04/10/2024
;
; Usiogope(2)
------------------------------------
5. Kwa sababu Muumba wako ni mume wako;
BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na mtakatifu wa Israel ndiye mkombozi wako;
Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.
6. Maana BWANA amekuita k**a mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni,
k**a mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako.
7. Kwa kitambo kidogo nimekuacha;
lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya.
8. Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu ktk dakika moja;
lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema BWANA, Mkombozi wako.
{ 54-5}
.
----------------------
Haleluja watu wa Mungu.
Neno la Mungu kupitia kinywa cha nabii Isaya linasema kuwa "kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jna lake;"
Kwa hiyo kusema kwamba Mungu pia ni mume wa wajane na ni mtetezi wao.
41;14
Usiogope, Yakobo uliyemdudu, nanyi watu wa Israel; mimi nitakusaidia,
asema BWANA, na mkombozi wako ni mtakatifu wa Israel.
Kwa hiyo Mungu huyu anayesema na nabii Isaya, ni Mungu wa wote wenye mwili asiye na ubaguzi
wala hangalii wewe umeolewa au mjane.
Neno la Mungu linaendelea kwa kusema "Yeye ni Mungu wa dunia yote"
Wakati wanadamu wanapofikiri wamekuacha, na kukutenga mbali nawe.
Na kufananishwa na mke aliyeachwa na mumewe na kuhuzunishwa rohoni, na kuwa mwenye dhiki na kukata tamaa.
2Kori 4;17
Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana.
Haleluya watu wa Mungu, kwa hiyo wakati unapihisi umeachwa na kuwa na dhiki, shida na taabu.
Mungu anayaachilia ili pale utakapoona umeaibika vya kutosha mbele za wanadamu, ndipo Mungu anakuinuwa na kukuweka mahala pa juu na kukuondolea aibu yako yote.
Na ndiyo maana kichwa cha somo tukapewa "USIOGOPE"
Maana pale utakspoogopa ndipo adui yako anachukuwa nafasi ktk maisha yako.
Kwa sbabu hiyo basi, haijarishi itakutesa kuasi gani, lakini neno moja ulishike ni hili .
31;3
BWANA alinitokea alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa upendo wa milele,
ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.
Hakika Bwana Mungu umetuita na kutupenda kwa fadhili za milele, hivyo tusiogope, wewe u pamoja nsi daima.
Mbarikiwe nyote
21/07/2024
.
[1]Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa k**e walizaliwa kwao,
[2]wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
[3]BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
[4]Nao Wanefili
walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
[5]BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote.
[6]BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
[7]BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya.
[8]Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
{Mwa 6;1-8}
.
Ahsante Mungu kwa upendo wako mkuu kwetu.
Ni neema yako tu inatupa kuwa hivi tulivyo.
Wana wa Mungu k**a tunavyoona kichwa Cha somo kisemacho "Uovu wa wanadamu"
Biblia inaeleza kuwa ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na Wana wa k**e walizaliwa kwao.
Vilevile tena imeeleza Wana wa Mungu waliwaona binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
Tunaona maandiko yamewatofautisha kati ya wanadamu na Wana wa Mungu k**a tulivyopewa ujumbe wetu siku ya leo.
Ayubu 1:6
[6]Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao.
Wana wa Mungu ndiyo hao waendao kujihudhurisha mbele za BWANA na shetani hakuwaacha naye akaenda kujihudhurisha.
Mwanzo 8:21
[21]BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai k**a nilivyofanya.
👇👇
Hapo Sasa tunaona jinsi mwanadamu alivyo muovu na mwenye mawazo mabaya siku zote k**a yanenavyo maandiko.
Warumi 1:28-31
[28]Na k**a walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
[29]Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,
[30]wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
[31]wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;
👇👇
Bado biblia inamfunua huyu mwanadamu ni nani .
Kwa hiyo k**a maandiko yanavyoeleza na msingi wa somo letu ulivyo kuwa Uovu wa mwanadamu.
Ndiyo huo ambao umetupa tofauti kati ya Wana wa Mungu na wanadamu.
Nami ombi langu kwetu sote tukawe Wana wa Mungu na si wanadamu (asili ya damu na nyama)
Mungu mwenye rehema na neema atubariki sisi sote.
21/07/2024
.
; Mnara wa Babeli ni nini?.
-----------------------------------------------------
[1]Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
[2]Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
[3]Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.
[4]Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
[5]BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.
[6]BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
[7]Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.
[8]Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.
[9]Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.
{Mwa 11;1-9}
Tunakushuru Mungu kwa wema wako na pendo lako kuu kwetu.
Ndugu zangu na Wana wa Mungu maandiko tunaona yakieleza namna watu waliokuwa wamedhamiria kujenga Mnara wa Babeli ili wamfikie Mungu.
