26/07/2024
Shairika NA Dominic
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Shairika NA Dominic, Library, Bakwata, Dar es Salaam.
26/07/2024
09/09/2023
K**A TATIZO NI DINI
Kipi kwako sijasema, nijuze nikitamke,
Siku zazidi yoyoma, nataka nikwite mke,
Wanangu wakuite mama, na wewe uwaitike,
K**a tatizo ni dini, badili tuishi wote.
Sitoficha ninasema, hilo ujue bayana,
Kwangu ndiwe chanda chema, kati ya nilowaona,
Moyo wangu wauchoma, kwa sababu twakinzana,
K**a tatizo ni dini, badili tuishi wote.
Katika hili nakili, wapo wengi wasichana,
Wenye rangi ya asili, uzuri wao ni mwanana,
Uloniteka akili, ni wewetu we kimwana,
K**a tatizo ni dini, badili tuishi wote.
Salamu zangu fikisha, kwa baba yako na mama,
Unijulishe na kisha, nami nimjuze mama,
Ya kwamba yule Aisha, majibu kwao ni mema,
K**a tatizo ni dini, badili tuishi wote.
Naomba lako sikio, nisikilize nasema,
Nijapo kua mumeo, tusemezane kwa mema,
Mana watu wengi wao, pendo kwao lishazima,
K**a tatizo ni dini, badili tuishi wote.
16/04/2022
TUMEPATA TUMAINI
Mama,
Njo mwanangu keti chini, nikujuze yalojili,
Jambo hili si utani, limenipa raha kweli,
Tena liweke moyoni, lazima tufike mbali,
Tumepata tumaini, rais kutoa kauli.
Mtoto,
Jambo hilo jambo gani, mbna wafurahi mama,
Lilokujaa moyoni, ukanitana kusema,
Vipi hilo tumaini, laruhusu wakulima ?
Tumapata tumaini, rais kutoa kauli.
Mama,
La! Sio la wakulima, rais alilolisema,
Latuhusu kina mama, na binti zetu kusoma,
Kaitangaza kiama, kwa wanao kula njama,
Tumepata tumaini, rais kutoa kauli.
Mtoto,
Vipi liwe nyota njema, hasa kwenu kina mama,
Kusoma si tangu zama, maika ile ya nyuma ?
Wasemaje kina mama, kwani nyi hamkusoma. ?
Tumapata tumaini, rais kutoa kauli.
Mama,
Enzi zetu za ujana, binti hawana nafasi,
Kazi zilitubana, tena kwa faida hasi,
Walosoma ni mabwana, waliopewa nafasi,
Tumepata tumaini, rais kutoa kauli.
Mtoto,
Naomba nijuze vema, nikuelewe mwanao,
Usemapo hamkusoma, unanipa mshangao !!?
Mbona wapo kina mama, tena wengi wenye vyeo,
Tumepata tumaini, rais kutoa kauli.
Mama,
Mwanangu nenda kasome, ukikomboe kizazi,
Kiepushe na ukame, kikinge na wabazazi,
Mabinti zetu msome, siwe k**a chetu kizazi,
Tumepata tumaini, rais kutoa kauli.
Mtoto,
Mama nimekusikia, mwanao nakuahidi,
Nafasi nitatumia, na katu sitakaidi,
Masomo kuzingatia, nitatilia juhudi,
Tumepata tumaini, rais kutoa kauli.
MANENO YA WAHENGA
Waliyanena wahenga, maneno yenye busara,
Yakawakuta majanga, na nyingi sana hasara,
Wale walio yapinga, wa pwani hata bara,
Kwa kusema ni ujinga, na kuyaita uchwara.
Walisema chanda chema, chanda chema vikwa pete,
Ni ni neno lenye hekima, sio chai na mkate,
Bali yule mke mwema, mwenye kuomba upate,
Huku naye kijituma, asiwe nyumbani bwete.
