01/06/2026
Maombi huwa tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine, na kinachotofautisha ni uzito wa maneno katika maombi, na uzito huu hutegemea mtazamo wako kwa Mungu katika kuwajibika katika hili unaloliona kwako ni tatizo.
Unapoenda mbele za Mungu lazima roho yako iwe sensitive. Uhalisia uliopo ndani ya moyo wako juu ya mtazamo wako kwa Mungu ndio unaokutengenezea uzito wa mtazamo wako kwa Mungu kuhusu kushughulika na case yako.
Mfumo ambao Mungu ameutengeneza kwenye moyo wako ni wewe kuwa na mahusiano mazuri na yeye.
Neno la Mungu linasema kuwa maandalio ya moyo ni ya mwanadamu, sio ya Mungu.
Kukabidhi mwezi maana yake ni kuuk**ata mwezi, unajiandaaje kuupokea na kuenenda kwenye huu mwezi mpya?
Chochote kilichoandikwa nyuma yake kuna roho, k**a kuna kitu kimeandikwa hata ujitahidi vipi, k**a hauna msaada wa Mungu huwezi kuona matokeo.
Ni kitu gani kimeandikwa kinyume na maisha yako kinyume na kufanikiwa? Maana mafanikio yanatakiwa kuonekanika na kushikika.
Ardhi inaweza kuandika habari kinyume na mtu, na popote atakapoenda as long as anakanyaga ardhi, hawezi kufanikiwa.
π Yeremia 22:30
BWANA asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.
Leo haijalishi nini kiliandikwa kinyume na wewe katika ardhi, tumeomba rehema lakini pia kuyafuta hayo matamko kwa Damu ya Yesu!
01/06/2026
WOMEN IN ACTION 2026π₯
Imerudi tena!
Na awamu hii idara ya wanawake imekuandalia mambo motomoto zaidi.
Kwa ambaye umeshawahi kuhudhuria hii utakuwa ni shahidi mzuri kwa jinsi ambavyo maisha ya watu yamebadilika kupitia hii event, wewe ambaye hujawahi kuhudhuria tunakushauri awamu hii usikose!
Dress code: Shade of Purple
Entrance: TSH 30,000
Date: 01st, August 2026
Event itafanyika hapahapa Reality of Christ Church, Sinza Mori.
Wahi ujipatie ticket yako mapema!
"Women in Action, Let's Connect"
31/05/2026
SIKU 5 ZA KUFUNGA NA KUOMBA (DAY ONE)π₯
Tunamshukuru Mungu kwa neema hii aliyotupa ya kuwa na mfungo katika majira haya.
Na kesho ikiwa siku ya kwanza tutaongozwa na Neno la Mungu kutoka;
π 1 Wathesalonike 3:9, Yeremia 22:30
Na tutakuwa na prayer points zifuatazo;
1. Kumshukuru Mungu kwa yale aliyotukirimia kwenye kila hatua
2. Kuomba rehema juu ya kila kilichoandikwa kinyume katika kuzaa(matokeo) na mafanikio.
Jioni kuanzia saa kumi na moja tutakutana hapa Reality of Christ Church, Sinza Mori karibu na ofisi za TAMWA kwa ajili ya maombi ya pamoja.
Tutakuwa mubashara pia kupitia ukurasa wetu wa YouTube wenye jina REALITY OF CHRIST CHURCH na kupitia ROC TV.
Karibu sana na Mungu akubariki.
31/05/2026
2. Maneno yana nguvu kuliko vita ya duniani.
1 Wafalme 19:2-4
Kwanini aliogopa maneno ya Yezebeli? Mtu ambaye alikuwa na nguvu kubwa sana ya Mungu maana alifanya makubwa.
Kumbuka Eliya alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kiroho na aliona mauti. Kuna watu wakitamka maneno yanakuja na umbo.
Ndio maana, kuna maneno ulishawahi kuyasikia na yakakutisha sana...maana yake yalikuja na umbo la hofu.
1 Samuel 17:1-11
Pande zote walikuwa wameshajiandaa na vita, ila kabla hawajaanza akatoka Goliath na kuanza kuwatisha. Waisraeli walichokosea ni kukaa na kumsikiliza kitu Goliath anasema.
Kosa kubwa ambalo watu wanalifanya ni kumsikiliza adui, k**a umeamua kupambana vita hakikisha unapigana hadi unamaliza.
