Saikolojia Na Wewe: Jijue Na Ujielewe Ufanikiwe

Saikolojia Na Wewe: Jijue Na Ujielewe Ufanikiwe

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Saikolojia Na Wewe: Jijue Na Ujielewe Ufanikiwe, Public & Government Service, Tabata Highway, Dar es Salaam.

PATA fikra na mawazo juu ya familia, mahusiano, matatizo ya maisha, changamoto mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kiteknolojia kwa kudurusi kurasa hii mara kwa mara.

17/02/2014

Hasira mama wa madhara

Watu wengi wanaokuwa na hasira huishia kupata hasara kubwa zaidi, kwa kuwa maamuzi yanayofanyika mtu akiwa na hasara huwa hayana tafakuri wala kujiuliza.
Ndio maana utasikia mama kamwagia mwanawe maji ya moto au kamrushia kisu au kamkata au kumchoma vidole kwa sababu kapoteza shilingi mia moja na vitu k**a hivyo. Ukichunguza sana unakuta kwa kuwa baba kamnyima mama Unyumba au hela ya matumzi!
Kila inapowezekana usifanye uamuzi wowote unapokuwa katika hali ya hasira. Kaa. Tulia. Hasira zikipungua au vizuri zaidi zikishaisha, sasa amua unalotaka kuamua. Kwayo njia hii aghalabu wewe na unaowapenda au kuwahudumia mtajikuta mko salama siku zote!

13/02/2014

Wanawake wasiofaa kuoa au kuolewa

WANAWAKE wote sio wanaofaa kuolewa. Wanaweza kuwa vijakazi au masuria, lakini hawafai kuwa wake. Suala la ndoa ni hiari yako. Ila ukoa watu k**a hao basi anza kuagana na raha, furaha, utulivu na amani siku hiyo hiyo. Kati ya wanawake ambao tunashauriwa na wahenga kutothubutu kuwaoa ni pamoja na:

1. Ananaa
Huyu ni yule asiyeisha kulalamika, kunung'uika, kusingizia hiki au kile, huyu au yule na asyekosa kuumwa kila siku;
2. Mananaa
Ni mwanamke ambaye akikutendea wema au akawatendea watu wako wema, siku moja atakuja kukumbusha kuwa k**a siyo yeye usingelipata kitu fulani.
3. Hananaa
Msichana alyeachana na mchumba wake ukamuoa wewe au mwanamke aliyeachika na kila siku anamkumbuka mume au mpenzi wake wa zamani;
4. Kayatul -kaifaa
Msichana au mwanamke mwenye kunukia sifa mbaya za kila aina;
5. Haadakaa
Msichana au mwanamke ambaye starehe yake sio kutafuta fedha, bali kutumia. Shopping kila siku, tena maduka ya kifahari ndiyo starehe yake. Ukipon kufilisika ni bahati yako;
6. Barakaa
Mwanamke au msichana ambaye kazi yake ni kujipodoa, kujiremba na ulmbwende wa kupita kiasi.Jiulize anajiremba kwa sababu yako au watu wa nje, kwani anatakiwa ajipendezeshe kwako na sio kwa wengine;
7. Shadakaa
Mwanamke au msichana ambaye hachoki kuzungumza ila anawachusha wengine kumsikiliza. Hafungi mdomo toka asubuhi hadi jioni, afadhali hata ya cherehani au CD au redio ambayo huzimika umeme ukikatika;
8. Afkani/Hazimo/Jangalala
Mwanamke au msichana ambaye ni mjinga na hataki kujifunza kitu kipya au cha zamani. Atakuzalia mazoba kebekebe ndani ya familia yako;
9. Mlevi
Mwanamke au msichana au mlevi hata k**a halewi sana muogope k**a ukoma. Pombe ikishamwingia, hujirahisisha kupita kiasi na ndio wasababishaji wakubwa wa nyumba nyingi vijijini kuungua na maisha ya watoto kuteketea;
10. Mtembea nusu uchi
Huyu k**a sinema au picha kila kitu keshakuonesha, ukimuoa ni kipi utakachokwenda kukiona isipokuwa vya kupitukia na tabia mbaya na chafu;
11. Mkalia umbeya
Kaziye si kutafuta na kuongelea juu ya maendeleo yake na watu wake, bali kusikiliza na kueneza umbeya kuhusu nani kafanya hiki au nani kafanyiwa na nani au nani kanunua au ana nini. Kwake yeye habari wengine wamefanza nini, siyo yeye anafanza nini kujiendeleza;
12. Asiye na haya
Mwanamke au msichana asiye na haya mbele ya watu mwepesi wa kuzainiwa na kutumiwa na watu wengine kwa zuri au baya kwa upande wako. Jihadhari sana na mwanamke wa aina hii;
13. Mtoa siri za ndani nje
Hafai kabisa mchumba au mke ambaye mambo yenu ya ndani ni yeye na siyo mtu toka nje anayekuwa ni wa kwanza kuyaanika hadharani. K**a mtembea uchi, huiacha nyumba uchi haijasetiriwa na jicho la wema au waovu, wacha Mungu wala wachawi;
14. Akufanyaye wewe mama na yeye ndiye baba
Mwanamke au msichana anayejitia uzungu hali wewe si wa kuridhia hilo akakutawala kwa kila kitu. Unaweza kuvumilia kwa muda, lakini Uafrika wako ukitiwa hamira na kuibuka basi nyumba hiyo huwa ni balaa baluwani!

