05/06/2026
Akikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchini leo 5.6.2026 jijini Dodoma amesema tuzo hiyo imetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza kilimo himilivu dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi na matumizi endelevu ya rasilimali za asili na uwekezaji katika teknolojia rafiki kwa mazingira.
Tuzo hiyo imepokelewa na Bi. Hawabai Adbulla kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji akiambatana na Bw. Alex Ndikile Katibu wa Mkurugenzi Mtendaji.
31/05/2026
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Kakurwa, ameipongeza TADB kwa utekelezaji wa Mradi wa TI3P, umeongeza thamani na kuchochea uzalishaji, kuimarisha mnyororo wa thamani na kuboresha maisha ya wafugaji katika sekta ndogo ya maziwa nchini.
Mhe. Waziri ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la TADB katika Maonesho ya 29 ya Wiki ya Maziwa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwembetogwa mkoani Iringa ambapo alipokea taarifa za utekezaji wa mradi wa TI3P kutoka kwa Mratibu wa Mradi huo Bw. Joseph Mabula.
Mhe.Waziri pia amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau wa kwenye sekta ndogo ya maziwa ili kuongeza tija kuchochea uzalishaji na kupanua masoko ya maziwa nchini, akieleza kuwa uwekezaji k**a wa TI3P ni nguzo muhimu ya mageuzi ya sekta hiyo.
30/05/2026
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Fabian Madele, ameusifu Mradi Shirikishi wa Wasindikaji na Wazalishaji wa Maziwa (TI3P) kwa mchango wake katika kuimarisha mnyororo wa thamani wa maziwa kupitia kuwaunganisha wazalishaji na wasindikaji wa maziwa nchini.
Dkt. Madele alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la TADB katika Maonesho ya 29 ya Wiki ya Maziwa yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwembetogwa mkoani Iringa, ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa Mratibu wa TI3P, Joseph Mabula.
Aidha, ameipongeza TADB kwa juhudi zake katika kuendeleza sekta ndogo ya maziwa na kuitaka kuongeza nguvu katika kuwaunganisha wafugaji na wadau wengine wa mnyororo wa thamani, pamoja na kuimarisha vyama vya ushirika ili kuwawezesha wafugaji wadogo kuongeza uzalishaji, tija na ushindani wa sekta hiyo.
30/05/2026
MAONESHO YA MIFUGO KANDA YA ZIWA (LAKEZONE LIVESTOCK EXPO) 2026
Mgeni Rasmi wa Maonesho ya Mifugo Kanda ya Ziwa 2026, Bi. Agnes Meena, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ameipongeza TADB kwa kuendelea kuwa suluhisho la mitaji kwa wafugaji nchini.
Akizungumza katika ufunguzi wa maonesho hayo, ameisihi TADB na wadau wengine wa sekta ya mifugo kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto za wafugaji na kuongeza tija katika ufugaji wa kibiashara.
Hadi sasa, TADB imetoa TZS bilioni 119 kwa maendeleo ya sekta ya mifugo, zikinufaisha Watanzania 60,848 kupitia uwekezaji katika ng’ombe wa maziwa, ng’ombe wa nyama, kuku na mifugo mingine.
30/05/2026
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imehudhuria Media Semina katika maadhimisho ya 29 ya Wiki ya Maziwa yanayoendelea mkoani Iringa, huku kilele cha maadhimisho hayo kikitarajiwa kufanyika tarehe 1 Juni 2026.
Katika semina hiyo TADB ilitoa elimu ya uelewa kuhusu majukumu na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo kwa wadau wa sekta ya kilimo na mifugo.
Aidha, washiriki walipata fursa ya kufahamu kuhusu Mradi wa TI3P na namna ulivyowanufaisha wafugaji pamoja na wadau wa sekta ndogo ya maziwa nchini kwa kuwawezesha kuongeza uzalishaji na kuboresha biashara zao.
Sambamba na hilo, TADB ilieleza umuhimu wa lishe bora na namna maziwa yanavyochangia kukamilisha mlo kamili kwa afya bora ya jamii.
27/05/2026
Tunawatakia Waislamu wote na Watanzania wote Sikukuu njema ya Eid-al-Adha yenye amani, furaha, upendo na baraka tele.
23/05/2026
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo tarehe 23.05.2026 imeendesha semina kwa wamiliki na wahariri wa redio za kijamii zipatazo 50 toka Tanzania Bara na Zanzibar. Lengo kuu lilikuwa ni kukuza uelewa juu ya majukumu ya TADB pamoja na kuonesha fursa zinazopatikana katika benki hiyo.
Aidha, washiriki wamejengewa uwezo wa kuripoti masuala ya maendeleo ya sekta ya kilimo, fedha za kilimo, na nafasi ya taasisi za kifedha katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa kilimo nchini. Hivyo, Mafunzo hayo yataimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya kijamii na TADB katika kuhamasisha uelewa wa umma kuhusu fursa za uwezeshaji wa kifedha kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wadau wengine wa mnyororo wa thamani katika sekta ya kilimo.
Semina hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Jengo la Mkandarasi Jijini Dodoma na kufunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Mipango, Ushauri na Mahusiano ya Taasisi TADB, ndugu Mkani Waziri, ambaye amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika kuelimisha jamii kuhusu mchango wa sekta ya fedha kwenye maendeleo ya kilimo na uchumi wa taifa kwa ujumla.
19/05/2026
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Bodi ya Usimamizi wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) leo Mei 19, 2026 zimesaini mkataba wa ushirikiano wa kikazi wenye lengo la kuongeza tija katika sekta ya kilimo, kuimarisha usimamizi wa mazao baada ya mavuno na kupunguza upotevu wa chakula nchini.
Makubaliano hayo yamesainiwa katika kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya WRRB yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Mwigulu Nchemba.
Mkataba huo umesainiwa kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Frank Nyabundege, na Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Asangye N. Bangu.
Ushirikiano huo unalenga kuimarisha mifumo ya uhifadhi wa mazao kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala, kuongeza thamani ya mazao, kuboresha upatikanaji wa masoko na huduma za kifedha kwa wakulima, pamoja na kuchochea usalama wa chakula na maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.
StakabadhiZaGhal