Follow instagram page ya Mfuko
ppfpensions.official ili kuweza kupata habari mbalimbali za shughuli za kila siku za Mfuko.
Maoni ya wanachama yatapokelewa na maswali mbalimbali yatajibiwa kupitia ukurasa huo.
Jiunge na PPF Kwa maisha bora ya sasa na ya baadaye.
PPF Pensions FUND
PPF is the oldest and the most experienced Pension Fund under the defined benefit system in Tanzania. The Fund was established in July 1978.
PPF Pensions Fund was established by the PPF Pensions Fund Act [CAP 372 R.E. 2002] as amended from time to time to provide pensions and other related terminal benefits to all employees from the formal and informal sectors of the economy.
Tembelea Tovuti ya Mfuko: www.ppf.or.tz
Istagram page:ppfpensionsfund.official
page:ppfpensionsfund
PPF Pensions Fund The PPF Pensions Fund was established by the PPF Pensions Fund Act [Cap 372 R.E 2002] as amended time to time with the objective of providing pensions and other related terminal benefits to all employees in the formal and informal sectors.
Mkutano wa 26 wa wanachama na wadau wa PPF
Mada kuu:" Tanzania ya viwanda:Umuhimu na wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii".
Mkutano utafanyika katika ukumbi wa Simba, AICC-Arusha Tarehe:23 na 24 Machi 2017.
Jiunge na PPF kwa maisha bora ya sasa na ya baadaye
Ongezeko na Ukuaji wa thamani ya Mfuko unatokana na vitu vifuatavyo:-
1. Ukusanyaji wa Michango kwa wakati
2. Uwekezaji Bora na salama wa michango
3. Utawala bora na
4. Ushirikiano mzuri kati ya Mfuko na wadau wake
Mfuko umeendelea kukua mwaka hadi mwaka na kuendelea kulipa Mafao kwa wanachama wake bila ya kukopa au kuuza rasilimali zake.
" Jiunge na PPF kwa maisha bora ya sasa na ya baadaye".
Katika kitabu cha Ninastaafu KAZI, Sistaafu Maisha (I Retire from Work and not life) cha mwandishi Mkumbo Mitula; Mwaka 2003 asilimia 4% ya Idadi ya watu walikuwa Wazee. Mwaka 2012 idadi hii iliongezeka na kufikia 5.6%. Inakadiriwa kuwa hadi mwaka 2050 idadi hii itaongezeka na kufikia asilimia 10% (Takribani watu millioni 8.3 ya idadi ya watu)
Mojawapo ya vigezo vinavyomwezesha mwanachama kupata pensheni iliyo bora katika Mafao ya Uzeeni ni:-
1.Idadi ya miezi Mwanachama aliyochangia katika Mfuko.
2. Wastani wa mishahara bora ya miaka mitatu katika kipindi cha miaka kumi ya mwisho ya uchangiaji wa mwanachama katika Mfuko
PPF Pensions Fund
ISO 9001:2008 Certified
Mfuko unatoa huduma zake kwa kuzingatia viwango vyenye ubora wa kimataifa wenye misingi ya ISO 9001 Viwango vya mwaka 2008.
Mfuko pia unawakaribisha kujiunga na Instagram page ya Mfuko ambayo ni ppfpensionsfund.official na kuweza kupata taarifa na ufafanuzi mbalimbali ambapo pia maswali yenu yatajibiwa katika Ukurasa huo.
Uanachama wa Mfuko
Uanachama wa Mfuko umegawanyika katika sehemu mbili k**a ifuatavyo katika Sekta rasmi
1.Mwajiriwa
Umri wa Mwanachama miaka 18-45, walio katika ajira za kudumu, walio katika ajira ya muda maalumu (contract), wafanyakazi waliopo kwenye probation, walioajiriwa tena baada ya kuacha kazi au mtu binafsi. Uanachama haukomi kwa kuhama kutoka mwajiri mmoja kwenda mwingine-kisheria, uanachama huendelezwa
2.Mwajiri
Waajiri wanaoandikishwa
Sekta rasmi na Sekta isiyo rasmi, Mashirika ya umma, taasisi za Serikali, Makampuni Binafsi, Makampuni yoyote yaliyosajiliwa au kuandikishwa, Taasisi za dini, mashule n.k
Viwango vya uchangiaji
Mfumo wa Asili Wa Pensheni
Moja kati ya viwango vifuatavyo kinaweza kutumika
a. 10% kwa mfanyakazi na 10% kwa mwajiri, au
b. 5% kwa mfanyakazi na 15% kwa mwajiri.
