BRELA Tanzania

BRELA Tanzania

Share

The Business Registrations and Licensing Agency deals with Business Names,Trade Marks,Industrial License, and Patents.

BRELA is a Government Executive Agency established under the Government Executive Agencies Act No. 30 of 1997. It was established on the 28th of October, 1999 by Government Notice No. 294 A published on the 8th October, 1999 and it was officially inaugurated on the 3rd December, 1999. AIM, ROLE AND STRATEGIC OBJECTIVES

AIM
-The aim of the Agency is to ensure that businesses operate in accordance

Photos from BRELA Tanzania's post 14/05/2026

MAWAKILI NA WAHASIBU WAPEWA MAFUNZO KUHUSU DHANA YA MILIKI MANUFAA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) leo Mei 13, 2026 imetoa mafunzo kwa wahasibu na mawakili kuhusu dhana ya Umiliki Manufaa (Beneficial Ownership), yaliyofanyika katika Ukumbi wa TAGLA jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuwajengea uwezo washiriki kuhusu umuhimu na utekelezaji wa dhana hiyo.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Kampuni na Majina ya Biashara kutoka BRELA, Bw. Isdor Nkindi, amewataka washiriki kuzingatia na kutekeleza ipasavyo dhana ya Umiliki Manufaa katika shughuli na mifumo ya taasisi wanazozihudumia.

Kwa upande wake, Afisa Usajili kutoka BRELA, Bi. Gift Wazingwa, amesema ni muhimu dhana ya Umiliki Manufaa kuzingatiwa sambamba na mifumo ya sheria inayotumika nchini ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika umiliki wa kampuni na biashara.

Aidha, washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza BRELA kwa kuandaa mafunzo hiyo, wakieleza kuwa imewasaidia kupata maarifa mapya yatakayowawezesha kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

BRELA imekua ikifanya Semina, Mafunzo, warsha pamoja na Kliniki za Biashara katika mikoa mbalimbali ili kuhakikisha wamiliki wa Kampuni wanapata uelewa wa kukidhi takwa la kisheria ya Miliki Manufaa.

12/05/2026

“Mafunzo ya Miliki Ubunifu”

Photos from BRELA Tanzania's post 12/05/2026

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa, leo tarehe 12 Mei 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Ilala, yakilenga kuboresha huduma za afya kwa watumishi wa Wakala.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi Kuu za taasisi hiyo, Bw. Nyaisa alisisitiza kuwa ustawi wa wafanyakazi ni nguzo muhimu katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi, sambamba na kuendana na dira ya taasisi.

“Afya ya mtumishi ni msingi mkuu wa ufanisi wa taasisi katika kuwahudumia wananchi, hivyo ni muhimu watumishi kuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya,” alisema Bw. Nyaisa.

Kwa upande wake, Meneja wa NHIF Mkoa wa Ilala, Aifena Mramba, alisema kikao hicho kimekuwa na tija kubwa na kimefungua fursa ya kushughulikia changamoto za watumishi kwa haraka zaidi.

Aidha, alieleza kuridhishwa na ushirikiano uliopo kutoka kwa uongozi wa juu wa BRELA, akibainisha kuwa NHIF inaendelea kuimarisha mifumo ya kidigitali ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama wake.

Naye Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji kutoka BRELA, Lameck Kabeho, alisema pande zote mbili zimejadili kwa kina namna ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili watumishi wanapohitaji huduma za afya katika vituo vya tiba.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa mtumishi wa BRELA pamoja na wategemezi wake wanapata huduma stahiki kwa wakati, bila usumbufu wowote,” alisema Bw. Kabeho.

Kikao hicho ni sehemu ya jitihada za BRELA kuendelea kuboresha ustawi wa watumishi wake kwa kuhakikisha wanapata huduma bora za matibabu kupitia NHIF bila vikwazo, hatua inayochochea ufanisi wa kazi.

11/05/2026
Photos from BRELA Tanzania's post 11/05/2026

ELIMU YA MILIKI UBUNIFU YAWAFIKIA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), leo Mei 11, 2026, imetoa mafunzo kwa Majaji wa Mahak**a Kuu na Manaibu Wasajili wa Divisheni ya Biashara kuhusu haki za miliki ubunifu, kwa lengo la kuimarisha usimamizi na ulinzi wa haki hizo nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Jaji Kiongozi, Mhe. Jaji Imani Aboud amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuimarisha uelewa na kubadilishana uzoefu katika eneo la miliki ubunifu.

