Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation

Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation

Share

Welcome to Foreign Tanzania Page. Through this page you will find range of activities relating to the work of the Ministry in Tanzania and abroad.

Photos from Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation's post 06/10/2025

Waziri Kombo apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Uholanzi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ufalme wa Uholanzi Mheshimiwa Marjo Johanna Jacoba Crompvoets, katika hafla iliyofanyika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar Es Salaam.

Mhe. Kombo amempongeza Mheshimiwa Crompvoets kwa uteuzi wake na amemuhakikishia ushirikiano wakati wote atakapokuwa anahudumu hapa nchini.

Aidha Waziri Kombo ameipongeza Serikali ya Uholanzi kwa jitihada za kuanzisha miradi mbalimbali inayoigusa jamii moja kwa moja na kuleta maendeleo ya jamii ikiwemo katika sekta za miundombinu, elimu, afya, mifugo, biashara na uwekezaji na utalii.

Naye Mhe. Crompvoets ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano uliopo na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo kupitia maeneo ya kipaumbele yakiwemo kilimo cha mbogamboga, matunda na maua.

Photos from Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation's post 01/10/2025

WAZIRI KOMBO: USHIRIKIANO WA AFRIKA NA NORDIC LAZIMA ULETE MATOKEO HALISI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amesisitiza umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti na endelevu ya ushirikiano kati ya nchi za Afrika na Nordic, akibainisha kuwa ushirikiano huo lazima ulete matokeo halisi kwa wananchi wa pande zote mbili.

Akizungumza na ujumbe unaohudhuria Mkutano wa 22 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kati ya Afrika na Nordic, unaofanyika mjini Victoria Falls, Zimbabwe, Waziri Kombo amesema mkutano huo ni fursa muhimu ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii, sambamba na kuchochea biashara, uwekezaji, teknolojia na nishati safi.

“Ushirikiano huu haupaswi kubaki kwenye makaratasi pekee. Tunapaswa kuhakikisha tunazitumia fursa zilizopo kwa vitendo ili kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi,” alisema Waziri Kombo, huku akisisitiza utayari wa Tanzania kushirikiana na nchi za Nordic kuendeleza miradi ya kimkakati yenye matokeo ya haraka.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. CP Suzan Kaganda, amewahimiza washiriki kutumia mkutano huo k**a jukwaa la kuimarisha diplomasia ya uchumi, kupitia sekta za biashara, uwekezaji, utalii, kilimo, elimu na ulinzi. Naye Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare Matinyi, amesisitiza fursa zilizopo Tanzania kwa ushirikiano wa kibiashara na kiuwekezaji na nchi za Nordic.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Seifu Kamtunda, ameeleza kuwa mkutano huo utajadili mada kuu zinazolenga kuimarisha uhusiano wa Afrika na Nordic, sambamba na kongamano la biashara litakalokutanisha wafanyabiashara, sekta binafsi, wavumbuzi vijana na taasisi za kitaaluma.

Mkutano wa mwaka huu unafanyika kuanzia tarehe 2–3 Oktoba 2025 chini ya kaulimbiu: “Ubunifu kwa Matokeo: Kutumia Teknolojia na Ushirikiano kwa Jamii Zinazojitayarisha kwa Baadaye.”

Taasisi mbalimbali kutoka Tanzania zikiwemo TIC, ZIPA, TCCIA na idara tofauti za Wizara ya Mambo ya Nje zinashiriki ili kuonesha maeneo ya kipaumbele na kukuza majadiliano ya kiuchumi na kidiplomasia.

Photos from Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation's post 01/10/2025

*Gavana wa Kisiwa cha Anjouan aikaribisha timu ya awali ya Madaktari toka Tanzania*

Gavana wa Kisiwa cha Anjouan,Mheshimiwa Dkt Youssef Zaidou ameikaribisha timu ya madaktari na wataalam wa afya toka Tanzania ambao ni msafara wa kwanza uliofika kisiwani humo kwa minajili ya Kambi Tiba.

