14/08/2026
SABABU 5 KWANINI HUWEZI KUMBADILI MWANAUME AMBAYE HAJAOKOKA UNAYETAKA AKUOE NA UMBADILISHE
1. Umeanzisha kitu kipya nje ya NENO LA MUNGU
-Hatuwahubirii watu habari za Yesu kwa ajili ya KUSUDI la kuwaoa au kutuoa bali ili wasipotee bali WAWE NA UZIMA WA MILELE (Yohana 3:16-18)!
-Msingi wa wanaotaka kuoa au kuolewa kwenye mwili wa Kristo tayari umewekwa ya kwamba "usifungiwe nira na asiyeamini kwa jinsi isiyo sawasawa" ikiwemo kwa mfumo huo wa nitaoelewa naye nimgeuze (2Wakorintho 6:14)!
2. Jiambie ukweli, tangu mwaka umeanza nje ya huyo "asiyeokoka" unayetaka uolewe naye umbadilishe, NI WANAUME WANGAPI UMEWAHUBIRIA HABARI ZA YESU NA WAMEOKOKA, WAKASIMAMA NA WANAENDELEA MBELE NA MOTO WA MUNGU KANISANI?
-K**a huna wanaume ambao ni MAVUNO yako kwa Yesu kwa njia ya INJILI, kinachokupa UHAKIKA kwamba utamuokoa na kumgeuza "asiyeamini" ukiolewa naye ni kipi? Mbona unapima kina cha maji kwa miguu yote miwili, si kichaa hiki kimekupata? Jiambie ukweli, hutaweza, unachezea shilingi kwenye tundu la choo, ni MCHEZO HATARI huo!
-Unafikiri MWANAUME ambaye anajua tayari moyo wako haumchukulii k**a "mavuno kwa Yesu" bali "darling" au "babe" atakubali umuamulie misingi ya anayoyaamini?
Endelea kucheza k**ari hiyo halafu utakuja kuwasimulia wanao na wajukuu namna ULIVYOLIWA KEKUNDU!
3. Hadi unakutana naye, k**a hajaokoka, na k**a hajafika kanisani, na INJILI inavyohibiriwa kila mahali, si kwenye TV, si kwenye redio, si mitandaoni, si kwenye magari nakadhalika, UNAHISI WEWE MPENZI WAKE NDIYE UNA INJILI AMBAYO INACHOMA MOYO WA MTU NA KUMFANYA ASEME NIFANYE NINI NIPATE KUOKOKA? Acha utani mrembo, kichwa chako kina shida!
-Hapo ulipo hauhusiki na injili kokote, si mtandaoni, si ushuhudiaji mitaani, na unataka uugeuze moyo wa MWANAUME sio? Una utani wewe mdada!
4. Hivi unafahamu, kuna watu ambao piga ua garagaza, hawatakuja KUOKOKA na hawakuja kuingia uzimani ingawa Bwana Yesu keshawafanyia kila kitu... Unaweza kukuta mmoja wa hao watu walioshindikana ni huyo baharia unayetaka AKUOE UMBADILISHE...
Ikitokea ikawa hivyo, utaweza KUISHI KWENYE NDOA ya namna hiyo hadi KIFO au utatafuta vifungu kwamba ni mzinzi ili uachike na kuweka rekodi ya kuolewa zaidi ya mara moja?
Unajua nini? Pressure yako ya kuolewa si kubwa KULIKO hatari ya kuangukia kwenye mikono ya mnyang'anyi k**a mtu yule aliyekuwa akielekea Yerusalemu!
5. Anayewaokoa watu na dhambi zao ni Yesu Kristo tu na si NDOA (Mathayo 1:21)!
-Hakuna kokote maandiko yanasema uoe au uolewe na asiyeamini halafu utambadilisha wewe, bali kuna maelekezo kwamba IKITOKEA KATI YA WANANDOA WAWILI WALIOOANA KABLA YA KUMPOKEA YESU, NA MMOJA AKAIPATA NEEMA YA WOKOVU, HALAFU KULE KUOKOKA KWAKE KUSIMKERE WALA KUMKWAZA YULE MWENZA ASIYEOKOKA, BASI ASIMWACHE, AKOMAE NAYE NA MUNGU ATAFANYA MUUJIZA NAYE AIPATE NEEMA YA WOKOVU, hii si ya walio nje ya NDOA, ni ya waliokuwa tayari kwenye NDOA (1Wakorintho 7:12-15)!
SASA WEWE RUKARUKA UYAKANYAGE,
MBONA UTAIMBA HALLELUJAH PEKE YAKO,
TUTAKUWA TUMEKAA PALEEEE TUNAKUCHORA,
HATUINGILII MAJANGA YASIYOTUHUSU,
TUKIJIKAZA TUTAKUSENG'ENYA KWAMBA ULIACHA WOKOVU ILI UKAOLEWE NA UTAUMIA ZAIDI,
BINTI YANGU SUMU HAIJARIBIWI KWA KUIONJA!
Bishop Dickson Dickson Cornel Kabigumila
ABC GLOBAL DUNIANI