Vijana watakiwa kutumia fursa ya ufugaji wa Nyuki huku TFS wakipongezwa kwa kuendelea kutoa Elimu na kuboresha Mazingira ya uchakataji wa Mazao ya Nyuki
Tanzania Forest Services Agency
We conserve and sustainably supply quality forest and bee products and services in Tanzania.
TFS has been given the mandate for the management of national forest reserves (natural and plantations), bee reserves and forest and bee resources on general lands. TFS as an Executive Agency will enhance the management and conservation of forest and bee resources for sustainable supply of quality forest and bee products and services. The Forest and Beekeeping Division will remain with the respons
Kuna maeneo ambayo lazima uyatembelee mwenyewe ili uyaelewe, na Magamba Nature Forest Reserve ni moja ya maeneo hayo.
Kupitia programu ya World Vision Tanzania, vijana kutoka Pangani, Mkinga, Kilindi na Handeni walipata fursa ya kujifunza uhifadhi wa mazingira kwa vitendo huku wakitembelea vivutio vya kipekee vya Magamba.
Waliondoka na maarifa mapya, kumbukumbu zisizosahaulika, na moyo wa kuwa mabalozi wa uhifadhi wa mazingira.
Karibu Magamba Nature Forest Reserve mahali ambapo asili inasimulia hadithi yake yenyewe.
🎥
PUGU KAZIMZUMBWI: Hazina ya Utalii, Historia na Bioanuai!
Wahifadhi kutoka Shamba la Miti Sao Hill wametembelea Hifadhi ya Msitu wa Asili ya Pugu Kazimzumbwi kujifunza mbinu za uhifadhi, usimamizi wa bioanuai na maendeleo ya utalii wa ikolojia.
Ikiwa karibu na Jiji la Dar es Salaam, Pugu Kazimzumbwi imeendelea kuwa kivutio cha kipekee kinachounganisha uhifadhi wa mazingira, historia na utalii endelevu kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo.
Je, umeshatembelea hazina hii ya asili?
Pia, usisahau kupigia kura Pugu Kazimzumbwi Nature Forest Reserve na Amani Nature Forest Reserve katika Tuzo za Kimataifa za Utalii.
30/05/2026
PUGU KAZIMZUMBWI: HAZINA YA UTALII INAYOHIFADHI HISTORIA NA BIOANUAI
Wahifadhi wa Sao Hill wavutiwa na mafanikio ya utalii ikolojia, watakiwa kuhamasisha kura za Tuzo za Kimataifa za Utalii
Na Mwandishi Wetu, Pwani
Hifadhi ya Msitu wa Asili ya Pugu Kazimzumbwi mkoani Pwani imeendelea kujidhihirisha kuwa moja ya hazina kubwa za utalii wa ikolojia nchini baada ya kuvutia wahifadhi kutoka Shamba la Miti Sao Hill waliotembelea eneo hilo kujifunza mbinu za uhifadhi, usimamizi wa bioanuai na maendeleo ya utalii endelevu.
Ziara hiyo imekuja wakati Tanzania ikiendelea kuimarisha juhudi za kuhifadhi rasilimali za misitu na kuendeleza utalii wa asili k**a sehemu ya kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa, huku Pugu Kazimzumbwi ikitajwa kuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kuhifadhi urithi wa kihistoria na mazingira ya kipekee karibu na Jiji la Dar es Salaam.
Wakati wa ziara hiyo leo, wahifadhi hao walitembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana ndani ya hifadhi hiyo ikiwemo misitu ya asili yenye bioanuai adimu, njia za utalii wa kutembea msituni, maeneo ya kihistoria pamoja na vivutio vya kiikolojia vinavyovutia watalii wa ndani na nje ya nchi.
Maofisa wa hifadhi hiyo waliwaeleza wageni hao kuhusu hatua zinazochukuliwa kulinda mazingira, kudhibiti shughuli zinazohatarisha misitu na kuendeleza utalii wa ikolojia unaochochea maendeleo ya jamii na kuongeza mapato ya taifa bila kuathiri mfumo wa ikolojia.