Michango hii hukatwa katika mshahara wa kila mfanyakazi kwa kutumia kiwango kilichokubalika na mwajiri ana wajibu wa kisheria kujazia kiwango kilichobakia. Michango hii inatakiwa kuwasilishwa na mwajiri katika Mfuko ndani ya siku 30 za mwezi unaofuatia.
Kuchelewa au kutowasilishwa michango ya wanachama ni kosa la jinai. Mwajiri atatozwa adhabu ya asilimia tano (5%) kwa kila michango iliyocheleweshwa kila mwezi kwa kipindi ambacho michango hiyo imecheleweshwa.
Pamoja na adhabu ya asilimiia tano kwa kila mchango uliocheleweshwa, hatua za kisheria huchukuliwa dhidi ya mwajiri anayechelesha michango
Majukumu ya Mfuko wa Pensheni wa PPF
1. Kuandikisha wanachama
2. Kukusanya Michango
3. Kuwekeza Michango iliyokusanywa ili kutunza thamani ya Fedha
4.Kulipa Mafao yaliyo bora ya Hifadhi ya Jamii kwa wanachama
Nia yetu ni kuboresha utendaji katika kila nyanja ya shughuli zetu za utendaji kwa njia ya utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa ubora wa kimataifa wenye misingi ya ISO 9001 viwango vya mwaka 2008.
Jiunge na PPF kwa maisha bora ya sasa na baadaye
Hifadhi ya Jamii ni nini?
Ni utaratibu/Mpango wa kuhakikisha kuwa mwananchi anapata hifadhi baada ya kuishiwa uwezo wa mwili kufanya kazi tutokana na uzee, ugonjwa au kufariki kwa aliyekuwa analeta kipato katika familia. Hifadhi za jamii ni programu za lazima zilizoanzishwa kisheria na huendeshwa kwa kuzingatia sheria ambapo watu huchangia sehemu ya Fedha kupitia mwajiri wao/Kujichangia na kuziweka katika Mfuko wa Pensheni
Wanachama gani wanaruhusiwa kwa mujibu wa sheria kuwa katika Mfumo wa Asili wa Pensheni?
Wanachama wanaoruhusiwa kwa mujibu wa sheria kuwa katika Mfumo wa Asili wa Pensheni na kufaidika na Mafao saba yanayotolewa kupitia Mfumo huo ni Watanzania wote wenye umri kuanzia miaka 18-45. Wafanyakazi wote wanaopata ajira wakiwa na umri wa miaka 45 na kuendelea hawataruhusiwa kuandikishwa katika Mfumo wa Asili wa Pensheni na badala yake wataandikishwa katika Mfumo wa uwekezaji amana.
Mfuko unapenda kuwasisitiza wale wote wanaoruhusiwa na sheria kuwa katika Mfumo huu kutumia nafasi hiyo vyema ipasavyo kwa faida yao, familia zao na Taifa kwa ujumla.
Mawasiliano Rasmi ya Mfuko;
Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Pensheni wa PPF
PPF House, Morogoro Rd/Samora Av., S.L.P 72473, Dar es Salaam, Tanzania
Simu +255 222110642/ +255 22 2113919-22/ +255 754 005756
Barua Pepe:[email protected], [email protected]
Tovuti;www.ppf.or.tz
Instagram page;ppfpensionsfund.official
Click here to claim your Sponsored Listing.
Location
Category
Telephone
Website
Address
PPF House Morogoro Rd/Samora Av . P. Box 72473
Dar Es Salam
Opening Hours
| Monday | 08:00 - 17:00 |
| Tuesday | 08:00 - 17:00 |
| Wednesday | 08:00 - 17:00 |
| Thursday | 08:00 - 17:00 |
| Friday | 08:00 - 17:00 |
