01/06/2026
Mhe. Reuben Nhamanilo Kwagilwa (Mb), Naibu Waziri (Muungano na Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), ametembelea banda la LATRA Juni 01, 2026 lililopo kwenye Maonesho ya Wiki ya Mazingira na kuelezwa shughuli zinazotekelezwa na LATRA.
Akiwa katika banda hilo Mhe. Kwagilwa (Mb) ameipongeza LATRA kwa juhudi za kudhibiti huduma za usafiri ardhini kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira kwenye vyombo vya usafiri na kuhamasisha matumizi ya Nishati safi kwa magari ya abiria.
Maonesho hayo yenye kaulimbiu isemayo Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania yanafanyika Juni 01 hadi 05, 2026 viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
31/05/2026
Wanasheria watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) wameshiriki mbio za pole pole - Wakili Marathon zilizoandaliwa na Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) Mei 31, 2026, uwanja wa Jamhuri, Dodoma
Mbio hizo zenye kaulimbiu “Huduma za Kisheria karibu zaidi na Watanzania” zimeongozwa na Mhe. Zainab Katimba (Mb), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.
22/05/2026
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeendesha kikao cha mafunzo kwa Mawakala wanaotoa leseni za usafirishaji kwa niaba ya LATRA kwa pikipiki za magurudumu mawili na matatu (Bodaboda na Bajaji).
Mafunzo hayo yametolewa Mei 21, 2026 ofisi za LATRA Mkoa wa Dar es Salaam na kuendeshwa na Bw. Patel Ngereza, kaimu Meneja leseni Usafiri wa Barabara LATRA na kuhudhuriwa na jumla ya kampuni 23 za Mawakala na baadhi ya maafisa wa LATRA.
Mafunzo hayo yamelenga kuwaelimisha mawakala hao namna bora ya kutekeleza majukumu yao, kuepukana na vitemdo vya Rushwa, na kuzingatia huduma bora muda wote wanapotoa huduma kwa niaba ya Mamlaka.
15/05/2026
Mha. Hanya Mbawala Mkurugenzi Udhibiti Reli (LATRA) ametoa wasilisho kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani Zanzibar (ZARTSA) wakati wa ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu iliyofanyika katika Ofisi za LATRA Makao Makuu, Mei 15, 2026 jijini Dodoma.