27/01/2014

USIACHE kuwa nami kesho kujua siku yako itakwenda kivipi? Huenda nikakuletea kile kile kilicho kichwani mwako baada ya kuzisoma nyota kwa jioni hii!

27/01/2014

HASIRA HASARA

Msemo huu ni rahisi na mwepesi. Lakini yanapokupata mambo yake ni mazito.
Kuna kazi ambazo kwa asili zinatakiwa kufanywa na watu wavumilivu, wenye subira na wasiokasirishwa haraka. Kazi hizi ni pamoja na ualimu, udaktari, unesi, uongozi wa kiimani, udereva na utoaji huduma mbalimbali !
Ushauri ni kwamba ukishajiona ni mtu wa hasira kubwa na kali, ni vyema usikubali kuajiriwa kaitka kazi hizo. Maana siku ya siku zikilipuka zitaiza wengine pengine na kukuliza wewe pia!
Kwa wanaoajiri ushauri wangu ni kwamba ipo haja ya kuwachunguza watu kabla ya kuajriwa. Na kwa kazi k**a hizi asijekuajiriwa mwalimu ambaye pamoja na kumchapa mtoto, anamsukumia teke la haja na kumlemaza mwanafunzi wake maisha.....Hasira hakika hasara, na awayo nayo haifai kwenye ajira k**a hizi.

NENDA na wakati, pata nyota yako ya kila siku kila asubuhi zinazokwenda na wakati na teknolojia ya leo toka kwa mtabiri anayechipukia kwa kasi sana Tanzania na Kenya....

25/01/2014

Jifunze saikolojia ili uongoze watu vyema.

Mfano hai wa umuhimu wa saikolojia na sosholojia hivi sasa ni ule unaoendelea nchini Misri ambako baada ya kuondolewa kwa serikali iliyoingia madarakani kidemokrasia kwa majenerali wao kutokuwa wanafunzi wazuri wa saikolojia na sosholojia ni dhahiri kabisa ukizingatia kwamba majenerali hao hao wameshaiabisha Misri mara kadha kwa kushindwa vibaya na jirani zao, kuwa utakapomwita mtu muuaji naye hakuwa muuaji 'neno' huumbwa atageuka na kuwa muuaji. Utakapomwita mtu gaidi, wewe mwenyewe kwa kauli zako utamuumba huyo gaidi.
Saikolojia inngeliwajuza watu hawa kuwa mwanadamu ni mwanadamu, si mavazi, sio cheo wala sio silaha inayokupa utofauti. Wewe ukiwa wa huu, wenzako kwa uadui au urafiki wa hila watageuka wa unhuu!
Kuijua saikolojia ni kujua namna za kuishi na watu wa aina zote!

14/01/2014

Usiongeze matatizo kwa kufanyiana ukatili...

Kuna matatizo mbalimbali yanayoweza kutokea katika ndoa. Leo nizungumzie lile la kidhana au kifikra. Dhana au fikra inawez kuwasilishwa kwa mwenzio kwa maneno au bila maneno.
Ikiwa unanuna na kutozungumza na mwenzako, kisha ukamkatalia tendo la ndoa baadaye bila mawasiliano yoyote, anakuelewaje? Hukuona ni adui mkubwa, na mapenzi huyeyuka. Na dhana mpya hupandwa kichwani kwake, kwamba tayari umekwishajitosheleza mahala pangine. Ni vyema, basi kujizuia kumkatili mwenzio wakati mnanuniana, na k**a ikilazimika hivyo tafadhali mtafadhalishe kwa kissababu chochote chenye uzito wa kutosha: siku zangu, sijisikii vizuri, sioni ham u kabisa, au nimechoka zaidi yakuchoka...unajua, subiri baadaye mwenzi wangu... na kadhalika....
Maisha ni mafupi, msipotezeane muda bure, ona wangapi wameshaondoka toka mwaka tuuanze...
Binadamu tumeumbwa tulivyoumbwa ili tuwe na tunayomficha mtu na shetani, na yale tuwezayo kuacha wazi. Migogoro mingi huletwa na wale wanaotaka kufunua yaliyofunikwa na wakati mwingine hadharani !!
Ukiyafunua yangu, yako kesho hayatafunuliwa ?

