Tanzania Commission for AIDS

Tanzania Commission for AIDS

Share

This blog aims to disseminate HIV and AIDS information to all ages.

26/05/2026

Tunawatakia waislamu na Watanzania wote heri ya sikukuu ya Eid Al Adha

Photos from Tanzania Commission for AIDS's post 26/05/2026

“HAFLA YA UTIAJI SAINI KATI YA TACAIDS NA NMB FOUNDATION”

Mei 26, 2026

Watumishi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania-TACAIDS na NMB Foundation wakiwa katika picha ya pamoja kwenye hafla ya kusaini hati ya Makubaliano ya pamoja iliyolenga kuwawezesha vijana kujukwamua kiuchumi na kijamii katika mradi wa Timiza Malengo, Jijini Dodoma

26/05/2026
Photos from Tanzania Commission for AIDS's post 26/05/2026

“HAFLA YA UTIAJI SAINI KATI YA TACAIDS NA NMB FOUNDATION “

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania-TACAIDS imeingia makubaliano pamoja na NMB Foundation kwa lengo la kuunganisha jitihada za kiafya na kifedha kwa walengwa wa Mradi wa Timiza malengo.

Zoezi hilo limefanyika tarehe 26 Mei, 2026 jijini Dodoma ili kufikia malengo ya pamoja kuwasaidia Wasichana balehe na wanawake vijana kuanzia miaka10-24 ambao ni wanufaika wa mradi huo.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania- TACAIDS, Dkt. Adam Mrisho amesema makubaliano hayo yanalenga kuwawezesha Wasichana balehe na wanawake vijana kujikwamua kiuchumi ili Kuwatoa katika hatari ya kupata mambukizi ya VVU (Virusi Vya UKIMWI)

“Umuhimu wa mradi huu ni kuwawezesha vijana hasa wasichana balehe kujikwamua kiuchumi ili kuwatoa katika mazingira hatarishi ya kupata maambukizi ya VVU.

Aidha, Dkt. Mrisho ametoa shukrani kwa NMB Foundation kwa ushirikiano wao Kwani utakua mfano kwa Sekta Binafsi na Sekta za umma kwa kuonesha namna umoja huo unavyoweza kuleta matokeo chanya katika maisha ya vijana na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NMB Foundation Bw. Nelson Karumuna amesema umoja huu ni kwa ajili ya kuwapatia walengwa elimu ya afya na stadi za maisha ili kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuweza kupunguza utegemezi na uchochezi unaoweza kupelekea hatari ya kupata Maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Hadi kufikia makubaliano haya Mradi wa Timiza Malengo umeweza kuwafikia walengwa takribani laki mbili na Ishirini katika Mikoa 10 ukilenga kutoa elimu ya Afya na stadi za maisha ili kuongeza uelewa juu ya VVU na UKIMWI ikiwemo elimu ya Kinga, Matibabu na Matunzo.

Photos from Tanzania Commission for AIDS's post 26/05/2026

TA

Photos from Tanzania Commission for AIDS's post 26/05/2026

“HAFLA YA UTIAJI SAINI KATI YA TACAIDS NA NMB FOUNDATION”

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania-TACAIDS na NMB Foundation iliyo chini ya Benki ya NMB (National Microfinace Bank) wamesaini hati ya makubaliano yenye lengo la utekelezaji wa pamoja wa mradi wa Timiza Malengo uliolenga kuwawezesha vijana kujikwamua Kiuchumi na kijamii ili kuepuka mazingira hatarishi ya kupata maambukizi ya VVU( Virusi Vya UKIMWI)

Hafla hiyo ya Makubaliano imefanyika tarehe 26 Mei, 2026 jijini Dodoma.

Photos from Tanzania Commission for AIDS's post 25/05/2026
Photos from Tanzania Commission for AIDS's post 21/05/2026

“TACAIDS YABORESHA HUDUMA ZA VVU NA UKIMWI -VITUO VYA MAARIFA”

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania- TACAIDS Dkt. Adam Mrisho amekutana na Mkurugenzi wa shirika la North Star Alliance (NSA) na kujadili namna bora ya kuboresha vituo vya maarifa vinavyotoa huduma za VVU na UKIMWI kwa madereva wa malori ya masafa marefu vilivyopo Kurasini- Dar-Es- Salaam, Ilula Mfuo - Iringa na Uzunguni- Songwe vinavyo simamiwa na shirika la North Star Alliance- NSA.

Dkt. Mrisho amekutana na kufanya mazungumzo leo tarehe 21 Mei 2026 na Mkurugenzi wa shirka la NSA Bi. Eva Mwai katika Ofisi za TACAIDS jijini Dodoma

Aidha Dkt. Mrisho amesema TACAIDS itakua mstari wa mbele katika kusimamia na kufuatilia vituo hivyo ili kuhakikisha huduma za VVU na UKIMWI zinawafikia walengwa kikamilifu .

Photos from Tanzania Commission for AIDS's post 21/05/2026

“TACAIDS NA LATRA WAJIPANGA KUTOA ELIMU KUPITIA USAFIRI WA ABIRIA “

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania-TACAIDS imefanya kikao cha majadiliano na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini-LATRA kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu VVU na UKIMWI kupitia vyombo vya usafirishaji ikiwemo mabasi ya abiria na treni ya mwendokasi .

Kikao hicho kimefanyika tarehe 20 Mei 2026 katika Ofisi za LATRA jijini Dodoma na kujadili ushirikiano wao katika kufikisha elimu kwa Jamii.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Adam Mrisho amesema TACAIDS imelenga kuandaa jumbe za video kwa kushirikiana na LATRA zitakazo ruka kupitia usafiri wa abiria kwaajili ya kutoa elimu kuhusu VVU na UKIMWI, Unyanyapaa kwa Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI-WAVIU, upatikanaji wa dawa za kufubaza VVU na kinga.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa LATRA CPA, Dkt. Habibu Suluo amesema upo umuhimu wa kutoa elimu hiyo Kwakua usafiri wa abiria ni moja Kati ya vyombo vinavyo tumiwa na jamii kwa kiwango kikubwa kwa rika tofauti.

Aidha kikao kimejadili kuhusu fedha za mapato ya Tozo katika kuimarisha Mwitikio wa UKIMWI nchini.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


P. O. Box 76987
Dar Es Salaam
255