01/06/2026
KATAVI
Pamoja Tujenge Viwanda.
SIDO was established as a parastatal organisation under Ministry of Trade, Industry and Marketing (now Ministry of Trade)
01/06/2026
KATAVI
Pamoja Tujenge Viwanda.
01/06/2026
DAR ES SALAAM
Karibu Tushiriki Pamoja.
31/05/2026
RUKWA
Kazi Inaendelea, Pamoja Tujenge Viwanda.
31/05/2026
ARUSHA
Pamoja Tujenge Viwanda.
Tunarithisha dhana ya viwanda vidogo kwa kizazi kijacho.
29/05/2026
DAR ES SALAAM
SIDO DAR NA CMT WAKUBALIANA KUWEKA MIKAKATI YA KUWAWEZESHA MAFUNDI
Tarehe 28 Mei 2026, SIDO Dar es Salaam ilifanya kikao kazi na uongozi wa Chama cha Mafundi Tanzania - CMT, wakiongozwa na Mwenyekiti Mhand. Mtendwa katikati pichani.
Agenda Kuu ya Kikao ilikuwa ni Kuweka mikakati ya pamoja ya kuwarasimisha mafundi na kuwajengea uwezo wa kitaalamu na kibiashara. Lengo ni kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ya Serikali na sekta binafsi.
Matokeo yanayotarajiwa baada ya kikao ni k**a ifuatavyo:
1. Kuongeza fursa za ajira kwa mafundi
2. Kuboresha ubora wa kazi na ufundi nchini
3. Kutoa ushindani kwa mafundi wa Kitanzania kwenye soko la kazi
Ushirikiano huu ni hatua muhimu ya kuhakikisha mafundi wetu wanapata nafasi, heshima na kipato kinachostahili.
Pamoja Tujenge Viwanda.
29/05/2026
MAFUNZO YA UTENGENEZAJI WA SABUNI YAMEKAMILIKA MKOANI SONGWE
Wajasiriamali wa Mkoa wa Songwe sasa wana ujuzi mpya!
Mafunzo ya utengenezaji wa sabuni za maji, sabuni za miche na bleach yamekamilika kwa mafanikio. Washiriki wamejipatia maarifa ya kutengeneza bidhaa bora, salama na zenye ubora wa kushindana sokoni.
Hatua inayofuata: Kutumia ujuzi huu kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo vya sabuni, kuinua kipato na kujiajiri wenyewe.
Hongera sana SIDO Songwe na wote mlioshiriki.
Anzisha Kiwanda na SIDO.
29/05/2026
VIWANDA VIPYA VYA CHAKULA VINAANZA PWANI!
Unataka kuanzisha au kuboresha uzalishaji wa bidhaa za chakula?
Kutana na Bi. Rachel - Mtaalamu wa usindikaji wa vyakula. Atakupa muongozo sahihi wa hatua kwa hatua ili uzalishe bidhaa bora, salama na zinazokidhi viwango vya soko.
Mada zinazofundishwa katika Mafunzo ya Usindikaji Vyakula, Mboga na Matunda ni:
1. Usindikaji wa vyakula mbalimbali
2. Ubora na usalama wa chakula
3. Ufungashaji na uthibiti wa ubora
4. Taratibu za kurasimisha bidhaa
Wasiliana nasi kwa namba 0766 311 320
Pata mafunzo na uanze kiwanda chako cha chakula ndani ya Mkoa wa Pwani.
Karibu Tukuhudumie.
29/05/2026
MBEYA
29/05/2026
SINGIDA
SIDO SINGIDA WAPATIWA ELIMU YA FEDHA NA UWEKEZAJI KWA WATUMISHI
Watumishi wa SIDO Mkoa wa Singida wamepatiwa Semina ya masuala ya fedha na uwekezaji iliyotolewa na Bi. Nyamwiza Kaiza kutoka NMB Benk.
Lengo la Semina husika ni kuwajengea uelewa wa usimamizi bora wa fedha binafsi, mbinu za uwekezaji, na huduma mbalimbali za kifedha zinazoweza kuboresha maisha yao.
Watumishi walipata nafasi ya kufahamu fursa zinazotolewa na NMB Benki kwa wafanyakazi, zikiwemo:
1. Mikopo nafuu
2. Akaunti maalum za wafanyakazi
3. Huduma za bima
Kwa upande wake, Bw. Melkiado January, Meneja wa SIDO Mkoa wa Singida, ameishukuru NMB Benki kwa semina yenye manufaa makubwa kwa watumishi. Pia amepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya SIDO na NMB.
SIDO KWA MAENDE
NJOMBE
SIDO NJOMBE YASHIRIKI UFUNGUZI WA KIWANDA CHA SAMADI MAKETE
Mhandisi wa SIDO Njombe, Andrew Masigo amehudhuria ufunguzi wa kiwanda cha kuzalisha samadi katika Wilaya ya Makete.
Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) linaendelea kutoa huduma za ushauri na mafunzo kwa wajasiriamali ili kukuza viwanda vidogo na kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini.
Bw. Aldo Sanga mmiliki wa kiwanda cha kuzalisha Samadi ya wanyama ni miongoni mwa wajasiriamali wanaonufaika na huduma za SIDO zilizotolewazo katika Wilaya ya Makete, Mkoani Njombe.
Samadi inayozalishwa ina umuhimu mkubwa katika:
a. Kuboresha rutuba ya udongo
b. Kuongeza uzalishaji wa mazao kwa njia rafiki kwa mazingira
c. Kupunguza matumizi ya mbolea za kemikali
SIDO itaendelea kushirikiana na wajasiriamali mbalimbali ili kukuza viwanda vidogo, kuchochea maendeleo ya uchumi na kuongeza ajira katika jamii hususan Vijana. SIDO ina ofisi katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
Pamoja Tujenge Viwanda, Karibu Tukuhudumie.
| Monday | 08:00 - 16:30 |
| Tuesday | 08:00 - 16:30 |
| Wednesday | 08:00 - 16:30 |
| Thursday | 08:00 - 16:30 |
| Friday | 08:00 - 16:30 |