Efatha Church Temeke

Efatha Church Temeke

Share

Efatha Church Temeke deals with the mission of healing and deliverance, containing 22 centers, under the Senior regional Pastor Ester Habakuki Hagai

this page is managed by Efatha ministry temeke, under Senior Regional Pastor Cecilia Mtunda Makundi, we intended to show how God fufill HIS promices to HIS people, basing on all the deads and events that are undertaken in all centres of Efatha Temeke, under control of ICT group of Efatha ministry Temeke, page lunchs all the events in image form and Videos, this is inorder to make all tongues, trib

01/06/2026

Hautabaki k**a ulivyokuwa katika msimu huu mpya. Roho wa Bwana atakuongoza, na kukupa hekima ili ushinde katika kila jambo.

Furahia na ushangilie wokovu wako! Badala ya huzuni, sasa ni majira ya kicheko, Mungu anaenda kufanya makuu katika maisha yako.

Umebarikiwa!


31/05/2026

"Thanks for Join Us"

Photos from Efatha Church Temeke's post 31/05/2026

MEZA YA BWANA

Mungu hadharau mwanzo mdogo, anza unapoanzia imani yako iwe k**a mbegu linda imani yako, ukilinda imani yako ndipo dhambi, magonjwa, shetani wachawi, njaa na hata dhiki zitakukimbia na ndipo utakapoona mema yakikujilia. Ayubu anasema utakusudia neno nao litatimia. Ukilinda imani yako isiyumbe hautasikia njaa wala kiu, maana yake mahitaji yako yatatimizwa.

Haya yote yatatokea kwako k**a utalinda imani yako. Tunapomega mkate na kunywa mvinyo, yale yaliyoshindikana yakawezekane, Biblia inasema “Imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo” mwana wa Mungu Neno hili litatimia kwako, hutaona kiu wala njaa maana mahitaji yako yatatimilizwa, unaenda kula na kunywa vile vitamanikavyo.

Biblia inasema Mungu ndiye uzima wako, baada ya kula na kunywa (meza ya Bwana) ule ugonjwa uliyokukandamiza utaondoka. Kwa mamlaka niliyonayo utaenda kutamka Neno leo na litakwenda kutimia, yule mgonjwa aliyekuwa kitandani kwamba ni mkubwa au mdogo anakwenda kuinuka, kwamba ulikuwa unaumwa na kansa, TB, presha, kisukari au aina yoyote ya ugonjwa leo huo ugonjwa umeondolea maana Bwana amesema amekuja ili sisi tuwe na uzima tele, leo unakwenda kuwa na uzima tele. K**a umekuja hapa ulikuwa na maswali yanayokusumbua umepata majibu yake. Mwanangu wacha ikawe hivyo kwako.

@ MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

Photos from Efatha Church Temeke's post 31/05/2026

MEZA YA BWANA

Yohana 6:33-35 “Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. Basi wakamwambia, Bwana, sikuzote utupe chakula hiki.”

Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.”

Yohana 1:1-5 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.”

Tunapokubaliana na neno tunakuwa tunapata uzima wa milele, tunaporuhusu Neno ndani yetu tunaruhusu Yesu akae ndani yetu, kwa maana Yesu ndiye uzima wetu. Tukikubali Neno tumemkubali Yesu, na hapo ndipo tunalinda imani yetu, ukiilinda imani yako itakupa kuponyeka, ukiamini kile unachokiamini mtu asikiondoe wala kukiharibu ndipo uponyaji unatokea kwako, Yusufu alilinda imani yake japokuwa alitupwa gereani lakini akaishia kuwa mtu mkuu, Daudi pia alilinda imani yake na akaishia kuwa mfalme. Imani ukiilinda unakuwa salama na kwako kunakuwa kwema.

Zaburi 128:1-4 “Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake, Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema…”

Yule amchaye Bwana atabarikiwa. Kumcha Bwana ni kulinda kile unachokiamini, unapolinda unachokiamini maisha yako yanaonekana yana mpangilio na ndipo Mungu anakufurahia, kwa maana unapolinda hicho unajiponya na mambo au ulimwengu huu na ndipo Mungu anakufurahia na kuruhusu mema yakujilie na kwako kunakuwa kwema.

Zaburi 126:6 “Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.”

Tunapolinda imani kuna magumu, machungu kudharauliwa na kusukumwa lakini usiangalie yale yanayoendelea bali angalia kile unachokiamini ili kikupe kile unachokitaka, hakikisha unalinda kile unachokiamini na ndipo kwako kutakuwa kwema na Mungu atakushangaza na kila mtu atakushangaa.

@ MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA

Photos from Efatha Church Temeke's post 31/05/2026

IBADA YA PAMOJA KANISA LA EFATHA MBAGALA | 31.05.2026

PICHA KATIKA MATUKIO

Photos from Efatha Church Temeke's post 31/05/2026

IBADA YA PAMOJA KANISA LA EFATHA MBAGALA | 31.05.2026

Matukio katika picha.

Photos from Efatha Church Temeke's post 31/05/2026

IBADA YA PAMOJA KANISA LA EFATHA MBAGALA | 31.05.2026

Zaburi 100:5
"Kwa kuwa BWANA ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi."

Photos from Efatha Church Temeke's post 31/05/2026

IBADA YA PAMOJA KANISA LA EFATHA MBAGALA | 31.05.2026

Zaburi 84:10
"Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu."

Karibu Nyumbani

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Mbagala
Dar Es Salaam
P.OBOX41587