“Maendeleo ya nchi yoyote yanategemea ubunifu. Hata hivyo, wamiliki wa ubunifu huo wamekuwa wakikumbana na changamoto za kisheria zinazofikishwa mahak**ani. Ni muhimu kwa sisi tunaosikiliza na kutafsiri sheria kuelewa kwa kina masuala haya ili kuhakikisha haki zinatendeka ipasavyo,” amesema Mhe. Jaji Aboud.

Ameongeza kuwa maamuzi ya mahak**a yana athari pana, kwani hutumika k**a rejea hata katika nchi nyingine, hivyo kuna umuhimu wa kuwa na uelewa wa kina kuhusu haki za miliki ubunifu.

Kwa upande wake, Jaji wa Mahak**a Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, Dkt. Cleoface Morris, amesema kuwa mashauri mengi yanayofunguliwa mahak**ani yanahitaji tafsiri sahihi ya sheria ili kuimarisha usimamizi wa haki za miliki ubunifu.

“Mafunzo haya yatatusaidia kuwa na uwiano katika utoaji wa maamuzi ndani ya Mahak**a Kuu, hasa kwa kuzingatia kuwa mashauri mengi yanafanana kimuktadha,” amesema Dkt. Morris.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa, amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mwendelezo wa juhudi za taasisi hiyo kutoa elimu kwa wadau mbalimbali, hususan katika eneo la miliki ubunifu ambalo bado linahitaji uelewa mpana zaidi nchini.

Ameeleza kuwa maamuzi ya majaji yana mchango mkubwa katika kulinda maslahi ya taifa katika sekta ya miliki ubunifu, na kwamba tayari zipo hukumu kadhaa ambazo zimekuwa msaada mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya BRELA.

“Tumeleta wataalam wa miliki ubunifu ili kujenga uelewa wa pamoja. Lengo letu ni kufikia hatua ambayo kila ubunifu unalindwa kisheria, kwa kuwa ni chanzo muhimu cha kipato kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla,” amesema Bw. Nyaisa.

09/05/2026

Ipday2026

08/05/2026

Wadau michezo na wanamichezo nchini wamehimizwa kutumia huduma za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa kusajili kazi zao za ubunifu na kujifunza kuhusu haki zao ili kuleta tija na ufanisi wa wanamichezo kwa kuwakomboa kiuchumi.

Wito huo umetolewa tarehe 08 Mei, 2026 na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Salvio Kapinga wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Miliki Ubunifu Duniani iliyofanyika hoteli ya Hyatt Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Judith Kapinga alisema kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuhahikisha wanamichezo na wadau wa sekta hiyo wanatumia Miliki Ubunifu kukuza tasnia ya michezo hapa nchini.

“Niwasihi viongozi wa vilabu vya michezo, mashirikisho na wadau wote wa michezo kuwasaidia wanamichezo katika vilabu na mashirikisho yenu kuhakikisha wanalinda haki zao ikiwemo matumizi ya picha au taswira zao katika bidhaa au biashara za watu wengine,’’ alisema Bi. Judith Kapinga.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa BRELA Prof. Neema Mori alisema ni muhimu wadau wa michezo wakajiepusha kabisa kutumia Miliki Ubunifu k**a vile Alama za biashara (logo) zisizo zao pasipo idhini ya wamiliki halisi ili kuepuka kuingia katika matatizo ya kisheria kwa kutumia Alama zilizosajiliwa na watu wengine.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa aliwakumbusha wadau na wanamichezo kutumia majina yao vizuri ‘Brand Names’ kujiandaa na maisha mengine baada ya kustaafu michezo.

“Naomba nitoe mifano michache kwa wachezaji wa kimatiafa wanaoendelea kunufaika kwa kutumia Alama za Biashara ingawa wengine wameshajiuzulu michezo, Alama ya biashara (logo) ya CR7 inayomilikiwa na mchezaji wa mpira wa miguu Christiano Ronaldo ni Dola za Kimarekani Milioni 900,” alisema Bw. Nyaisa.

Kwa upande mwingine Mwenyeki wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mhandisi Leodigar Tenga alisema wakati taifa likiwa kwenye maandalizi ya AFCON 2027 ni vyema wafanyabiashara na wadau wote wa michezo wakahakikisha wamelinda bunifu zao ili kuepuka wizi na uharamia kwenye bidhaa na huduma kwa upande wa matumizi ya Alama (brands) zilizopata umaarufu na ambazo ni bora.

08/05/2026

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


BRELA HOUSE, Plot No. 23, , Block No. 20, , Shaaban Rober Street/Sokoine Drive
Dar Es Salaam
P.O.BOX9393

Opening Hours

Monday 08:30 - 15:30
Tuesday 08:30 - 15:30
Wednesday 08:30 - 15:30
Thursday 08:30 - 15:30
Friday 08:30 - 15:30