Mtaka cha uvunguni, kitanda asiinue,
Akili mwake kichwani, ni vipi ajikwamue,
Afikwapo mitihani, tatizo alitatue,
Na tena awe makini, kesho lisijirudie.
Asofunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu,
Katika kila kaziye, mbele huona ukungu,
Na daima maishaye, hugubikwa na machungu,
Mtu huyo ni ambaye, asompendeza Mungu.
Wahenga hao husema, akiba ndo haiozi,
Wema afanyao mama, faidaye iko wazi,
Jinsi anavyo jinyima, japokua hana kazi,
Mtoto apate kusoma, na mwisho apate kazi.
D.D.Titus
Dar Es Salaam
@ 2019
TUSEME ASANTE MUNGU,
1. Wengi tulianza nao, na leo hawapo tena,
Sisemei wenye vyeo, pia na yao majina,
Ndugu zetu wengi wao, hao wametangulia,
Tuseme asante Mungu, kwa zawadi ya uzima.
2. Hazikosi changamoto, hilo linajulikana,
Ingawaje za mpito, kwa wazee na vijana,
Zilitupa tumbo joto, ilipokuja Corona,
Tuseme asante Mungu, kwa zawadi ya uzima.
3. Tazama barabarani, ajali zilotokea,
Na wagonjwa mawodini, vitanda wamelalia,
Mimi nawe tu nyumbani, kazi zinaendelea,
Tuseme asante Mungu, kwa zawadi ya uzima.
4. Jiulize ndugu yangu, wewe umempa nini ?
Mpaka haya machungu, yasikufike kwa nini ?
Tuungane ndugu zangu, kumshukuru manani,
Tuseme asante Mungu, kwa zawadi ya uzima.
5. Ndani ya mwaka mzima, ni mengi tumeyaona,
Wingi wa zake rehema, usiku hata mchana,
Baraka hakutunyima, kwetu amezimimina,
Tuseme asante Mungu, kwa zawadi ya uzima.
D.D.Titus
Wa Dominic
30/12/2021
07/12/2021
ZAMANI NA SASAHIVI.
Usipokua makini, huwezi jua undani,
Jambo hili si utani, ni gumu kulibaini,
Limewaweka mezani, wasomi na watu duni,
Kuzijua tofauti, zamani na sasahivi.
Kumbuka nyingi tafiti, hazikupata fumbuzi,
Ikawekwa mikakati, pia nayo hikukidhi,
Leo ni nyingi k**ati, changamoto kudhibiti,
Hizi ndizo tofauti, zamani na sasahivi.
Jambo walilobaini, kwamba hiki ndo kiini,
Kupoteza tamaduni, na kuenzi za kigeni,
Kwatuweka matatani, siri metoka mezani,
Hizi ndizo tofauti, zamani na sasahivi.
Zamani hapa mzizima, ndo jiji lilorindima,
Makao kwenda Dodoma, faraja kwa wakulima,
Zimewafika huduma, Kagera mpaka Ruvuma,
Hizi ndizo tofauti, zamani na sasahivi.
Mipaka mji husika, zamani linyanyasika,
Ulinzi kuwa wa shaka, si jambo kusimulika,
Leo ulinzi hakika, hilo liwezi pingika,
Hizi ndizo tofauti, zamani na sasahivi.
Mbuga k**a Serengeti, zamani zitamaniki,
Hazikuwepo nishati, na hilo halipingiki,
Baada ya karabati, pesa kede kwa malaki,
Hizi ndizo tofauti, zamani na sasahivi.
Mfumo wa kulipa kodi, zamani libisha hodi,
Zilipotea rekodi, zile za walipa kodi,
Na sasa elektroniki, taifa lizurumiki,
Hizi ndizo tofauti, zamani na sasahivi.
Tofauti ziko wazi, za sasa na zamani,
Zamani haya makazi, hayakwenda kwa ramani,
Hapo sijagusa kazi, ni wazi hazifanani,
Hizi ndizo tofauti, zamani na sasahivi.