10/01/2014

Kwanini ni rahisi kushindwa kuliko kufanikiwa katika biashara ya magazeti Tanzania ?

UINGIAJI kaitka biashara ya uchapishaji na uuzaji magazeti Tanzania hivi leo ni kitu kigumu sana sio kutokana na ushindani mkubwa bali kutokana na changamoto zilizopo katika uanzishaji miradi ya kiuchapishaji hapa nchini.
Hapa chini ni baadhi ya changamoto ambazo mjasiriamali anayetaka kuthubutu kuingia kwenye biashara ya uchapishaji, usambazaji na uuzaji gazeti atapaswa kuzikabili penda asipende:
Masharti na urasimu katika uanzishaji gazeti. Ili kuanzisha gazeti ni lazima utafute usajili wake na kuna masharti na urasimu yatakayokutoa jasho hadi ufanikishe kupata urajisi kamili. Kenya huwa unaanza gazeti na kulichapisha moja kwa moja na baada ya kuwa mitaani ndio unakwenda kulisajili ;
Hata ukinunua gazeti toka kwa mtu mwingine. Inaweza ikawa ni rahisi zaidi kununua haki za umiliki gazeti toka kwa aliyeshindwa kulichapisha, lakini epuka matapeli waliojaa katika eneo hili. Aidha wanaokukodishia gazeti ukianza kufanikiwa ni rahisi kukugeuka au kukataa makubaliano ya awali na kutaka marejeo ya mkataba;
Seng'eng'e ya genge la mawakala. Kizingiti kikubwa sana hivi sasa ni genge la mawakala ambao wana umoja katika kukusaidia kufanikisha azma yako au kuliua gazeti lako likingali changa bado. Hawa wana mbinu za kila aina kuhakikisha k**a hawakutaki, unashindwa na unashindwa vibaya. Ujanja na ajizi inayofanyika kwenye eneo hili inaweza ikwa inachangia mtu au shirika kukosa asiimia 25 ya mapato yake halali;
Ukame wa watu wanaojua usimamizi na menejimenti ya magazeti. K**a inavyojulikana, mameneja na maofisa wengi kwenye magazeti Tanzania ni watu waliopata ujuzi na maarifa ya kazi zao kutokana na kuwepo kwenye gazeti jengine, lililopo au lililokufa. Aidha, ndivyo ilivyo kwa vyombo vingine vya habari k**a tivii na redio pia. Bado hatujawa na shule kuu inayowafunza watu kuwa mameneja wa vyombo vya habari. Tija katika utendaji kazi inaweza kushuka kwa asilimia 50 kutokana na kuajiriwa watu wasio na uwezo unaostahili kufanya kazi walizopewa;
Changamoto katika upatikanaji matangazo ya kutosha. Ili kupata matangazo ya kutosha unahitaji kuwa na gazeti lililokuwepo kwenye mzunguko kwa miezi k**a sio miaka kadhaa. La sivyo, lazima uwe na fedha au mtaji wa kutosha kuweza kuwanunua watoa matangazo mbalimbali ili ufanikishe azma ya kujiendesha pia kwa kutumia pato linalotokana na matangazo. La sivyo, wewe mwenyewe uwe na biashara zako kadhaa ambazo zinahitaji kujitangaza na zitakuwa zikilipa gazeti bila kujali udugu uliopo;
Ubia kati ya mawakala na wafanyakazi wa viwanda vya uchapishaji utakakokuwa ukichapisha gazeti lako. Upo uwezekano mkubwa wa kuwa na watu wako au Idara yako ya Usambazaji inayoshirikiana kwa heri au shari na mafundi wa kiwanda cha uchapishaji. Kinachofanyika hapa ni kwamba, mafundi kiwandani hawayaharibu kabisa magazeti machafu (reject) k**a wanavyopaswa, hadi yawe yasiyosomeka. Bali huyaacha mengi yakiwa bado yanaweza kuonekana k**a yaliyorudi baada ya magazeti safi kuuzwa. Wakala wanauziwa magazeti hayo machafu na kuyarudisha kwako mchapishaji k**a vile ni nakala zilizorudi bila kuuzwa (returns),lakini wao wameshauza pengine na kumaliza mgawo wao wa kila siku. Kwa namna hii, hasara unakula wewe, wakati mchapishaji na idara yako ya usambazaji inazidi kuvimbiana tu. Mtu au kampuni inaweza kupoteza kufikia asilimia 30 ya mapato halali kwa hujuma zinazofanywa katika eneo hili;
