06/11/2016
FILAMU HIPO JIKONI ITAKUWA MITAANI MWEZI WA KUMI NA MBILI(12) 2016
KAENI MKAO WA KULA WADAU WANGU
ukurasa huu utakuonyesha hadithi zinazoingia mitaani,utapata kujua siri za mizimu,majini,maisha & ugaidi
06/11/2016
FILAMU HIPO JIKONI ITAKUWA MITAANI MWEZI WA KUMI NA MBILI(12) 2016
KAENI MKAO WA KULA WADAU WANGU
11/08/2016
...
Matukio katika hadithi
ya
...
11/08/2016
..
Yaliyomo katika hadithi
..
17/05/2016
Hello fans wangu, story ya "PETE YA JINI" inatengenezwa kuandalia katika mtindo wa movie ndiyo maana nimesimamisha kuendelea, movie hipo mbioni mwaka huu inatoka, inawaletea story nyingine muda si mrefu. usikose
05/03/2016
Habari za mida hii ndugu wasomaji,? hivi karibuni nilionesha jinsi zilivyo lakin watu wengine hawakusadiki... leo nimeamua kuonesha picha ya PETE hizi zikivaliwa kidoleni wakati umekosea masharti madhara ni haya>>
02/01/2016
heri ya mwaka mpya fans wangu, kaeni mkao wa kula story ya KIU YA DAMU mtaani mwaka huu, bei ni nafuu sana
15/12/2015
PETE YA JINI
( )
....kila mmoja alikuwa anachangia hoja kadri ya uelewa wake na mawazo yake. mmoja wa wachawi alisimama na kuchangia "kwa jina naitwa Asha Rashid natokea Tanga wilaya ya Andeni,mim naomba niwaulize swali,hivi kile kitoto kimewashindaje wakuu zangu? nipeni kaz mim nimalizie"
umati wa wachawi ukaangua kicheko, "hahahaha..." kwa hali yeyote hile Bi.Asha alikuwa anavituko kwenye vikao,maana wachawi wengine walikuwa wakicheka hadi wanalala chini. "swali zuri Bi.Asha," aliongezea yule mganga rafiki wa babu "sisi tumehisha fahamu makosa yetu na tumehisha jua kuna nin kwa yule kijana", umati wa wachawi wote walishtuka na kuhuliza kwa pamoja k**a wameambizana " eeh! mumejua kuna nini!!!?"
yule mganga mchawi akaendelea, "ndiyo,yule kijana nyota yake ni kali sana ndiyo maana alipona,jana tulipata kuiangalia nyota ya kijana na kuipatia majibu" hapa naomba nielemishe ulimwengu kuhusu nyota,ngoja nikupe siri moja kuu sana,kila mwanadamu anapozaliwa huwa anakitu.....
15/12/2015
PETE YA JINI
( #11)
..babu na yule rafiki yake mganga waliniangalia kwa mshangao.Watu walinizunguka k**a waandishi wa habari huku kila mmoja akitaka kujua nimepatwa na nin
"Nabil ulipatwa na nin" nilitikisa kichwa nikihashiria sijui kipi kilichonipata. "BABU YAKO NA RAFIKI YAKE MGANGA NDIYO WALIKUTUMIA JINI LA KICHAWI LIKUUWE LAKIN NIMEKUOKOA"
nilisikia sauti kwa mbal ikininong'oneza. babu na rafik yake mganga walinifata na kuniambia "nabil twende ukaoge upate nguvu mjukuu wangu" ' "asante babu,subil kidogo nitaende mwenyewe" niliwajibu akina babu
Hulikuwa usiku mnene wa giza chini ya mti mkubwa sana wa mwembe,kulikuwa na kikao cha watu wengi kilikuwa kikiendelea,hakikuwa kikao salama bali kikao cha wachawi wakijadiliana jinsi ya kuniangamiza. katika kikao hicho watu wengi walikuwa wamekaa chini huku waendesha kikao wanne walikuwa wamekaa mbele,babu na yule mganga walikuwa miongoni mwa waendesha kikao.kikao kilikuwa kimechangamka maana kila mmoja alikuwa anachangia hoja.....