@ 2013
01/10/2021
MWANANGU USIACHE MKE
Wito wako na mkeo, leo nimeuitika,
Na kesho kabla machweo, tanibidi kuondoka,
Maana shamba mazao, ulinzi waitajika,
Mwanangu siache mke, sababu ya kosa moja.
Kosa moja sio hoja, kaeni myamalize,
Shik**aneni pamoja, manani msimkwaze,
Mwanenu huyu mmoja, malezi msikatize,
Mwanangu siache mke, sababu ya kosa moja.
Kupiga sio kufunza, mke utamzeesha,
Utamfanya ajuza, mashavu kuporomosha,
Watakiwa kumtunza, kisha kumpendezesha,
Mwanangu siache mke, sababu ya kosa moja.
Tamaduni za kigeni, kuiga zitakuponza,
Zifuate za nyumbani, njema zilizo kukuza,
Mkeo muite ndani, sio sauti kupaza,
Mwanangu siache mke, sababu ya kosa moja,
Na mambo mema ya ndani, jirani hayamuhusu,
Tena kaeni makini, sijekua makasuku,
Ya ndani yawe ndani, nje waone mabusu,
Mwanangu siache mke, sababu ya kosa moja.
Mama yenu kijijini, hili limemshangaza,
Iweje huku mjini, ugomvi mwaukoleza,
Mmemtia huzuni, nashindwa kuwaeleza,
Mwanangu siache mke, sababu ya kosa moja.
Mke anabarakaze, vizuri ukimtunza,
Mkae akuliwaze, kazini wakikukwaza,
Kisha akubembeleze, mawazo kuyapoteza,
Mwanangu siache mke, sababu ya kosa moja.
MPENZI
Naijulikane kwamba, wewe ni wangu mpenzi,
Mwenye umbo nane namba, kipimwa yako saizi,
Simnene si mwembamba, dongo lako mfinyanzi,
Sitochoka kukupamba, kwa tungo nzuri na tenzi.
Hebu amini mpenzi, ya dhati niyasemayo,
Mwingine sitomuenzi, mpenzi tuliza moyo,
Wewe wangu toka enzi, nilokukabidhi moyo,
Tafadhari wangu mwenzi, kwako mimi sina choyo.
Na sipendi tuwe mbali, majukumu yalazimu,
Natamani kila hali, niipate yako tamu,
Sautiyo ya asili, ipoze zangu stimu,
Kuanzia kwenye mwili, hadi ndani kwenye damu.
Wazuri wapo wengi, wewe kwangu ni pekee,
Nimefika nchi nyingi, wewe bado u pekee,
Wapo wanunua rangi, eti mi niwachekee,
Wewe una sifa nyingi, na nyingine za pekee.
Kwako sina wasiwasi, kwenye joto nipepee,
Nijione mie bosi, na tajiri wa pekee,
Wasinitie mkosi, tena mbali wapotee,
Wale wachongao nyusi, kujiita mabebee.
Deo Titus
06/07/2021
HERI NA OLE WAO
Ni heri wale walio, faraja ya waliao,
Wawapao tegemeo, kufuta machozi yao,
Walio lao kimbilio, kwa yalio mbele yao,
Ni heri na ole wao, kwa haya wayafanyayo.
Ole wao wafanyao, kazi zisizo haliali,
Wawafanyao wenzao, daraja kupata mali,
Ni hakika mwisho wao, hautokua wa mbali,
Ni heri na ole wao, kwa haya wayafanyayo.
Ni heri yule Mwalimu, chimbuko la taaluma,
Aliye chanzo muhimu, katika zote huduma,
Maana pasipo Mwalimu, mambo huenda mrama,
Ni heri na ole wao, kwa haya wayafanyayo.
Ole wake yule mwana, alofunzwa na mamaye,
Kukua na kutukana, kutojua thamaniye,
Kumuona si wamana, kisa mali na kaziye,
Ni heri na ole wao, kwa haya wayafanyayo.
@
2017.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Website
Address
Bakwata
Dar Es Salaam