Nachotaka mjue kuwa hawa watu walitoka ktk nchi yao na kwenda ktk nchi ya ugeni na kuanza kuwaza mioyoni mwao
👇👇
"Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.
]Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote." 🫂
👆👆
Ni kwamba hawa watu kwanza waliiacha asili yao k**a maandiko yanenavyo.
Ilikujiinua na kupeana fahari wao kwa wao.
Yohana 5:44
[44]Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwuutafuti?
👆👆
Hapa tunaanza kuona Mnara si jengo Wala matofari Bali ni sifa au tabia ya mtu au watu ktk jamii mahali.
Ya kwamba ni watu wenye kuacha kumpa Mungu nafasi ndani mwao bali ni na nafasi zao hujitukuza.
Mwanzo 18:21
[21]basi, nitashuka sasa nione k**a wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na k**a sivyo, nitajua.
👇👇
Ndipo maandiko yanautonyesha
Mungu alivyozitazama dhamiri za hao wajengao Mnara ambao ni tabia zao na Wala si Mnara halisi.
Kwa sababu wameacha tabia ya uungu ambayo ni asili yao tangu mwanzo.
Zaburi 2:1,4
[1]Mbona mataifa wanafanya ghasia,
Na makabila wanatafakari ubatili?
[4]Yeye aketiye mbinguni anacheka,
Bwana anawafanyia dhihaka.
Wakati mataifa wanafanya kila wanaloona linafaa kwa nafasi zao k**a wajengao Mnara lakini Mungu anawatazama toka mbinguni na anawafanya dhihaka.
Ndugu zangu na Wana wa Mungu tutambue kuwa Mungu hadhihakiwi K**a ambavyo wale waliokusudia kujenga Mnara.
Mungu wetu atubariki sote.
08/06/2022
;
: JINA LA YESU LINAPONYA.
-------------------------------------------------------------------
32. Hata Petro alipokuwa akizunguka zunguka pande zote akawatelemkia na watatkatifu waliokaa Lida .
33. Akamwona mtu mmoja huko , jina lake Ainea , mtu huyo amelaka kitandani miaka minane, maana alikuwa amepooza.
34. Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka , ujitandikie. Mara akaondoka.
35. Na watu wote waliojaa Lida na Sharoni wakamwona , wakamgeukia Bwana.
{ 9;32-35}
;
Bwana Yesu asifiwe wapendwa watu wa Mungu,
Watu wa Mungu tunaposema jina la Yesu linaponya neno hili ni amini na kweli, tunamwona Petro baada ya mizunguko yake na aka ametelemkia ktk mji wa Lida.
Biblia inasema Petro alimwona alimwona mtu mmoja aitwaye Ainea, mtu huyo alikuwa amepooza kwa muda wa miaka minane amelala kitandani , na bila shaka alikuwa hajiwezi homa.
Na jamii nzima iliyokuwa ikimzunguka haikuwa na lolote la kufanya zaidi ya kumuacha wakisubili afe tu.
Lakini tunamwona mtume Petro baada ya kumwona akamwambia "Ainea Yesu Kristo akuponya; ondoka ujitandikie." Mara akaondoka.
Na watu wote waliokaa Lida na Shaaloni wakamwona, wakamgeukia Bwana.
Kwa hiyo baada ya matendo makuu, yaani baada ya kuona kuponywa kwa yule Ainea kupitia mkono wa Petro watu wote walimwamini Bwana Yesu(wakaokoka).
Mpendwa yawezekana bado hujamwamini Bwana Yesu, naomba utambue kuwa Jina la Yesu ni lenye mamlaka na tena lina nguvu linaponya, na kuzishinda nguvu za giza .
Na k**a una mgonjwa, au tawezekana ni mdhaifu wa mwili na roho liitie Jina la Yesu kwa maana lina ponya na kufariji.
Usikate tamaa hata k**a ni kwa muda mrefu unateseka na kupitia changamoto mbalimbali za maisha.
Jina la Yesu litakuheshimisha na kukutia nguvu wakati wote.
MUNGU ATUBARIKI SOTE.
14/03/2021
Ufunuo 3; 2
Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.
21/09/2019
Pole kwa Wanachikola wenzangu kwa msiba wa Madeje Chikoti.
09/04/2018
Karibuni wadau wa Chikola tuyajenge
21/11/2017
Pole kwa wanafamilia na ndugu jamaa na marafiki kwa kuondokewa na Mzee wetu Chikoti Mchiwa kilichotokea muda wa SAA 3....... Usiku.
Ni kifo ghafla.
19/08/2017
Habarini ndugu jamaa na marafiki, nawapenda sana.