
Toka: Morogoro, Tanzania
Kazi: Mjasiriamali (Self-employed)
Elimu: Cheti cha Sekondari (High School Diploma)
Hali ya Mahusiano: Katika uhusiano
Urefu: 1.72m
Kauli mbiu: “To always be happy, life is too short.”
Kauli pendwa: “Information is power.

📺Umaarufu Kupitia Big Brother Africa
Mwisho alipata umaarufu mkubwa baada ya kushiriki katika misimu miwili ya _Big Brother Africa(BBA)
| Msimu | Mwaka | Nafasi Aliyomaliza | Siku Alizokaa ndani ya Mjengo.
| Season 1 | 2003 | Nafasi ya 2 (Runner-up) | 106 |
| Season 5 (All Stars) | 2010 | Nafasi ya 4 | 91 |
| *Jumla* | — | — | *197* |

Katika msimu wa kwanza, Mwisho alijulikana kwa haiba yake ya urafiki, utulivu, na ucheshi. Alikuwa mmoja wa washiriki waliopendwa sana na watazamaji barani Afrika.

Maisha ya Baadaye
Baada ya Big Brother:
- Aliripotiwa kuishi Morogoro, karibu na hifadhi ya taifa, akifurahia maisha ya utulivu na amani
- Alionekana kwenye kipindi cha televisheni kinachoitwa Boys Boys Talk kilichorushwa na TV1 Tanzania akishirikiana na Bingwa wa Ngumi uzani wa juu ambaye ni rafiki wake wa karibu sana Zola D King.
- Kwa mujibu wa mijadala ya mtandaoni, baadhi ya watu walimwona akijihusisha na shughuli za kilimo, hasa mpunga, maeneo ya Ifakara na Morogoro

Hobbies na Vipaji
- Kuogelea (swimming)
- Kupanda milima (hiking)
- Michezo mbalimbali: rugby, basketball, squash, volleyball, table tennis
- Kusoma vitabu
- Anajulikana kwa kusema: “Sina muda wa kukasirika, nina mambo bora ya kufanya!”

Tunakuombea sana Ndugu yetu mwisho mwampamba katika nafasi Yake ya udiwani hakika anafaa kuwa kiongozi kijana yupo na maono makubwa

Wasiliana nasi, E-mail: [email protected]
ni mtu mchapa kazi kweli kweli

20/05/2025

Rais Samia Suluhu Hassan Atoa Onyo Kali kwa Wanaharakati wa Kigeni

Katika hatua inayozua mjadala mkubwa, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa onyo kali kwa wanaharakati wa kigeni, akisisitiza kuwa Tanzania haitaruhusu kuingiliwa na wageni katika masuala yake ya ndani. Kauli hii imekuja baada ya serikali kuwak**ata na kuwafukuza wanaharakati kadhaa wa Afrika Mashariki waliokuwa wamewasili nchini kuhudhuria kesi ya mwanasiasa wa upinzani, Tundu Lissu.

Rais Samia ameeleza kuwa baadhi ya wanaharakati kutoka mataifa jirani wanajaribu kuvuruga amani ya Tanzania, akisema kuwa nchi hiyo haitavumilia "machafuko" yanayoletwa kutoka nje. Aidha, vyombo vya usalama vimeagizwa kuhakikisha kuwa watu wasio na maadili kutoka nje ya nchi hawapati nafasi ya kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania.

Hatua hii imeibua ukosoaji kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu, hasa kutoka Kenya, ambao wanapanga kuishtaki serikali ya Tanzania kwa kile wanachodai kuwa ni ukiukaji wa haki za kibinadamu. Mwanaharakati mashuhuri wa Kenya, Boniface Mwangi, bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Tanzania, huku mke wake akieleza kuwa hajafanikiwa kuwasiliana naye tangu alipok**atwa.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amesisitiza kuwa vitendo vya serikali yake havina upendeleo bali ni sehemu ya juhudi za kulinda mamlaka na uthabiti wa taifa. Hali hii inaendelea kuzua mjadala kuhusu mipaka ya uhuru wa wanaharakati na mamlaka ya serikali katika kudhibiti shughuli zao.

Wasiliana nasi, E-mail: [email protected]
.

Photos from Uongozi na siasa's post 20/05/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, *Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan* akimkaribisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia *Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah* mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Mei, 2025.🇹🇿💪

11/04/2025

Hivi karibuni, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, alikutana na Profesa Abdulrazak Gurnah, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi ya mwaka 2021, jijini London. Mkutano huu ulikuwa wa kihistoria, ukizingatia mchango mkubwa wa Profesa Gurnah katika fasihi ya Kiswahili na kimataifa, pamoja na nafasi yake k**a mmoja wa Watanzania waliotambuliwa kimataifa kwa kazi zao za kipekee.

Katika mazungumzo yao, Rais Mwinyi alimpongeza Profesa Gurnah kwa mafanikio yake makubwa, akisisitiza jinsi tuzo hiyo ilivyoipa heshima kubwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Aidha, walijadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya fasihi, elimu, na umuhimu wa kuendeleza lugha ya Kiswahili k**a nyenzo ya kuimarisha utamaduni na urithi wa Kiafrika.

Profesa Gurnah, ambaye ni mzaliwa wa Zanzibar, alionyesha shukrani zake kwa heshima aliyopewa na Rais Mwinyi, huku akisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuandika na kuchangia katika kukuza fasihi ya Kiswahili na kimataifa. Mkutano huu ulionyesha mshik**ano wa viongozi na wasanii katika kukuza utamaduni na elimu, na ni mfano wa jinsi ushirikiano wa aina hii unavyoweza kuleta maendeleo chanya katika jamii.

Wasiliana nasi, E-mail: [email protected]
.hmwinyi

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


SalaSala
Dar Es Salaam