National Sports Council of Tanzania

National Sports Council of Tanzania

Share

Official page of The National Sports Council of Tanzania which was enacted by the Act of the Parliament of the United Republic of Tanzania

FUNCTIONS OF THE NATIONAL SPORTS COUNCIL OF TANZANIA
The National Sports Council of Tanzania was enacted by the Act of the Parliament of the United Republic of Tanzania No: 12 of 1967 and its amendments Act No: 6 of 1971. The act gives the council a supreme power to supervise all kind of sports in the country both professional and amateur. In summary, the National Council of Tanzania does the foll

11/11/2023

TIMU YA TAIFA YA KRIKETI WANAWAKE KUWEKA KAMBI HONG KONG CHINA KUJIANDAA NA MASHINDANO YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA MWEZI DISEMBA

#Mashindano ya Vishale Afrika Masharika#

*Wazazi watakiwa kuwapa watoto wao nafasi ya kushiriki michezo mbalimbali*

Afisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Charles Maguzu amewaasa wazazi kutokuwa wabaguzi wa michezo ambayo wanataka watoto wao washiriki badala yake wawaruhusu watoto hao kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa Vishale (Darts).

Maguzu ameyasema hayo siku ya leo Novemba 09, 2023 wakati wa hafla ya kukabidhi bendera kwa kikosi cha timu ya Taifa ya Mchezo wa vishale ambacho kinatarajiwa leo kwenda jijini Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano ya Afrika Mashariki yanayoanza tarehe 10 hadi Novemba 12, 2023.

Maguzu alisema kuwa matarajio ya Serikali ni kwamba kikosi hicho kitarudi na ushindi na kueleza kwamba wana imani wachezaji waliopata fursa wamepatikana kihalali na watakwenda kufanya vizuri na kurudi na ushindi.

"Kwa niaba ya Serikali tuwapongeze viongozi kwa juhudi za kukuza mchezo huu na wadhamini waendelee kuwaamini  na kuwashika mkono na kuwataka wakafanye vizuri katika mashindano hayo," alisema Maguzu .

Aidha, ametoa rai kwa viongozi wa mchezo huo kuhakikisha unaenea kwenye maeneo mbalimbali na kuchezwa katika ngazi ya shule Ili kupata wachezaji wengi watakaoshiriki Mashindano ya ndani na kimataifa.

Naye Nahodha wa timu  yaTaifa ya Mchezo  huo Johakim Mollel, àmesema wamejipanga kufanya vizuri katika mashindano hayo na kueleza kuwa, wanakwenda kupambana, kushindana na sio kushiriki katika mashindano hayo.

Msafara wa kikosi hicho unaundwa na watu nane wakiwemo wachezaji sita wanaume wakiwa wanne ambao ni Noah Issa, Johakim Mollel, Yohana Kisau na  John Mlay huku wanawake wakiwa wawili Happynes Modah na Irene Kihupi sambamba na viongozi wawili.

Mashindano hayo yatahusisha nchi tano ikiwemo mwenyeji Kenya, Uganda Tanzania, Rwanda na Burundi. 09/11/2023

vishale yaagwa

#Mashindano ya Vishale Afrika Masharika# *Wazazi watakiwa kuwapa watoto wao nafasi ya kushiriki michezo mbalimbali* Afisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Charles Maguzu amewaasa wazazi kutokuwa wabaguzi wa michezo ambayo wanataka watoto wao washiriki badala yake wawaruhusu watoto hao kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo mchezo wa Vishale (Darts). Maguzu ameyasema hayo siku ya leo Novemba 09, 2023 wakati wa hafla ya kukabidhi bendera kwa kikosi cha timu ya Taifa ya Mchezo wa vishale ambacho kinatarajiwa leo kwenda jijini Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano ya Afrika Mashariki yanayoanza tarehe 10 hadi Novemba 12, 2023. Maguzu alisema kuwa matarajio ya Serikali ni kwamba kikosi hicho kitarudi na ushindi na kueleza kwamba wana imani wachezaji waliopata fursa wamepatikana kihalali na watakwenda kufanya vizuri na kurudi na ushindi. "Kwa niaba ya Serikali tuwapongeze viongozi kwa juhudi za kukuza mchezo huu na wadhamini waendelee kuwaamini na kuwashika mkono na kuwataka wakafanye vizuri katika mashindano hayo," alisema Maguzu . Aidha, ametoa rai kwa viongozi wa mchezo huo kuhakikisha unaenea kwenye maeneo mbalimbali na kuchezwa katika ngazi ya shule Ili kupata wachezaji wengi watakaoshiriki Mashindano ya ndani na kimataifa. Naye Nahodha wa timu yaTaifa ya Mchezo huo Johakim Mollel, àmesema wamejipanga kufanya vizuri katika mashindano hayo na kueleza kuwa, wanakwenda kupambana, kushindana na sio kushiriki katika mashindano hayo. Msafara wa kikosi hicho unaundwa na watu nane wakiwemo wachezaji sita wanaume wakiwa wanne ambao ni Noah Issa, Johakim Mollel, Yohana Kisau na John Mlay huku wanawake wakiwa wawili Happynes Modah na Irene Kihupi sambamba na viongozi wawili. Mashindano hayo yatahusisha nchi tano ikiwemo mwenyeji Kenya, Uganda Tanzania, Rwanda na Burundi.

