Bodi ya Filamu Tanzania

Bodi ya Filamu Tanzania

Share

Huu ni ukarasa rasmi wa Bodi ya Filamu Tanzania.

Kupitia ukurasa huu unaweza kupata habari na picha za matukio mbalimbali ya Bodi ya Filamu Tanzania, pia kupitia ukurasa huu unaweza kuwasilisha maoni, maswali, hoja na mapendekezo yako. Bodi ya Filamu Tanzania ni taasisi ya Serikali yenye dhamana kusimamia maendeleo ya sekta ya filamu nchini Tanzania.

25/01/2019

Tanzia: Nguli wa Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini Bi. Salome Nonge maarufu kwa jina la Mama Abduli amefariki dunia leo Tarehe 25 Januari, 2019 akiwa nyumbani kwake Mburahati jijini Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa ini.

11/01/2019

Tunapongeza jitihada chanya za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anazozionesha katika kukuza na kuendeleza uchumi wa Taifa letu kwa kufanikisha ununuzi wa ndege hii yenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 160. Hongera Mhe. Rais kwa kuudhihirishia Ulimwengu Uwezo wa Tanzania ambapo kwa pamoja tunasema "Tanzania Roho Ya Afrika, Anga Linashangilia"

Kununuliwa kwa Ndege hii kutafungua fursa nyingi za kiuchumi nchini kupitia Sekta mbalimbali k**a Usafirishaji na Uchukuzi, Utalii, Biashara, Filamu na zaidi kuimarisha azma ya kufikia uchumi wa Viwanda.

Aidha kupitia uwekezaji huu utarahisisha Mawasiliano na Uchukuzi kwa kuruhusu Watendaji katika Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza kwa kutembelea Tanzania na kufanya kazi kwa wakati kutoka eneo moja kwenda lingine kutokana na uhakika wa usafiri bora wa anga.

Photos from Bodi ya Filamu Tanzania's post 02/10/2017

Bodi ya Filamu Tanzania imetunukiwa cheti cha udhamini kwenye kilele cha 36 cha Tamasha la Kimataifa la Utamaduni na Sanaa Bagamoyo. Mgeni rasmi kwenye kilele hicho Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson alimkabidhi Katibu Mtendaji wa kwa niaba ya TaSUBA

20/07/2017

Mwanafamilia mpya kwenye ukurasa wetu karibun sana. Kupitia ukurasa huu utapata taairfa mbalimbali zinazohusu Bodi ya Filamu Tanzania na sekta ya filamu nchini Tanzania.

Bodi ya Filamu Tanzania Huu ni ukarasa rasmi wa Bodi ya Filamu Tanzania. Kupitia ukurasa huu unaweza kupata habari na picha za matukio mbalimbali ya Bodi ya Filamu Tanzania, pia kupitia ukurasa huu unaweza kuwasilisha maoni, maswali, hoja na mapendekezo yako.

28/06/2017

Wana familia wapya kwenye familia yetu kubwa ya Bodi ya Filamu Tanzania tunawakaribisha. Mjisikie mko nyumbani. Tuendelee kupashana habari na kufungua fursa zinazopatikana kwenye tasnia ya filamu nchini Tanzania.

Bodi ya Filamu Tanzania Huu ni ukarasa rasmi wa Bodi ya Filamu Tanzania. Kupitia ukurasa huu unaweza kupata habari na picha za matukio mbalimbali ya Bodi ya Filamu Tanzania, pia kupitia ukurasa huu unaweza kuwasilisha maoni, maswali, hoja na mapendekezo yako.

Photos from Tanzania Film Board's post 23/06/2017
Photos from Bodi ya Filamu Tanzania's post 09/06/2017

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fissoo amemtembelea na kufanya mazungumzo na Naibu Balozi wa China ofisi kwake leo. Kwenye mazungumzo hayo Ubalozi wa China umeonyesha nia ya kushirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania kuongeza masoko ya filamu za Tanzania nchini China, kushirikiana kutengeneza filamu, kubadilishana uzoefu na kutoa nafasi za mafunzo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya filamu nchini

Photos 01/06/2017

VIJANA WAPENDA FILAMU JITOKEZENI KWA WINGI

29/05/2017
25/04/2017

Utambulisho rasmi kwa yoyote anaefanya biashara ya filamu nchini ni kitambulisho, gharama yake ni sh 10,000/ kwa mwaka au sh 26/ kwa siku. Tafadhali fika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania kujiipatia kitambulisho chako

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


Samora Machel
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 09:00 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30