27/05/2026
COSTECH inawatakia EID - AL - ADHA MUBARAK 🌙🕌♥️
page of Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) | Get update of whats Happening in Tanzania Research,Technology and Innovation.
27/05/2026
COSTECH inawatakia EID - AL - ADHA MUBARAK 🌙🕌♥️
26/05/2026
KUIMARISHA UBUNIFU NA USIMAMIZI WA HAKI MILIKI KANDA YA KASKAZINI
Ili kukuza uwezo wa taasisi zetu katika kuendeleza ubunifu na kusimamia Haki Miliki (IP) kwa tija, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeandaa mafunzo ya kujenga uwezo kwa taasisi 12 za Utafiti na Maendeleo (R&D) pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu (HL) kutoka mikoa ya Arusha, Tanga na Kilimanjaro kuanzia tarehe 18 hadi 22 Mei, 2026 katika Chuo cha Uhasibu jijini Arusha.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Dkt. Judith Kadege kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu na Muwezeshaji wa mafunzo hayo alikuwa Prof. Saudin Mwakaje.
Mafunzo haya yametoa fursa ya Kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa Haki Miliki, ubunifu na uhamishaji wa teknolojia, Kujenga uwezo wa wataalamu katika utafutaji na uandishi wa hataza (patent search & drafting) pamoja na kukuza ushirikiano kati ya vyuo vikuu, taasisi za utafiti, sekta binafsi na Serikali kwa ajili ya kuharakisha biashara na matumizi ya matokeo ya tafiti za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STI).
Kupitia vikao hivi, viongozi wa taasisi wameonyesha dhamira ya kuwekeza katika usimamizi wa Haki Miliki, kukuza biashara za ubunifu na kuimarisha mifumo ya ulinzi wa mali bunifu ndani ya taasisi zao. Taasisi zilizoshiriki ni CAMARTEC, TEMDO, TPHPA, KCMUCo, KCRI, MUCO, NM-AIST, TAWIRI, TARI-SELIAN, TACRI NIMR-TANGA, na SIDO.
Matokeo yanayotarajiwa kuongezeka kwa ubunifu unaolindwa kisheria, ushirikiano thabiti wa kitaasisi, na ongezeko la maombi ya hataza nchini.
07/05/2026
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) Prof.Adolf Mkenda, leo tarehe 07 Mei, 2026 amewasilisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara Bungeni jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara wakifuatilia Bajeti hiyo miongoni mwao ni Prof. Carolyne Nombo, Katibu Mkuu WyEST, Naibu Katibu Mkuu WyEST Prof. Daniel Mushi na Dkt. Amos Nungu Mkurugenzi Mkuu ,Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
Kuelekea Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia tarehe 7 - 8 Mei,2026
04/05/2026
01/05/2026
Heri ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi
26/04/2026
Heri ya Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano
05/04/2026
Heri ya Sikukuu ya Pasaka
🐰
| Monday | 09:00 - 15:30 |
| Tuesday | 07:30 - 15:30 |
| Wednesday | 07:30 - 15:30 |
| Thursday | 07:30 - 15:30 |
| Friday | 07:30 - 15:30 |