Wa usawa

Wa usawa

Share

politician

27/04/2025

Hii ni nchi yetu sote, wenye mamlaka tendeni haki.
Acheni kuonea watu kwa namna k**a hii.

20/03/2023

Hii ni picha ya sehemu ya utumbo mdogo (ileostomy) ambayo Minza anaitumia kwa ajili ya kupata choo, baada ya kufanyiwa upasuaji. Anatakiwa kutumia mifuko maalumu (Stoma/colostomy bags) ili kuepusha kupata maambukizi. Tumepata mifuko 50 hadi sasa. Mifuko hiyo ni disposable, means inaweza kutumika mara 1 tu na kutupwa. Mifuko 50 aliyopata inaweza kutumika hardly kwa mwezi mmoja.

Hivyo inahitajika mifuko zaidi. Kwa yeyote mwenye pharmacy na anaweza kujitolea mifuko hii, tafadhali fanya hivyo k**a sehemu ya sadaka yako. Minza akiruhusiwa kutoka hospitali akaenda kutumia matambara, atapata infection, na kazi yote ya matibabu tuliyofanya itakua kazi bure.

Jambo la pili ni kuhusu gharama za matibabu anazodaiwa Bugando 3.4M. Hadi sasa kiasi kilichochangwa ni TZS 2.5M, bado 900K kukamilisha deni hilo la hospitali. Matarajio ni fedha hiyo ilipwe kesho asubuhi ili Minza aende nyumbani. Kuwa sehemu ya kurudisha tabasamu la Minza.

Tuma sadaka yako kwenda M-PESA 0752581983, Tigopesa 0719744954, CRDB 0150633516500 GIFTED HEARTS FOUNDATION.

23/02/2023

Ameandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____
Kwaresma imeanza. Ukifunga, Umfungue Mwingine. Safari ya siku 40 kwenda Galilaya, imeanza (jana). Hii ni KWARESMA. Ukifunga kula, umfungulie aliyefunga kwa kukosa chakula. Bajeti ya chakula mpe mhitaji maskini.

Ukifunga kunywa soda/bia. Bajeti mnunulie soda aliyeshindwa kununua soda. Mnunulie maji yeye aliye na kiu, anayeona maji ya Dasani ni anasa (kwa kushindwa kumudu gharama).

Utambue kuna watu hulazimika kufunga bila kusubiri Kwaresma. Siku inaisha hawajatia kitu mdomoni, asubuhi mchana au jioni, kutokana na hali duni ya maisha. Kufunga bila kuwafungua hao ni sawa na kufuata masharti ya daktari ili kupunguza uzito. Huo ni uchoyo mambo leo.

Ukifunga kumbuka kuwafungua wengine. Wafungue wale waliofunga bila kusubiri Kwaresma. Mathayo 22:36-39.

28/10/2022
01/10/2022
22/09/2022

Ukisikia za uso, zile za uso zenyewe ndo hizi sasa...

Want your business to be the top-listed Government Service in Dodoma?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Website

Address


Dodoma