Gavana Dkt Zaidou alitoa shukrani kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza ahadi yake kwa wakazi wa kisiwa hicho aliyoitoa kwa Rais Azali Assoumani na wananchi wa Comoro alipohudhuria sherehe za Uhuru mwezi Julai.

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Comoro aliushukuru uongozi wa kisiwa hicho chini ya Gavana na Wizara za Afya na Mambo ya Nje Comoro kwa kufanikisha mapokezi makubwa ya madaktari hao.

Madaktari toka taasisi za Jakaya Kikwete na Hospitali ya Taifa Muhimbili wamewasili tayari na baadaye wiki hii madaktari kutoka Hospitali za Benjamin Mkapa,Taasisi za Mifupa na Mishipa ya Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wakiambatana na Bohari ya Dawa (MSD) watawasili kwa kambi hiyo itakayojikita kutibu magonjwa ya saratani,macho,meno,moyo,ngozi,figo,matatizo ya uzazi kwa wanawake na wanaume na mifumo ya mkojo.

Jumla ya wataalam 45 toka Tanzania watashiriki kambi hiyo ya wiki moja.

Photos from Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation's post 01/10/2025

WAZIRI KOMBO AWASILI ZIMBABWE KUSHIRIKI MKUTANO WA 22 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA AFRIKA NA NORDIC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amewasili jijini Victoria Falls, Zimbabwe, kushiriki Mkutano wa 22 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika na Nordic, unaofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 3 Oktoba, 2025.

Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Victoria Falls Mhe. Waziri Kombo amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. CP Suzan S. Kaganda, pamoja na viongozi wa ngazi ya juu kutoka Tanzania na Zimbabwe. Ziara yake inafanyika kufuatia mwaliko rasmi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Prof. Dkt. Amon Murwira.

Mkutano wa mwaka huu unaongozwa na kaulimbiu isemayo: “Innovation for Impact: Leveraging Technology and Collaboration for Future-Ready Societies” (Ubunifu kwa Matokeo: Kutumia Teknolojia na Ushirikiano kwa Jamii Zinazojitayarisha kwa Baadaye). Kaulimbiu hii inalenga kusisitiza umuhimu wa ubunifu, teknolojia na mshik**ano wa kimataifa katika kujenga jamii imara kwa maendeleo ya baadaye.

Shughuli za siku ya kwanza zinajumuisha Kongamano la Biashara (Business Forum) linalokutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi za Afrika na Nordic (Denmark, Finland, Iceland, Norway na Sweden), kwa lengo la kukuza fursa za biashara na uwekezaji baina ya pande hizo mbili.

Katika mkutano huo, Mhe. Waziri Kombo anatarajiwa kuwasilisha vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita katika nyanja za biashara, uwekezaji, elimu, teknolojia na maendeleo ya kijamii, sambamba na kuimarisha ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na nchi za Nordic.

Aidha, atafanya mazungumzo ya kidiplomasia na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika na nchi za Nordic, ikiwa ni sehemu ya jitihada endelevu za kuimarisha uhusiano wa Tanzania na nchi washirika na marafiki wa maendeleo

Photos from Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation's post 30/09/2025

BALOZI MACOCHA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA SINGAPORE

Balozi wa Tanzania nchini Singapore mwenye makazi yake nchini Indonesia, Mhe. Macocha Tembele amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Singapore, Mhe. Tharman Shanmugaratnam katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Istana Septemba 2025.
Katika mazungumzo yao, wawili hao waligusia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Singapore katika sekta za biashara, uwekezaji, nishati na elimu.

29/09/2025

Tanzania na Hungary zaimarisha ushirikiano wao katika sekta za maendeleo

29/09/2025

Hon. Péter Szijjártó’s speech during his official visit to Tanzania today September 29,2025

Photos from Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation's post 29/09/2025
Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Kivukoni Road
Dar Es Salaam
9000