📌SAMIA KALAMU AWARDS 2026🔥🖊️
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Peter Mwasalyanda akizungumza na Waandishi wa Habari, kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi wa Samia Kalamu Awards 2026, tarehe 31 Mei, 2026 katika ofisi za TCRA jijini Dar es Saalam.
Mkurugenzi kuu ametoa wito kwa washiriki wote wenye sifa za kushiriki kuchangamkia fursa hii ya kujipima na alitoa wito kupata maelezo zaidi kupitia tovuti ya https://samiaawards.tz/.
Unaweza kufuatilia yaliyojiri kwenye mkutano huo kwenye chaneli ya YouTube ya TCRA au kupitia kiunganishi hiki https://www.youtube.com/watch?v=Av1-vFFp6w0&t=500s
Tanzania Communications Regulatory Authority
#NiRahisiSana kuwa Salama Mtandaoni!! It merged the former Tanzania Communications Commission and the Tanzania Broadcasting Commission.
The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), established by the TCRA Act no. 12 of 2003 is an independent Authority for the Postal, Broadcasting and Electronic communications industries in the United Republic of Tanzania. Its role include licensing and regulating the Postal services, Broadcasting services and Electronic Communications sectors in the United Republic of Tanzania.
01/06/2026
📌Idadi ya laini za simu kwa (P2P) kwa jinsia
Ripoti ya hali ya sekta ya Mawasiliano robo mwaka inayoishia Machi 2026 inaonesha umilikiwa wa laini za simu kwa jinsia umeongezeka kwa kiwango kinachofanana cha 4.65% ambapo wanaume wanaomiliki laini za simu ni milioni 56,912,362 kutoka 54,382,299 ya mwezi desemba 2025 huku wanawake wakiwa milioni 53,812,076 kutoka idadi ya 52,812,076 mwezi desemba 2025.
Umiliki wa laini za simu umekuwa msaada kwa kurahisisha shughuli za watumiaji wa huduma za mawasiliano kwaajili ya kukuza biashara na kuwezesha ukuaji wa sekta nyingine k**a afya, elimu na kilimo.
Tembelea tovuti ya TCRA (www.tcra.go.tz), au kupitia kiunganisho https://bit.ly/4nepmJM au skani kodi ya QR iliyopo kwenye bango ilikupitia ripoti kamili ya takwimu ya sekta ya Mawasiliano (Januari - Machi 2026).
Nakala kwa Lugha ya Kingereza (English version): https://bit.ly/4n8fAsq
📌SAMIA KALAMU AWARDS 2026🔥🖊️
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Peter Mwasalyanda akizungumza na Waandishi wa Habari, kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi wa Samia Kalamu Awards 2026, tarehe 31 Mei, 2026 katika ofisi za TCRA jijini Dar es Saalam.
Mkutano huo umefungua rasmi jukwaa kwa wanahabari kujisajili na kuwasilisha kazi zao ili kushiriki tuzo za Uandishi wa Habari na Makala za Maendeleo (Samia Kalamu Awards - SKA) 2026 zikiwa na lengo la kuendelea kuhamasisha uzalishaji wa maudhui yenye ubora yanayochangia maendeleo ya Taifa.
Unaweza kufuatilia yaliyojiri kwenye mkutano huo kwenye chaneli ya YouTube ya TCRA au kupitia kiunganishi hiki https://www.youtube.com/watch?v=Av1-vFFp6w0&t=500s
📌SAMIA KALAMU AWARDS 2026🔥🖊️
Tembelea samiaawards.tz kufahamu zaidi kuhusu makundi ya Tuzo na vigezo vya jumla vya ushiriki wa Tuzo za Waandishi wa Habari za Maendeleo (Samia Kalamu Awards - SKA) 2026.
📌SAMIA KALAMU AWARDS 2026🔥🖊️
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Peter Mwasalyanda akizungumza na Waandishi wa Habari, kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi wa Samia Kalamu Awards 2026, tarehe 31 Mei, 2026 katika ofisi za TCRA jijini Dar es Saalam.
Mkutano huo umefungua rasmi jukwaa kwa wanahabari kujisajili na kuwasilisha kazi zao ili kushiriki tuzo za Uandishi wa Habari na Makala za Maendeleo (Samia Kalamu Awards - SKA) 2026 zikiwa na lengo la kuendelea kuhamasisha uzalishaji wa maudhui yenye ubora yanayochangia maendeleo ya Taifa.
Unaweza kufuatilia yaliyojiri kwenye mkutano huo kwenye chaneli ya YouTube ya TCRA au kupitia kiunganishi hiki https://www.youtube.com/watch?v=Av1-vFFp6w0&t=500s
31/05/2026
📌MBEYA EXPO 2026
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya, Bi. Erica E. Yegella, ametembelea banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika Maonesho ya 4 ya Mbeya Expo 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Uhindini Jijini Mbeya.
Bi. Yegella alipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na TCRA pamoja na elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi na salama ya huduma za mawasiliano, usalama mtandaoni na fursa zinazopatikana kupitia teknolojia za kidijiti.
