Sikiza! Lala nayo hii.ππΏ
Huko nyuma ilikuwa mtu anaweza akaanzisha biashara Tanzania aliyoisajili nje ya nchi. Kisha baada ya miaka mitano ya kupata faida kubwa huku akiwa na msamaha wa kodi(Tax Holiday) anaiuza kampuni na kubadilisha jina. Kampuni mpya inaendelea na biashara ileile huku nayo ikijipatia miaka yake mitano ya msamaha wa kodi. Nchi haipati chochote!π
MfanoππΏ
Celtel=>Zain=>Airtel
KC Mstaafu Zitto Kabwe akabadilisha mchezo huu mwaka 2012 akiwa bungeni Dodoma.
Nimekuwekea video. Msikilize yeye mwenyewe uone akisimulia jinsi mchakato wa kutunga sheria ulivyokuwa kwenye bunge lililotawaliwa na CCM. Tangu sheria hiyo itungwe, nchi yetu inafaidika.πͺπΏ
ACT Wazalendo
ACT Wazalendo
ACT Wazalendo ni chama cha siasa kilichoundwa kwa kufuata misingi ya Ujamaa wa Kidemokrasia na chenye shabaha kuu ya kusimamia Mabadiliko na Uwazi nchini.
Official page ya Chama cha ACT-Tanzania
31/05/2026
"Usiweke ukuta kwenye sauti mpya za kidemokrasia."
Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo
Zitto Kabwe
"JKT si chombo cha Muungano. Zanzibar ina idara maalumu yenye hadhi na majukumu yanayofanana na JKT; ambayo ni JKU. Kuwalazimisha vijana wa Zanzibar kujiunga JKT ni kupora mamlaka ya Zanzibar."
Mwenezi wa ACT Wazalendo
Salim Bimani
31/05/2026
TAARIFA KWA UMMA
"JKT si chombo cha Muungano. Tunapinga vijana wa Zanzibar kulazimishwa kujiunga na JKT ndipo wapate ajira kwenye vyombo Muungano k**a vile JWTZ na Idara ya Uhamiaji.
Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo
Salim Bimani
"Nchi ya Benini kwenye kila ekari moja ya pamba, wanavuna kilo 800. Sisi tunavuna kilo 200. Kwa nini mkulima wa Benini apate mara nne ya mkulima wa Tanzania? Sababu sekta ya kilimo haijapewa kipaumbele."
Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo
Zitto Kabwe
"Mwaka wa jana Uganda wameuza nje kahawa za thamani ya USD Bilioni 2.6, lakini sisi ambao tuna mara tatu ya ardhi inayolima kahawa kuliko Uganda, tumepata k**a USD Milioni 150."
Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo
Zitto Kabwe
30/05/2026
"Mamlaka ya dola yasimame k**a ngao ya kulinda utu wa Mwananchi."
Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo
Zitto Kabwe
29/05/2026
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu, amefanya kikao leo 29 Mei, 2026 na Wawakilishi watokanao na ACT Wazalendo katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Kikao hicho kilijadili kazi nzuri zinazofanywa na Wawakilishi hao kwa niaba ya wananchi na kusisitiza kuendelea kusimamia sera na maslahi ya wananchi kwa bidii na maarifa.
29/05/2026
Ameandika mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu
JUKWAA LA MAJADILIANO NA WANACHUO
Wanafunzi wa vyuo vikuu wana wajibu wa kipekee katika mapambano ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ya Taifa letu. Historia inaonesha kuwa vijana wa vyuo vikuu wamekuwa sehemu muhimu ya mabadiliko makubwa katika jamii nyingi duniani.
Kwa dhamana yangu k**a Mbunge, ninakusudia kuanzisha utaratibu wa kukutana mara kwa mara na wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu kwa ajili ya kusikiliza mawazo yao, kujadiliana nao kuhusu masuala ya Taifa, na kutumia fikra pamoja na mapendekezo yao katika kutekeleza wajibu wangu ndani na nje ya Bunge.
Majukwaa haya yatakuwa nafasi ya wazi ya kubadilishana mawazo kuhusu siasa, uchumi, ajira, elimu, Katiba, utawala, demokrasia, maendeleo ya vijana na mustakabali wa nchi yetu.
Iwapo ungependa kushiriki katika majukwaa hayo, tafadhali wasilisha taarifa zifuatazo:
β’ Jina kamili
β’ Chuo unachosoma
β’ Kozi/programu unayosoma
β’ Namba ya simu
Kupitia njia zifuatazo:
1. Inbox:
Facebook: Ado Shaibu
X: Ado Shaibu
Instagram: Ado Shaibu Ado
2. Email:
[email protected]
3. Simu ya Ofisi:
0618 345 158
"Tuna jeografi ambayo nchi nyingi za Kiafrika hazina. Sisi tunaunganisha masoko mawili; soko la SADC na EAC. Tungenyimwa kila kitu, bandari tu ingeweza kuiendesha hii nchi. Je! Tunaitumia hiyo jeografia?"
Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo
Zitto Kabwe
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Website
Address
Dar Es Salaam