Ukisoma mstari wa 9-11
Pata picha mmeinuka kwa ajili ya kupigana vita, halafu ghafla tu anainuka huyu Goliath. Ilikuwa ni vita ya jeshi kwa jeshi, kwanini kwa wafilisti ainuke mmoja? Na alitoa maneno ambayo yakavaa umbo la hofu na waisraeli wakaogopa sana.
Jiulize, ni maneno gani ambayo huwa unakutana nayo na yakabeba umbo la hofu?
Hofu kwa waisraeli ilikuwa kubwa, hadi Daudi alipokuja kuinuka.
Kuna maneno yanabeba maumbo, ndio maana unatakiwa kuwa makini sana unapomsikiliza mtu au unapogombana na mtu maana kuna vitu anaweza kuviongea na vikakuletea shida sana.
Usiipuuzie nguvu ya maneno na wala usiichukulie kirahisi.
Usiwe mwepesi wa kutamka na usiwe mwepesi wa kuchukulia rahisi maneno unayotamkiwa.
31/05/2026
NGUVU YA MANENO YA KINYWA CHAKO
Ili kitu kitokee katika ulimwengu wa mwili ni lazima kitokee kwanza katika ulimwengu wa roho kwanza.
Na katika ulimwengu wa roho kuna pande mbili;
Upande wa Nuru - Mungu
Upande wa giza - Shetani
Pande hizi zote mbili zinatumia maneno, upande wa giza wanatumia manuizo, upande wa nuru tunatumia maneno.
Mfano; mtu akienda kwa mganga akapewa vitu akaweka njia panda, k**a ukiviondoa tu bila kuondoa manuizo aliyotamka kabla wakati anaweka basi jua tu hakuna kitu umefanya.
Katika ulimwengu wa roho kwa sisi Wakristo tunaita maombi, ndio maana ni changamoto sana kuomba kimyakimya bila kutamka.
Marko 11:12-14,20-21
K**a Yesu alijibu akauambia huu mti ina maana kuna kitu huu mti ulitamka. Yesu akaulaani akasema kuwa mtu asile matunda kutoka kwenye ule mti tena, na ndivyo ilivyokuwa.
Maneno unayotamka yana nguvu kubwa sana katika ulimwengu wa roho.
Mwanzo 1:1-3
Giza lilikuwepo na Roho wa Mungu alikuwepo lakini hakuna chochote kilichotokea hadi Mungu alipotamka. Roho Mtakatifu anaweza akashuka sehemu lakini kuna Neno linatakiwa kutamkwa kwanza ili Roho Mtakatifu aingie kwenye kazi ya kukifanya kile kitu kiwe halisi. Na Mtumishi wa Mungu anatakiwa kuwa sensitive kiroho, maana atakachotamka sawasawa na mapenzi ya Mungu Roho Mtakatifu ataingia kazini kuhakikisha kinatokea.
Mungu akatamka iwe Nuru na kukawa na Nuru. Kwahiyo kuna matamko yanaweza kukitoa kitu kwenye ulimwengu wa roho kuja kwenye ulimwengu wa mwili.
Tamko lolote linalotolewa na mtu aliyekuzidi kiroho(kiumri/dimension katika ulimwengu wa roho) lina maana kubwa sana maana atakachokisema kitaenda kuwa. Na hii ni kwa pande zote mbili, wa giza au wa nuru.
1. Maneno yoyote yanayotamkwa ni roho, na hayo maneno yanaweza kuwa na nguvu kubwa.
Yohana 6:63
Maneno yana roho ndani yake, yanaweza kubariki au kulaani.
Hata kwenye unabii kuna wakati anaweza akaona na akakwambia, kuna wakati haoni ila anakiumba, na hiki kitu kitatokea katika ulimwengu wa mwili.
Watumishi wote wana uwezo wa kuumba, lakini sio wote wana uwezo wa kuona.
31/05/2026
SHUHUDA NA SHUKRANI π₯
Mungu anapotenda kitu kwako huwa sio kwa ajili yako tu, huwa ni kwa ajili ya watu wengine pia ambao wanasubiri kusikia Mungu alichokutendea ili nao imani zao ziinuke na atende na kwao pia.
Leo kuna ambao wamerudi kumshukuru Mungu kwa yale aliyoyatenda kwenye maisha yako.
Kwa wewe ambaye unamuamini Mungu kwa ajili ya jambo fulani, akatende na kwako pia!