14/12/2015
*PETE YA JINI*
SEHEMU YA #11 ITAENDELEA LEO
05/12/2015
*PETE YA JINI*(10 )
...Hapohapo mwili wote ukasisimuka nikajihisi nipo na hali nyingine ambayo sijawahi kupata maishani,maana mwili ulichangamka kupita kiasi.Ndani ya sekunde kadhaa yule jini alitoweka mazingira yale.Upepo wenye kibaridi ukasikika "vuuh"
Nikiwa bado natembeza macho yangu huku na kule nilijikuta nipo juu ya machela pale nyumbani kwa babu,na umati wa watu umejaa huku mwili wangu umejaa jasho jingi k**a nimemwagiwa maji. Akina mama wengine walikuwa wananipepea kwa khanga zao,kwa awamu hii walikuwa wameniweka nje.nilivuta picha nikapata kufahamu kumbe nilipo ondoka na jini hawakujua bali walijua nimezimia. maana nilisikia sauti za watu wakisemezana "amezinduka,amezinduka" Nilijihisi kupata nguvu za kuinuka,nikajaribu kuinuka taratibu nikafanikiwa, watu walianza kupigwa na putwaa kutokana na hali niliyokuwa nayo lakini nimeweza kuinuka huku nikionekana niliyepata nafuu, nilitazama huku na huku nikamuona babu na yule rafiki yake mganga wakiangaliana kwa mshangao....
11/11/2015
*PETE YA JINI*(09)
..naishi humu baharin(alisota kidole chake kuonyesha bahari) nilipata wasiwasi niliposikia akitamka kuwa yeye ni jini,hofu ilinitanda maana nilikuwa naogopa kwa sababu mim najua majin ni viumbe hatari na katiri ambao ni maadui kwa binadamu. "husiogope nabil" alisema jini. nilijiuliza jina langu amerijuaje
"nipo hapa kwa ajil ya kukulinda" kisha alitoa pete nzuri hiliyokuwa inawaka k**a shaba akanivalisha. Hapa nataka kuelemisha jamii kuwa NAJMAT NNUR KHATMIA huyu ni jini mzuri sana na jini huyu umsaidia mtu katika mambo mengi maishan jini huyu mtu anaweza kuwa nae asijitambue,jini huyu umpa mwanadamu vitu vingi na kumuwezesha kumsaidia kumlinda na hata kumunyanyua kimaisha na kipato jini huyu ukiwa nae mwilin unaweza kupata vitu mbalimbali bila kutarajia unaweza kukutanishwa na mtu au watu ukapata mafanikio makubwa sana.Basi,baada ya kuvalishwa hile PETE YA JINI hapohapo mwili wote ukasisimuka nikajihisi nipo na hali nyingine ambayo sijawahi kupata maishan.... ITAENDELEA
10/11/2015
*PETE YA JINI*(08)
Alinivuta nikainuka na kumfuata nyuma kila anapoelekea.tulikuwa tunatoka eneo hilo kwa kutembea taratibu lakin ingawa kulikuwa na umat mkubwa wa watu hakuna mtu yeyote aliyebahatika kutuona wakati tunaondoka,nilishtuka sana nilipojikuta tupo eneo lenye upepo mkali uliokuwa unavuma taratibu na michanga ya eneo hilo ilikuwa mnyeupe k**a seruji,nilipata picha kuwa haikuwa sehemu nyingine bali pembezoni mwa bahari, ingawa sikuweza kutambua ni bahari gani,hata yule mzee sikuweza kudhubutu kumuhuliza maana muda wote huo nilikuwa nimepigwa na mshangao kwa hayo mauzauza. Yule mzee aliniangalia kwa makin sana akatoa tabasamu "mjukuu wangu,mzimu wako ni mkubwa sana,pia mshukuru allar wako,maana amekukomboa toka mikononi mwa simba" aliniambia yule mzee Nilijitahidi kuondoa woga hili nipate kumuhuliza hata swali moja "kwan wewe ni nani"
"hahahaha.. swali zuri mjukuu wangu,mim naitwa jini NAJMAT NNUR KHATMIA,jini mtawala wa pete na bahati mvuto na muonekano" naishi humu baharin...itaendelea