04/11/2023

Waandaaji wa mbio watakiwa kushirikisha Watu wenye mahitaji maalum.

04/11/2023

Msimu wa Tano wa Mashindano ya Riadha ya Wanawake Novemba 24 - 26, 2023 Jijini Dar es salaam.

04/11/2023

Mwanamke Afya Marathon(MAM MARATHON)

02/11/2023

Msimu wa tano mashindano ya riadha Wanawake(Ladies First)

Photos from National Sports Council of Tanzania's post 01/11/2023

Katibu Mkuu Msigwa ateta na Mabondia

Katibu mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa mapema asubuhi ya Novemba Mosi amekutana mabondia walioshinda mapambano yao ya mikanda ya ubingwa wa Baraza la Ngumi Duniani, WBC na ubingwa wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini TPBRC katika ofisi za Baraza la Michezo BMT.

Mabondia hao ambao ni Fadhili Majiha aliyeshinda mkanda wa Ubingwa wa WBC Afrika alioshinda kwa kumshinda Bongani Mahlangu wa Afrika Kusini wakati Pius Mpenda akishinda mkanda wa WBC Peace nchini Uturuki kwa kumchapa Dauren Yeleussino wa Kazakhstan huku Ibrahim Class akishinda ubingwa wa Taifa wa TPBRC dhidi ya Xiao Tau Su wa China.

Msigwa amewataka mabondia hao kuhakikisha wanaweza kujitunza ili waendelee kufanya vizuri katika mapambano yao wanayocheza kimataifa huku akitoa ahadi ya serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuwaunga mkono kwenye mchezo huo.

Photos from National Sports Council of Tanzania's post 01/11/2023

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa akipokea taarifa fupi ya BMT kutoka kwa Katibu Mtendaji Bi. Neema Msitha leo Novemba 01, 2023 wakati alipokutana na Menejimenti ya Baraza hilo akiwa katika ziara yake ya kwanza katika taasisi hiyo baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais wa awamu sita Dkt. Samia Suluhu kuongoza Wizara hiyo.

Photos from National Sports Council of Tanzania's post 01/11/2023

Katibu Mkuu Gerson Msigwa Novemba Mosi, 2023 akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wakati wa ziara yake kikazi katika Taasisi hiyo inayosimamia michezo siku chache baada ya kuteuliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongoza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

01/11/2023

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa, leo tarehe 1 Novemba, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa, amewapongeza mabondia Pius Mpenda aliyeshinda mkanda wa WBC Peace, Fadhil Majiha aliyeshinda mkanda wa WBC Africa na Ibrahim Class aliyeshinda mkanda wa TPBRC katika mapambano yao waliyocheza tarehe 28 na 29 Oktoba, 2023.

31/10/2023

TAFF wapokea vifaa vya michezo kutoka K4S

Want your business to be the top-listed Government Service in Dar es Salam?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Address


MKAPA STADIUM, 2nd Floor, TAIFA Road, DAR-ES-SALAAM
Dar Es Salam
MKAPANATIONALSTADIUM

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:00
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 03:00
Friday 07:30 - 15:30
Sunday 07:30 - 15:30