31/05/2026
Mungu huwa unamsifu ukiwa wapi? Ukiwa na hali gani?
Msifu Mungu wakati wote maana kupitia sifa Yeye hutenda makuu maana maandiko yanasema Yeye huketi kwenye sifa.
31/05/2026
Tulipata nafasi nzuri ya kuandaa ibada, tuliongozwa na Mtumishi wa Mungu Minister Sia Kyando.
Ametuongoza katika maombi mazuri sana na tunajua kabisa kwa maandalio haya, Mungu anaenda kufanya kitu kikubwa sana siku ya leo.
30/05/2026
π
SUNDAY SERVICE β 31 MAY 2026 π
Karibu sana katika Sunday Service ya kesho, Jumapili tarehe 31 Mei 2026, kuanzia saa 3:00 kamili asubuhi hapa Reality of Christ β Sinza Mori.
Tutakuwa na muda maalum wa kuabudu, kuomba na kujifunza Neno la Mungu ambalo lina uwezo wa kubadilisha maisha yako. Usikubali kukosa ibada hii ya kipekee.
πReality of Christ, Sinza Mori (Karibu na Ofisi za TAMWA)
β° Muda: Saa 3:00 Asubuhi
π΄ Vilevile tutakuwa LIVE kupitia:
πΊ ROC TV
βΆοΈ Reality of Christ Church β YouTube Channel
Mwalike na mwingine aje apokee kile ambacho Mungu ameandaa kwa ajili yake.
Karibu sana, Mungu akubariki! π
30/05/2026
Wakati Mungu anamtengeneza mwanadamu, hakuishia tu kwamba ailime ardhi, lakini pia alimpa maelekezo ya nini ale na nini asile, lakini pia alimuhakikishia uzima.
Leo hii kwenye nyumba ya boss wako ambapo Mungu amekuweka jua kabisa wewe ni suluhisho hapo, wengine ni kuwasaidia watoto wao, wengine dukani, etc
Na hawa maboss unatakiwa kujua kuna waliofunga, wapo walioomba na wewe ni majibu ya maombi yake. Jua kabisa haupo hapo kwa bahati mbaya.
Na ukiwa hapo waheshimu uliowakuta hapo, na fanya kazi vizuri. Neno la Mungu linasema kuwa chochote ambacho mikono yako imepata kukifanya kifanye kwa moyo, sio k**a unamfanyia mwanadamu bali k**a unamfanyia Mungu.
Mungu hajakuweka kwenye hiyo nyumba kwa bahati mbaya, kuna baraka zako zipo hapo.
Kumbuka zile nguvu za giza kwenye ukoo zina tabia ya kufuatilia, ndio maana leo hii unajisikia tu hutaki kukaa hapo, na hata ukiulizwa sababu ya msingi hauna. Nini kinapelekea wewe kuwa hivyo?
π Mwanzo 3:1-6
Shetani pia anaweza kuja k**a nyoka. Ukiwa unaota sana nyoka jua kabisa adui yupo kazini. Na kuna wengine wametoka kwenye familia ambazo wamehakikishiwa kuwa nyoka huyo ni salama, anatunza familia wala haumi...huyu nyoka ni adui!
Hawa anaongea na nyoka, nyoka anaanza kutengeneza mazingira ya kuwatoa kwenye eneo sahihi...na ndicho ambacho adui hufanya, atatengeneza scenario ambayo ukiifuata hii itakutoa kwenye sehemu sahihi.
Na adui alivyo mjanja, anaweza kuja kwako kupitia huyo Mangi, kupitia huyo rafiki.
Ukisoma mstari wa sita utaona namna ambavyo mwanamke alishawishika, na kupitia hivyo kutolewa kwenye kusudi ni rahisi. Kuna watu ambao kuna vijana waliwaambia waache kazi na watawaoa, leo wameacha, wameolewa na sasa wana watoto. Kazi ya mwanamke ni kuwa msaidizi, pale ambapo mume atashindwa mwanamke unatakiwa kusaidia...wewe upo kwenye nafasi nzuri ya kuweza kusaidia? Vipi kuhusu kusudi lako?
Mwanzo 3:6-8
Baada ya kula tunda kilichofuata ni aibu, wakagundua kuwa wapo uchi.
Huyo adui alifanikiwa kuwatoa Adam na Hawa kwenye eneo sahihi, leo popote ambapo adui anataka kukutoa Mungu ataenda kukufungua!