GPSA Tanzania

GPSA Tanzania

Share

Official Facebook Account of Government Procurement Services Agency of Tanzania

Photos from GPSA Tanzania's post 31/05/2026

GPSA YAFANYA USAFI WA MAZINGIRA YA OFISI KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI 2026

Kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kwa mwaka 2026, viongozi na watumishi wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) washiriki usafi wa mazingira kuzunguka Ofisi na vituo vyake siku ya Jumamosi tarehe 30/05/2026.

CPA Juliana Mero (Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani-GPSA) akizungumza kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu Prof. Geraldine Arbogast Rasheli kuwa Wakala unatambua umuhimu wa mazingira safi katika kujenga afya bora, kuongeza tija kazini na maendeleo endelevu, ambapo zoezi hili limefanyika katika mikoa yote Tanzania Bara.

CPA Juliana Mero ameongeza, " Kwa GPSA, maadhimisho ya siku ya mazingira duniani si tu fursa ya kukumbusha umuhimu wa kuhifadhi mazingira, bali pia mwito wa kuchukua hatua za vitendo zinazochangia kujenga mazingira safi, salama na endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho".

GPSA inajivunia mchango wake kiujumla katika utunzaji wa mazingira kupitia mfumo wa kidijitali wa utoaji wa huduma zake wa GIMIS ambapo umepelekea kupunguza matumizi makubwa ya karatasi katika Ununuzi wa Umma pamoja na Ununuzi wa bidhaa zisizochafua mazingira ili kuhakikisha fedha za umma zinachangia uchumi wa kijani (Green economy).

Aidha, Wakala unahamasisha matumizi ya nishati safi ya gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG-V) na umeme (EV) kwenye magari ya Serikali kwa ujenzi wa vituo vyake katika Mpango Mkakati wake 2026/27-2030/31).

Siku ya kilele ya maadhimisho ya Mazingira Duniani (World Environment Day) ni Juni 5, 2026, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu 2026 ni "Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania".

27/05/2026

Photos from GPSA Tanzania's post 14/05/2026

KAIMU AFISA MTENDAJI MKUU GPSA AFUNGUA MAFUNZO YA UKAGUZI WA NDANI WA MFUMO WA UDHIBITI UBORA (ISO 9001:2015) KWA MAAFISA (CHAMPIONS) WA GPSA WA MIKOA YOTE

​Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Bw. Mwakiselu Mwambange (Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji) amefungua rasmi mafunzo maalum ya siku tano (yaliyoanza tarehe 11-15 Mei,2026) kwa maafisa wa GPSA kutoka mikoa yote Tanzania Bara, yanayolenga kuwajengea uwezo wa kuwa Wakaguzi wa Ndani (Internal Auditors) wa mfumo wa Udhibiti wa Ubora wa Kimataifa (ISO 9001:2015) yanayofanyika katika ukumbi wa NSSF Mkoani Morogoro jana Jumanne tarehe 13/05/2026.

​Mafunzo haya ni sehemu ya mkakati wa Wakala kuhakikisha kuwa huduma zake zinazotolewa kwa taasisi za Serikali zinakidhi vigezo vya ubora wa kimataifa na kuleta tija katika matumizi ya fedha za umma.

Mafunzo haya yanatolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na amewaasa washiriki wote kuwa chachu ya mabadiliko na kuleta matokeo endelevu yatakayowezesha GPSA kushindana Kimataifa.

Naye Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini Bw. Salum Masenga ametoa shukrani za dhati kwa Afisa Mtendaji Mkuu Prof. Geraldine Arbogast Rasheli kwa niaba ya champions wa ISO kwa maono yake na uwezeshaji unaowezesha kazi ya kuiwezesha Wakala kupata cheti cha ithibati wa ubora wa kimataifa (ISO certification) kufanikiwa.

Aidha ISO itaiwezesha Wakala kuboresha huduma zake na hivyo kuleta tija katika Ununuzi wa Umma kwa kuwa GPSA ndiye mnunuzi Mkuu wa Umma.

Photos from GPSA Tanzania's post 14/05/2026

MKUU WA MKOA WA SIMIYU ATEMBELEA OFISI YA WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI (GPSA) SIMIYU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha atembelea Ofisi ya Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) iliyopo mtaa wa Nyaumata katika wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu jana Jumatano tarehe 13 Mei, 2026 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea Taasisi za Serikali zilizoko Mkoa wa Simiyu.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mhe.Macha kutembelea ofisi za GPSA tangu awe Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, na amepokewa na Kaimu meneja GPSA-Simiyu Bi. Wilfrida Maucky. Mhe. Macha ametoa pongezi kwa Afisa Mtendaji Mkuu GPSA Prof. Geraldine Arbogast Rasheli kwa kazi nzuri na maboresho mbalimbali ya GPSA, huku akiwaasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma.

Photos from GPSA Tanzania's post 02/05/2026

MEI MOSI 2026: GPSA YAADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) waungana na wafanyakazi wote nchini Tanzania kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), siku ya tarehe 1 Mei, 2026 ambapo Kitaifa imefanyika Mkoani Njombe na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika maadhimisho haya, Wakala unajivunia kuwa Taasisi ya kimkakati wa ununuzi wa Umma inayounganisha wadau ambao ni wazabuni na wazalishaji wakubwa pamoja na Taasisi za Serikali katika kupata Vifaa na Huduma Mtambuka ikiwemo vifaa vya ofisi, mafuta,magari pamoja na ugomboaji na uondoshaji mizigo.

Aidha, Wakala umefanya maboresho makubwa katika utoaji wa huduma zake kidijitali na hivyo kuwezesha wateja wetu kupata vifaa na huduma kwa urahisi na kwa thamani halisi ya fedha.

Wakala unashiriki maadhimisho haya Kitaifa Mkoani Njombe, na pia katika Mikoa yote Tanzania Bara.

Wakala unajivunia wafanyakazi wake katika ofisi na vituo vyote katika Mikoa yote kwa uchapaji kazi, weledi na uadilifu wao.

Maadhimisho ya Mei Mosi hufanyika kila mwaka duniani kote k**a jukwaa la kutambua mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii pamoja na kuhimiza mazingira bora na salama ya kazi.

Kaulimbiu ya Mei Mosi 2026 ni “Kazi zenye staha ni nguzo imara kwa maendeleo endelevu katika utekelezaji wa Dira 2050”.

01/05/2026

30/04/2026

Hongera Joseph Kayombo kwa kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).

Photos from GPSA Tanzania's post 30/04/2026

GPSA YASHIRIKI SIKU YA MWANAMKE NA KAFITI JIJINI MWANZA 2026

Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) yashiriki katika siku ya Mwanamke na Kafiti siku ya Jumamosi tarehe 29/04/2026 jijini Mwanza ambapo zaidi ya watu 1,000 wameshiriki ikiwemo makundi maalum wakiongozwa na wanawake.

Mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ambaye amemwakilisha Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt Dorothy Gwajima.

Wakala umetoa elimu kuhusu huduma inazotoa, pamoja na fursa kwa makundi maalum ikiwa ni utekelezaji wa takwa la la Kisheria la kutenga asilimia 30 ya bajeti ya ununuzi kwa ajili ya makundi maalum (Wanawake, Vijana, Wenye Ulemavu na Wazee).

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Off Nyerere Road, Keko Mwanga
Dar Es Salaam
9150

Opening Hours

Monday 08:00 - 15:30
Tuesday 08:00 - 15:30
Wednesday 08:00 - 15:30
Thursday 08:00 - 15:30
Friday 08:00 - 15:30