16/10/2025
MIAKA 10 YA TBPL 🔥🔥🔥🔥.
Katika kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Tanzania Biotech Products Limited (TBPL), hafla maalum imefanyika ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, kwa pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Dkt. Nicolas Shombe, wameongoza zoezi la kukata keki ya kumbukizi k**a ishara ya furaha, mafanikio, na ukuaji endelevu wa kiwanda hicho.
Tukio hilo limeudhuriwa na viongozi wa serikali, wadau wa sekta ya viwanda, watafiti, na wafanyakazi wa TBPL na NDC.Limeakisi safari ya mafanikio ya kiwanda hicho katika kipindi cha miaka kumi, safari iliyojengwa juu ya misingi ya ubunifu wa teknolojia za kibaiolojia, uzalishaji wa bidhaa bora, na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa viwanda nchini.
16/10/2025
MIAKA 10 YA TBPL
“Tumeongeza uwezo wa uzalishaji wa bidhaa za kibayoteki zinazotumika katika sekta ya afya na kilimo. Tumeajiri na kuwajengea uwezo vijana zaidi ya 200 wa Kitanzania katika nyanja za sayansi, utafiti, na teknolojia.Tumewekeza katika miundombinu ya kisasa ya maabara na viwanda, vinavyokidhi viwango vya kimataifa. Tumechangia katika kuimarisha afya ya jamii kupitia bidhaa salama, zenye ubora, na zinazozalishwa hapa nchini”
Maneno ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika laTaifa la Maendeleo (NDC) Dkt. Nicolas Shombe kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 10 ya TBPL.
16/10/2025
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara amewasili Kiwanda cha TBPL katika maadhimisho ya miaka 10.
DKatibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara, Dkt. Hashil Abdallah, amewasili katika kiwanda cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) k**a mgeni rasmi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa kiwanda chichi kinachozalisha bidhaaa bora za kibaolojia nchini.
15/10/2025
TaFF yaitembelea NDC kufanya tathmini ya Mradi wa upandaji Miti
Mapema leo hii 15/10/2025 NDC yapokea ugeni kutoka mfuko wa misitu Tanzania (TaFF ) ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano wa taasisi hizo mbili, ugeni huo ulikuwa na lengo la kufanya tathmini ili kujua changamoto maoni na mapendekezo katika kutekeleza mradi wa kuendeleza shamba la miti ya mpira liliyopo Kalunga mkoani Morogoro
Ushirikiano huo ulikuja baada NDC kupokea ruzuku kiasi cha mil. 400 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kupanda miti ya mpira ambapo mpaka sasa kiasi cha TSh.mi 201 kimepokelewa na kuweza kupanda miti katika hekta zipatazo 38.5
Naye mkurugenzi wa viwanda vya kuongeza thamani NDC
Bi. Esther Mwaigomole amewapongeza TaFF na kuwashauri kuongeza ushirikiano katika maeneo ya utafiti na utunzaji wa miti ya mpira na si upandaji peke yake ili kiuweza kufikia malengo yaliyowekwa.
15/10/2025
MIAKA 10 YA TBPL🔥🔥🔥🔥🔥
Mkoa wa pwani tuna jambo letu Kesho 16/10/2025. Karibuni sana TBPL.
14/10/2025
Leo tunakumbuka shujaa wa uhuru, mwalimu wa amani, na msingi wa taifa letu. Pumzika kwa amani Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 🇹🇿.
10/10/2025
Usikose kutufuatilia hii leo kupitia Star Tv, Tutazungumza juu ya mafanikio ya kiwanda chetu cha TBPL kinachozalisha bidhaa za kibaiolojia bora zaidi barani Afrika.
08/10/2025
Kesho, tarehe 8 Oktoba 2025, kampuni ya Tanzania Bottling & Packaging Limited (TBPL) itakuwa na heshima ya kushiriki kwenye kipindi maarufu cha Good Morning kinachorushwa na Wasafi FM.
Katika mahojiano hayo maalum, tutazungumza kuhusu mafanikio ya miaka 10 ya safari yetu ya kiwanda cha TBPL – tukitazama kwa karibu maendeleo tuliyopata, changamoto tulizovuka, na mipango yetu ya baadaye katika kukuza viwanda na kusaidia maendeleo ya kiuchumi nchini.
Tunawaalika wasikilizaji wote kufuatilia kipindi hiki maalum ili kujifunza zaidi kuhusu historia ya TBPL, ubunifu wetu, mchango wetu kwa jamii, na dira yetu ya muda mrefu katika sekta ya viwanda na biashara.
08/10/2025
Kutana na Meneja masoka wa kiwanda cha kuzalisha dawa za kibaiolojia cha Tanzania Biotech Products Limited akizungumia miaka 10 ya kiwanda hicho kupitia kipindi cha 🇹🇿 cha
06/10/2025
Kutana na Meneja masoka wa kiwanda cha kuzalisha dawa za kibaiolojia cha Tanzania Biotech Products Limited akizungumia miaka 10 ya kiwanda hicho kupitia kipindi cha cha
12/09/2025
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera, amefanya ziara ya kikazi katika miradi mikubwa ya kimkakati ya Liganga na Mchuchuma, inayosimamiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).
Katika ziara hiyo, Dkt. Serera aliambatana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa NDC, Dkt. Nicolaus Shombe, ambapo walipata fursa ya kujionea hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa miradi hiyo ya kimkakati yenye lengo la kuendeleza sekta ya viwanda nchini kupitia uchakataji wa chuma na makaa ya mawe.
Wakiwa wilayani Ludewa, wageni hao walipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Olivanus Thomas, ambaye aliwapongeza kwa kufuatilia kwa karibu maendeleo ya miradi hiyo na kusisitiza umuhimu wake katika kuleta fursa za ajira, kuongeza mapato ya Serikali na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa Ludewa na taifa kwa ujumla.
Ziara hiyo imetoa nafasi ya kujadili changamoto na fursa zilizopo katika utekelezaji wa miradi hiyo, sambamba na kuimarisha mshik**ano kati ya Serikali Kuu, NDC, na viongozi wa eneo husika ili kuhakikisha mradi huu wa kimkakati unatekelezwa kwa ufanisi na kuwanufaisha Watanzania.
05/09/2025
Tunawatakia Waislamu na Watanzania wote, Maulid Al Nabi njema.
Siku hii ikawe ya kheri na baraka tele.