HESLB Tanzania

HESLB Tanzania

Share

Official page for Higher Education Students' Loans Board (HESLB)

20/05/2026
01/05/2026

PAULO GODFREY MACHIMO
Afisa TEHAMA Mwandamizi
Mtumishi Hodari HESLB mwaka 2025/2026

Njombe, Mei 1, 2026

Afisa TEHAMA Mwandamizi wa HESLB, Bw. Paulo Godfrey Machimo, ameibuka kuwa Mtumishi hodari wa taasisi kwa mwaka huu 2025/2026.

Machimo ametoa shukrani kwa Menejimenti na watumishi wote wa HESLB kwa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na uwepo wa mazingira bora ya kazi.

“Ninaishukuru Menejimenti na watumishi wenzangu kwa ushirikiano wa kiutendaji na kujenga mazingira bora ya kazi. “, amesema Machimo.

Menejimenti na watumishi wote wa HESLB wanakupongeza ndugu Machimo kwa juhudi, maarifa na ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yako.

Big Up 👍🏽

Photos from HESLB Tanzania's post 17/04/2026

Matukio Mbalimbali katika picha wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya “Kiduchu”.

Photos from HESLB Tanzania's post 17/04/2026

Mhe. Wanu Azindua Kampeni ya ‘Kiduchu’ kuhamasisha Urejeshaji Kidogo Kidogo
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, amezindua rasmi kampeni ya “Kiduchu” na kusisitiza umuhimu wa urejeshaji wa mikopo ya elimu ya juu unaozingatia uwezo wa kila mnufaika hususan katika sekta isiyo rasmi ili kuhakikisha uendelevu wa mfuko kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Uzinduzi huo umefanyika leo, (Aprili 17, 2026), katika ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Kanda ya Mashariki, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Wanu amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano (kuanzia 2021/2022 hadi 2025/2026), Serikali imefanikiwa kutoa TZS 3.6 trilioni kwa wanafunzi wa vyuo ngazi ya elimu ya kati na ya juu, hatua iliyowezesha vijana wengi kupata elimu bila vikwazo vya kifedha.
Kwa upande wa makusanyo, amebainisha kuwa HESLB imeendelea kuimarisha ukusanyaji wa mikopo kupitia juhudi mbalimbali za uhamasishaji, hatua inayolenga kuhakikisha kuwepo kwa mfuko endelevu wa kugharimia elimu ya kati na ya juu nchini.
Mhe. Naibu Waziri ameeleza kuwa bado kuna changamoto ya baadhi ya wanufaika, hususan wenye kipato cha chini, ambao hawajaanza au wamesitisha urejeshaji wa mikopo kutokana na hali zao za kiuchumi.
Kutokana na hali hiyo, Mhe. Wanu amezindua rasmi kampeni ya “Kiduchu” yenye kaulimbiu “Fresh, Tunasonga!”, inayolenga kuwahamasisha wanufaika kuanza kurejesha mikopo yao kwa kiasi kidogo walichonacho, kwa kuanzia TZS 5,000. Kampeni ya “Kiduchu”, imelenga kuwafikia wanufaika 135,186 wanaodaiwa jumla ya TZS 920 bilioni.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa HESLB, Prof. Hamisi Dihenga, amesema kampeni hiyo inaakisi kaulimbiu ya “Kazi na Utu” kwa kuzingatia hali halisi ya kipato cha wanufaika.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dkt. Bill Kiwia, alieleza kuwa madeni yaliyoiva yanafikia TZS 2.78 trilioni kutoka kwa wanufaika 539,103, ambapo hadi sasa TZS 1.84 trilioni zimekusanywa kutoka kwa wanufaika 403,917 waliokwisha. Hata hivyo, bado kuna wanufaika 135,186 ambao hawajafikiwa wanaodaiwa TZS 920 bilioni.

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salaam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


P. O Box 76068
Dar Es Salaam

Opening Hours

Tuesday 08:00 - 17:00
Wednesday 08:00 - 17:00