30/05/2026
Mashabiki wa Arsenal wanaendelea kuonyesha uzalendo na ubinadamu kwa kushiriki zoezi la uchangiaji damu katika siku ya Champions Day yanayoendelea Viwanja vya Posta, Kijitonyama.
Wakati tukisubiri tamko la Mheshimiwa Waziri wa Afya kuelekea Siku ya Mchangiaji Damu Duniani, tunakukaribisha nawe kuwa sehemu ya kuokoa maisha.
K**a uko maeneo haya au jirani, fika katika banda la Mpango wa Taifa wa Damu Salama uchangie damu na utoe tumaini kwa wanaohitaji huduma ya damu salama.
🩸 Changia Damu, Okoa Maisha.
29/05/2026
Wizara ya Afya, kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), inakukaribisha kushiriki katika Kampeni ya Kitaifa ya Kuchangia Damu kuanzia tarehe 1 hadi 14 Juni 2026.
Tone moja la ubinadamu. Changia damu, okoa maisha. 🩸✨
Kuelekea kilele cha Siku ya Mchangia Damu Duniani, ungana na Watanzania wenzako nchi nzima kuonyesha upendo wa dhati kwa vitendo. Fika katika
Vituo vya damu salama kanda.
Hospitali za Rufaa kanda.
Hospitali za Mikoa.
Hospitali za Wilaya.
Maeneo ya wazi.
Kambi za Jeshi., au maeneo yote yatakayotangazwa karibu nawe .
Mchango wako ni uhai kwa mwingine! 🇹🇿
DamuSalama
20/05/2026
Watumishi wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama wakiendelea na kikao kazi cha kuandaa Mpango Mkakati (Strategic Plan) wa miaka mitano, kinachofanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 20–24 Mei 2026.
Kikao hiki kina lengo la kupanga mikakati ya kuimarisha huduma za damu salama nchini, kuongeza upatikanaji wa damu salama na kuhakikisha ubora wa huduma kwa wananchi.
Pamoja tunaendelea kujenga mfumo madhubuti wa damu salama kwa afya na maisha ya Watanzania. 🩸🇹🇿
AfyaKwaWote
09/05/2026
Dharura haitoi taarifa. Ajali, upasuaji wa dharura, mama anayejifungua au mtoto anayehitaji matibabu anaweza kuhitaji damu wakati wowote. Changia damu leo ili kuhakikisha damu salama inapatikana kabla haijahitajika kuokoa maisha.