Mtihani katika usambazaji. K**a nilivyosema awali ukitegemea usambazaji kupitia wakala waliopo hivi leo, lolote linaweza kutokea. Nimekwishaona mawakala waliosusia kuuza gazeti eti tu kwa sababu hawakualikwa kwenye hafla ya kulizindua gazeti husika. Hatari kubwa inakuwepo pale ambapo mkuu wa usambazaji anawez akafanya maamuzi ya kifedha au kibiashara bila kumshirikisha meneja mkuu;
Mtihani katika viwanda vya uchapishaji. Bado uaminifu na udhibiti katika mashirika mengi ya uchapishaji ni mdogo na kwa kuwa kazi yenyewe inafanyika USIKU, ina mianya kadhaa inayotumika kupoteza lengo na mafundi uchapishaji kuhakikisha kwamba wanalichapisha gazeti wakati ambapo hamna udhibiti wa kutosha.
Wafanyakazi wapowapo na wasiojitambua. Magazeti mengi bado yanaajiri wafanyakazi ambao hawajali kinacholisibu gazeti, bali wanafikiria tu mishahara na posho zao wakati wote. Hiyo ni haki yao. Lakini, je, katika nyakati hizi mkiachia gazeti kuwa na mianya mingi kiasi hicho huo mshahara kweli utapatikana kiurahisi au kazi itakuwa ni kulipana tarehe 32 k**a sio 45 ya kila mwezi? Tambua malipo ya mishahara yanapocheleweshwa, wafanyakazi wanavunjika moyo, wanakosa hamasa na wengi wao wanakuwa madeiwaka kwa magazeti au vyombo vingine vya habari. Ajizi toka kwa waajiriwa na wale wanaostahili kuiona mali ya kampuni k**a vile ni mali yao inachangia kupotea kwa zaidi ya asilimia 25 ya mapato ya mtu au kampuni;
Maudhui zianzofanana na wengine. Ukiyaangalia magazeti mengi nchini huwa na habari zilezile k**a ni udaku, ni udaku au k**a ni habari za kwaida, habari ni zile zile na pengine zimeandikwa na mwandishi huyo huyo kwa majina tofauti. Kablal hujaingia kwenye biashara ya gazeti hakikisha kuwa una mawazo ya maudhui tofauti kabisa angalau kwa robo gazeti k**a sio thuluthi gazeti tofauti na ya yale yaliyomo kila leo kwenye magazeti yaliyopo.
Kufa kwa soko la mazoea na kuzuka soko jipya la vijana wa smartphone. Hivi leo wasikilizaji wengi wa redio za kitaifa na watazamaji wa tivii za kitaifa na wasomaji wenye uwezo wa kununua magazeti ni wale wenye umri wa miaka 45 na kuendelea. Walio chini ya hapo wengi wao wanapendelea kufuatilia mambo kwenye tovuti au simu zao za mkononi. Mwelekeo huu inaelekea ndio tu umeanza kuchanua hivi sasa na utazidi kuendelea kadri simu za smartphone zinavyozidi kufirika na kuwa za bei nafuu zaidi nchini;
Ukosefu wa ubunifu na uvumbuzi wa mambo mapya. Chombo cha habari cha kesho na keshokutwa kitakachofanikiwa, kwa maoni yangu, kittakuwa ni kile kitakachoweza kuivisha katika chungu kimoja biashara ya simu za mkononi ma maudhui hitajika; matangazo ya tivii na redo na matumizi yanayoendana na wakati ya tovuti kwa kuwa na wavuti zinazobeba yale yaliyomo kaika midia nyengine.
Baada ya muda sio mrefu pia, makampuni ya magazeti yatakayochangia kuwa na mashine za bei nafuu za kumuwezesha mtu kuchapisha nakala chache tu za gazeti (zima au sehemu yake ) nyumbani au ofisini kwake ndio yatakayoendelea kuvuna kutoka kwa wasomaji wake waaminifu.
Ieleweke kwamba hatusemi moja kwa moja kwamba yeyote anayetaka kuanzisha gazeti Tanzania atashindwa. La, hasha ! K**a una vyanzo vingine vya fedha vya kutegemea ma visivyokauka kiurahisi; k**a una njia za kupata matangazo kutoka serikalini na mashirika makubwa; k**a una wafanyakazi wachache na wanaoweza kufanya kazi sio chini ya masaa 14 kwa siku na k**a utaweza kufuatilia yote yanayofanywa na walio chini yako, bado uchapishaji gazeti sio kazi mbaya na hasa k**a utakuja na maudhui inayosadia kuwaamsha na kuwawezesha watu kimawazo, kiajira na kiuchumi kwa ujumla.

>
+255782808539
[email protected]

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


Tabata Highway
Dar Es Salaam
11337