Akizungumza baada ya kutembelea vivutio hivyo, Kiongozi wa Msafara huo, CO I Donald Makupa, alisema uzoefu walioupata katika Hifadhi ya Msitu wa Asili ya Pugu Kazimzumbwi utakuwa chachu ya kuboresha mikakati ya uhifadhi katika maeneo wanayoyasimamia.
“Tumeshuhudia namna ambavyo uhifadhi wa misitu unaweza kwenda sambamba na maendeleo ya utalii. Maarifa haya yatatusaidia kuimarisha usimamizi wa rasilimali za misitu na kuongeza thamani ya maeneo yetu ya uhifadhi,” alisema Makupa.
Aliongeza kuwa ushirikiano na kubadilishana uzoefu kati ya taasisi na maeneo mbalimbali ya uhifadhi ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha sekta ya misitu na utalii inaendelea kukua kwa manufaa ya taifa.
29/05/2026
KAMISHNA WA UHIFADHI TFS ASHIRIKI KIKAO CHA RAIS SAMIA KUPOKEA TAARIFA YA SENSA YA WANYAMAPORI NCHINI
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo leo Mei 29, 2026 ameshiriki kikao cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan cha kupokea Taarifa ya Sensa ya Wanyamapori iliyofanyika nchini kote kwa mwaka 2024/2025.
Taarifa hiyo imewasilishwa Ikulu jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (MB) kupitia Tanzania Wildlife Research Institute.
Kikao hicho kimewakutanisha viongozi na watendaji mbalimbali wa sekta ya uhifadhi na maliasili nchini kwa lengo la kupokea tathmini ya hali ya wanyamapori, mafanikio ya juhudi za uhifadhi pamoja na mwelekeo wa usimamizi endelevu wa rasilimali za asili nchini.
TFS Shinyanga inakukaribisha kwenye UZINDUZI RASMI wa Lubaga Forest Ecotourism Centre; eneo jipya la kipekee la utalii ikolojia lililopo katikati ya uzuri wa asili wa msitu wa Lubaga.
Video hii inakupeleka moja kwa moja kwenye mandhari ya kuvutia, maeneo ya kupumzikia, vibanda vya asili, sehemu za kupiga picha, utalii wa baiskeli na burudani mbalimbali zitakazopatikana ndani ya kituo hiki kipya cha utalii.
Karibu tushuhudie mwanzo mpya wa utalii wa mazingira Shinyanga.
📍 Lubaga Forest – TFS (Msitu wa Hashi)
🗓 27 Juni, 2026
27/05/2026
DONORS IMPRESSED BY PROGRESS OF MIOMBO FOREST MANAGEMENT PROJECT
By Our Correspondent
A delegation of development partners and donors supporting the Participatory Miombo Forest Management Project, including the Food and Agriculture Organization of the United Nations (FAO), the Global Environment Facility (GEF) and the Vice President’s Office – Division of Environment, has toured project sites to assess implementation progress.
During the visit, the delegation inspected newly constructed facilities, the distribution of modern beehives to local communities and the rollout of energy-efficient cooking stoves aimed at reducing dependence on firewood and charcoal.
Project officials said the initiative seeks to curb land degradation, strengthen sustainable management of Miombo forests and improve livelihoods through environmentally friendly economic activities, particularly beekeeping and forest-based enterprises.
The delegation also visited restored landscape areas and community projects benefiting residents through participatory forest management initiatives.
Officials noted that the five-year project aims to reverse environmental degradation and biodiversity loss while supporting social and economic development in communities surrounding Miombo forests.
The donors expressed satisfaction with the progress achieved so far, describing the project as a strong example of successful collaboration between government institutions, international organisations and local communities.
The project is being implemented by the Tanzania Forest Services Agency (TFS) in partnership with FAO through funding from GEF, with support from various environmental and development stakeholders.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
P. O. Box, Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
40832