Akiwa katika banda hilo, Bi. Yegella amepongeza juhudi za TCRA za kuendelea kuwafikia wananchi kwa elimu ya mawasiliano na ameeleza dhamira yake ya kuhamasisha na kuleta vikundi mbalimbali vya vijana, wanawake na wajasiriamali kutembelea banda la TCRA ili kujifunza namna ya kutumia huduma za mawasiliano na teknolojia za kidijiti kujiletea maendeleo.
Aidha, amesema elimu inayotolewa na TCRA inaendana na kampeni yake ya “Fursa Sana”, inayolenga kuwawezesha wananchi kutambua na kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii zilizopo katika mazingira yao, hususan kupitia matumizi ya teknolojia na majukwaa ya kidijiti.
TCRA inaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho ya Mbeya Expo 2026 kuhusu matumizi salama ya mawasiliano, usajili wa majina ya tovuti za .tz, usalama mtandaoni na fursa za uchumi wa kidijiti.
31/05/2026
📌MBEYA EXPO 2026
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, ametembelea banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
katika Maonesho ya 4 ya Mbeya Expo 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Uhindini Jijini Mbeya.
Mhe. Mahundi alipata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na TCRA pamoja na elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu matumizi salama ya mawasiliano, usalama mtandaoni na fursa zinazopatikana kupitia teknolojia za kidijiti.
Mhe. Mahundi amepongeza utendaji kazi wa TCRA katika kusimamia sekta ya mawasiliano nchini na juhudi zake za kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu fursa za kiuchumi, kijamii na kielimu zinazopatikana kupitia mitandao na teknolojia za kidijiti.
TCRA inaendelea kushiriki Maonesho ya Mbeya Expo 2026 kwa lengo la kuhamasisha matumizi sahihi ya huduma za mawasiliano na kuwawezesha wananchi kunufaika na fursa za uchumi wa kidijiti.
31/05/2026
📌SAMIA KALAMU AWARDS 2026 YAZINDULIWA RASMI
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) zimeanza maandalizi ya Tuzo za Uandishi wa Habari na Makala za Maendeleo (Samia Kalamu Awards - SKA) 2026 zikiwa na lengo la kuendelea kuhamasisha uzalishaji wa maudhui yenye ubora yanayochangia maendeleo ya Taifa.
Akizungumza Jumapili tarehe 31 Mei, 2026 jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa mchakato wa kupokea kazi za kushindanishwa, Mwenyekiti wa SKA na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Peter Mwasalyanda, amesema SKA ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuendelea kutambua mchango wa Waandishi wa Habari za maendeleo nchini.
Amesema tuzo hizo zinalenga kutambua, kuthamini na kuhamasisha uzalishaji wa maudhui ya ndani yenye ubora yanayochangia kuelimisha, kuhabarisha na kuburudisha, huku yakiimarisha taswira chanya ya Taifa kupitia habari za maendeleo.
Mwasalyanda amesema katika awamu ya kwanza ya tuzo hizo kulikuwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa sekta ya habari wakiwemo taasisi za habari, Waandishi wa Habari binafsi, watengenezaji wa maudhui mtandaoni na Maafisa Habari wa Serikali.
Taarifa zaidi kuhusu SKA 2026 zinapatikana kwenye tovuti ya samiaawards.tz au kupitia kiunganishi hiki https://samiaawards.tz/
31/05/2026
📌SAMIA KALAMU AWARDS 2026📌
Fuatilia mubashara Mkutano na Waandishi wa Habari unaofanyika ofisi za TCRA jijini Dar es Salaam kupitia chaneli ya YouTube ya au bofya kiunganishi hiki 👉🏾
https://youtube.com/live/Av1-vFFp6w0?feature=share
📌FURSA SANA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaendelea kusisitiza jamii kuchangamkia fursa zilizopo mtandaoni kwenye zama hizi za kidijiti na kuzingatia matumizi sahihi na salama ya huduma na bidhaa za mawasiliano.
TCRA inatoa wito kwa jamii kuzichangamkia fursa k**a vile kutangaza biashara kupitia mitandao, kupata elimu, kuongeza ujuzi, kutafuta ajira, kutengeneza mtandao (networking), pamoja na kuonesha vipaji vinavyoweza kuwa vyanzo vya ajira ya kudumu, na fursa nyingine nyingi.
MUHIMU
📌Mawasiliano baina ya mtoa huduma na mtumiaji wa huduma za mawasiliano ni kupitia namba 100 pekee;
📌 Ripoti majaribio ya utapeli kupitia namba 15040 (tuma namba ya aliyekupigia au kukutumia ujumbe wa kitapeli);
📌 Hakiki laini zilizosajiliwa na NIDA yako kwa kubofya *106 #
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Mawasiliano Towers, 20 Sam Nujoma Road
Dar Es Salaam
14414
Opening Hours
| Monday | 08:00 - 18:00 |
| Tuesday | 08:00 - 18:00 |
| Wednesday | 08:00 - 16:00 |
| Thursday | 08:00 - 18:00 |
| Friday | 08:00 - 18:00 |
