HESLB Tanzania

Call Directions Website Contact the organization

HESLB Tanzania Official page for Higher Education Students' Loans Board (HESLB)

15/09/2026
MTUHUMIWA WA KUFUTIA MADENI WANUFAIKA WA MIKOPO AKIRI KOSA NA KUIOMBA RADHI BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU ...
10/09/2026

MTUHUMIWA WA KUFUTIA MADENI WANUFAIKA WA MIKOPO AKIRI KOSA NA KUIOMBA RADHI BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU (HESLB)

Mtuhumiwa wa kughushi na kujifanya mtumishi wa Bodi ya Mikopo sambamba na kuwalaghai wanufaika kuwa anaweza kuwafutia mikopo, amekiri makosa na kuhukumiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma, leo Ijumaa tarehe 4/9/2026.

Mtuhumiwa huyo Nicholaus Komba Mahitana aka Abdallah Mahimbo amehukumiwa kulipa faini ya Tzs. 1,600,000/=, kurejesha fedha taslimu Tzs 3,000,000/= pamoja na sharti la kuripoti katika kituo Kikiuu cha Polisi Mkoani Mbeya mara moja kwa mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu. Kesi hii imehitimishwa leo baada ya mtuhumiwa kumuandikia barua DPP akiomba kuridhia Mkataba wa kukiri makosa (Plea Bargaining).

Tukio hilo limeshuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Dkt. Bill Kiwia, ambaye baada ya hukumu hiyo amewaasa wanufaika wa mikopo kufuata utaratibu sahihi wa urejeshaji na kuepuka kutumia vishoka ambao wanaweza kuwaingiza kwenye matatizo makubwa ikiwemo kupoteza ajira zao .

NAIBU KATIBU MKUU ELIMU AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI HESLBNaibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ...
10/09/2026

NAIBU KATIBU MKUU ELIMU AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI HESLB

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, amezindua Baraza jipya la Wafanyakazi la HESLB, akisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa watumishi katika kujadili masuala ya msingi yanayolenga kuboresha utendaji na ufanisi wa taasisi.

Uzinduzi huo umefanyika leo, 07 Septemba 2026, katika Hoteli ya Cate, Morogoro, ukiambatana na mafunzo kuhusu majukumu na umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi pamoja na majadiliano ya hoja za wafanyakazi.

Akizungumza katika mkutano huo, Prof. Mushi amesema Baraza hilo ni jukwaa muhimu la ushirikishwaji linalowawezesha watumishi kutoa maoni, kujadili changamoto na kupendekeza maboresho kwa ajili ya kuongeza uwajibikaji, nidhamu na tija katika taasisi.

“Baraza la Wafanyakazi ni sehemu kubwa sana ya ushirikishwaji wa wafanyakazi na kujenga umiliki wa pamoja wa shughuli za taasisi. Ni jukwaa la kutoa maoni na kuboresha utendaji ili kuongeza uwajibikaji, nidhamu na tija ya pamoja,” amesema Prof. Mushi.

Amesema pia, Baraza hilo lina nafasi muhimu katika kuhakikisha kuwa maslahi ya mwajiri na wafanyakazi yanalindwa kwa pamoja na kusaidia katika usuluhishi wa masuala yanayoweza kujitokeza baina ya pande hizo mbili.

Prof. Mushi amesisitiza kuwa watumishi ni rasilimali muhimu katika taasisi, akiiagiza Menejimenti ya HESLB kuendelea kuboresha ustawi na maendeleo yao, huku wajumbe wakihimizwa kujenga hoja, kusikilizana na kushirikiana ili kuongeza tija na kutoa huduma bora kwa Watanzania.

Awali, akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, amebainisha kuwa Baraza la Wafanyakazi lina umuhimu mkubwa katika kujenga mazingira bora ya kazi na kuwezesha watumishi kushiriki katika mijadala inayohusu ustawi wao na maendeleo ya taasisi.

Dkt. Kiwia amesema miongoni mwa mambo muhimu yatakayofanyika katika kikao hicho ni mafunzo ya uelewa kuhusu Baraza la Wafanyakazi, pamoja na kujadili hoja za wafanyakazi.

Katika hatua nyingine, Naibu Katibu Mkuu Prof. Mushi ameishukuru Serikali kwa kuongeza bajeti ya mikopo na ufadhili, huku akiitaka HESLB kubuni njia za kuongeza fedha ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike.

Dkt. Kiwia Aishukuru Bodi ya Wakurugenzi ya HESLB Inayomaliza Muda WakeMkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunz...
02/09/2026

Dkt. Kiwia Aishukuru Bodi ya Wakurugenzi ya HESLB Inayomaliza Muda Wake

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dkt. Bill Kiwia, ametoa shukrani za dhati kwa Bodi ya Wakurugenzi ya HESLB inayomaliza muda wake, akieleza kuwa ushirikiano mzuri na uongozi wa Bodi hiyo umeiwezesha HESLB kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kufikia malengo yake ya kimkakati katika kipindi cha miaka mitatu (2023-2026).

Dkt. Kiwia ametoa shukrani hizo wakati wa hafla fupi iliambatana na vikao maalum kati ya Menejimenti ya HESLB na Bodi ya Wakurugenzi vilivyofanyika tarehe 01 na 02 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Malaika.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Kiwia amesema Bodi hiyo imekuwa ya kipekee kutokana na ushirikiano wake wa karibu na Menejimenti, jambo lililowezesha HESLB kutekeleza mikakati mbalimbali yenye lengo la kuongeza ufanisi ikiwemo utoaji wa mikopo na kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wenye uhitaji wanapata fursa ya kupata elimu ya juu.

“Kwa niaba ya Menejimenti na watumishi wote wa HESLB, ninawashukuru kwa dhati Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi kwa ushirikiano wenu wa karibu, ushauri na uongozi mlioutoa katika kipindi chote cha uongozi wenu. Bodi hii imekuwa ya kipekee na imeiwezesha HESLB kutekeleza mikakati muhimu ya kuongeza idadi ya wanafunzi wanaonufaika na mikopo, huku tukijenga msingi wa kuwa na mfuko endelevu wa mikopo,” amesema Dkt. Kiwia.

Ameongeza kuwa, mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wa Bodi hiyo yenye wajumbe 9 wanaowakilisha maeneo ya sheria, fedha, elimu ya juu na elimu ya kati, ni matokeo ya ushirikiano, uongozi thabiti na maamuzi ya kimkakati yaliyolenga kuimarisha huduma zinazotolewa na HESLB kwa wanafunzi na wadau wake.

Dkt. Kiwia amewashukuru Wajumbe wa Bodi hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Hamisi Dihenga kwa kujitolea kwao, weledi na usimamizi madhubuti, akisema Menejimenti inathamini mchango wa kila mmoja katika kuhakikisha HESLB inatimiza dhamana yake ya kuwezesha wanafunzi wa Kitanzania kupata elimu ya juu kupitia mikopo na ruzuku.

Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kushukuru, kutambua, kuthamini na kuaga kwa heshima Bodi ya Wakurugenzi inayomaliza muda wake.

Address

P. O Box 76068
Dar Es Salaam

Opening Hours

Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00

Telephone

+255222864640

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HESLB Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to HESLB Tanzania:

Shortcuts

Share